Elections 2010 Wengi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutopiga kura 2010

Mwanzo » Habari
60,000 vyuo vikuu hawatapiga kura
NA WAANDISHI WETU
4th October 2010
B-pepe
Chapa
Maoni
Wako likizo lakini walijiandikisha vyuoni
Havitafunguliwa kabla ya Uchaguzi Mkuu
Kiravu asema hawana la kufanya

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imepigilia msumari wa mwisho juu ya hatma ya upigaji kura kwa zaidi ya wanafunzi 60,000 wa vyuo vikuu nchini ambao wako likizo lakini wakiwa wamejiandikisha kwenye vituo vilivyo vyuoni kwao.
Mkurugenzi wa Nec, Rajabu Kiravu, akizungumza na NIPASHE jana alisema hawana cha kufanya juu ya wanafunzi walioko likizo kwa kuwa mchakato wa kuboreshwa kwa daftari la wapigakura ulishafungwa, kwa maana hiyo wanafunzi hao hawatapiga kura.
NIPASHE ilimtafuta Kiravu kuzungumzia habari hizo baada ya kufanyika kwa kongangamamo la wahitimu na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu lililofanyika hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi hao walitoa rai kwa serikali kufanya jambo moja kati ya mawili ili kuwapa fursa ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Walitaka ama waruhusiwe kupiga kura wakiwa likizo kwa kuwekewa utaratibu maalum huko waliko, au vyuo vifunguliwe kabla ya Oktoba 31, mwaka huu ili wapate fursa hiyo kwani walijiandisha wakiwa vyuoni.
Wanafunzi hao na wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini, walitoa malalamiko hayo jana kwenye kongamano ambalo lilijadili masuala ya uchaguzi mkuu.
Walisema kama hawatapewa fursa hiyo, watakuwa wananyima haki yao ya msingi kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba ya Tanzania ambayo inatoa haki kwa kila raia kuchagua kiongozi anayemtaka.
Kwa kawaida vyuo vya elimu ya juu nchini hufunguliwa kwa muhula wa kwanza wa masomo kati ya Septemba na Oktoba, lakini mwaka huu vyuo hivyo vitafunguliwa Novemba baada ya Uchaguzi Mkuu.
Kiravu alisema Nec ilitoa muda kwa wananchi wote wakiwemo wanafunzi kubadilisha taarifa zao ili kupiga kura katika maeneo yao mapya na kwamba kama hawakufanya hivyo wao hawawezi kutoa muda mwingine kwa kuwa daftari limeshafungwa.
“Tuliishatoa nafasi tena kwa kutangaza kwa wananchi wakiwemo wanafunzi kwamba mtu anayetaka kubadilisha taarifa zake wafanye hivyo, lakini kama hata hao wanafunzi walishindwa kufanya hivyo daftari limeishafungwa na sasa tunafanya mambo mengine alisema,” Kiravu.
Akizungumza katika kongamano la jana, mgombea wa ubunge Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam kupitia Chadema, John Mnyika, alisema, mwaka huu watawatumia wanafunzi wa vyuo vikuu kama mawakala ili kuhakikisha wanalinda kura zao zisiibwe.
Aidha, alisema chama chake katika jimbo lake kitaweka mawakala ambao ni wafanyakazi pamoja na wale watakaoteuliwa na viongozi wa kata wa Chadema na kwamba watakuwa na mawakala wa aina tatu wakiwemo wafanyakazi.
Kuhusu serikali kufungua vyuo vya elimu ya juu kabla ya uchaguzi mkuu, Mnyika aliitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuharakisha mpango huo ili kuwawezesha wanafunzi kupiga kura maeneo waliyojiandikishia.
Alidai kuwa serikali imefanya makusudi kuchelewesha kufungua vyuo kwa maagizo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili wanafunzi wasiweze kukipigia kura Chadema na kuongeza kwamba mabadiliko ya kweli katika nchi hii yataletwa na wasomi.
Alisema kama wasomi wasipoleta mabadiliko kwa kuindoa CCM madarakani watakuwa wanawasaliti wananchi hasa waliopo vijijini.
Alijigamba kuwa wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo hawakulipwa posho wala kusafirishwa kwa mabasi kama inavyofanya CCM katika mikutano yao na kwamba walikwenda wenyewe hali inayoonyesha kwamba wana uzalendo wa kweli na mapenzi kwa Chadema.
Mnyika ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema ni vigumu wananchi kuendelea kukiamini CCM kwa kuwa ahadi walizotoa mwaka 2005 wameshindwa kuzitekeleza na badala yake wameendelea kutoa zingine mwaka huu.
Aliwataka vijana hao kuhakikisha kila mmoja anashawishi watu wanne hadi watano ili kukipigia kura Chadema mwaka huu ili kukiwezesha kuingia madarakani na kuunda serikali.
Mnyika aligusa hisia za wanafunzi hao na kuwafanya wapandwe na jazba baada ya kuwaambia kuwa Chadema ikiingia madarakani kitu cha kwanza itakachofanya ni kuvunja Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) kwa kuwa imeshindwa kukidhi mahitaji wa wanafunzi na kuunda mMamlaka ya kugharamia masomo ya elimu ya juu.
Alisema mamlaka hiyo itakuwa inasomesha wanafunzi wote elimu ya juu bure ambapo wataunda matawi katika kila mkoa ambayo yatakuwa yanashughulikia utoaji wa elimu ya juu bure kwa wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi hao wakichangia mada kwenye kongamano hilo walisema ikiwa serikali haitafungua vyuo itakuwa inawanyima haki yao ya kikatiba.
Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi kutoka Chuo cha Biashara (CBE), Lutashobya Lutashobya, alisema Nec inatakiwa kuliangalia suala hilo mapema iwezekavyo ili wanafunzi nao wapate haki yao ya kupiga kura.
“Tunashangaa kwa nini vyuo havifunguliwi mapema, CCM inataka kuhujumu haki yetu ya kikatiba ya kupiga kura na kumchagua kiongozi bora, lakini hili likishindikana itabidi tuhamasishane sisi kwa sisi ili kuwashawishi wananchi wanaovaa nguo za rangi ya kijani ambao wanaoipenda Chadema, lakini wanaogopa kusema wazi ili wakipigie kura chama hicho,” alisema.
Mhitimu mwingine kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Docas Mnanga, aliitaka Chadema kutimiza ahadi yao ya kuvunja haraka HELSB na kuunda mamlaka ya kugharimia masomo ya elimu ya juu.
Aliunga mkono hoja ya Chadema ya kuvunja bodi hiyo kwa madai kuwa inachangia kuwepo vitendo vya rushwa na imeshindwa kuonyesha ufanisi tangu ilipoundwa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitila Mkumbo, alisema Ilani ya chama chochote cha siasa inatakiwa kutoa majibu kwa wananchi kuwa itawafanyia nini.
“Nimejaribu kupitia Ilani za vyama vyote, lakini ya CCM inasema itajenga barabara au kuchimba visima… hii maana yake ni miradi sio dira, kwa kawaida ilani inatakiwa kubebwa na dira sio miradi,” alisema.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe na Naibu wake, Gaudensia Kabaka, walipotafutwa kupitia simu zao za mkononi kuelezea madai ya wanafunzi hao hawakupatikana.
 
Duh...hii rafu imechezwa wazi wazi! ccm ni mbuzi kweli!! yani naendelea kuwachukia hapa!
 
Kwa nini wasiruhusiwe kupiga kura ya rais iwapo wana shahada ya kupigia kura?
 
Mbinu zote safari hii hazifui dafu. watu wana mwamko safi. safari hii mafisadi mtajificha ulaya make hapa hapakaliki
 
Hapa nazidi kuwachukia CCM hapa wanacheza rafu za kimafya Go to hell ccm

Inabidi warusiwa kupiga kura ya Rais tu
 
NEC watumie busara, wawaruhusu vijana wetu kupiga kura ya urais. vinginevyo NEC wana kesi ya kujibu hapo baadae kwa kudhurumu haki za watu.
 
jf tusaidieni hawa ccm sijui wanatutakia nini sisi wanafunzi wa vyuo vikuu hawawezi kutekeleza madai yetu hadi hapo tutakapoanzisha bonge ya mgomo,kura ni haki yetu wasituchezee
 
Tunawaomba wana vyuo wote kila mahali uliopo anza sasa kuhamasisha watu wengine kupigia CHADEMA kura, kama muko 60,000 basi kila mwanachuo na mapenzi mema na nchi hii akihamasisha watu 5 -10 mahali alipo itakuwa imekula kwao. Ebu fanyeni hivyo kuanzia leo. Mabadiliko yako ya Bodi yako, KATIBA MPYA, elimu bure kwa wadogo zetu, afya bure kwa watanzania wote iko mikononi mwenu na watanzania wote wasio faidika na ufisadi; ushindi tayari huko upande wetu.
 
Wanafunzi waitisha serikali
Imeandikwa na Lucy Lyatuu; Tarehe: 4th October 2010 @ 07:27

WANAFUNZI wa elimu ya juu ambao ni wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameitaka serikali kufungua vyuo hivyo kabla ya siku ya kupiga kura la sivyo watahamasisha wananchi kupiga kura ya mabadiliko.

Wakati wanafunzi hao wakitoa kauli hiyo, chama hicho pia kimesema kitawatumia wanafunzi hao kulinda kura za wagombea wake.

Mwenyekiti wa Kamati ya wahitimu na wanafunzi wa elimu ya juu ya Chadema, Richard Manyanga alisema hayo jana Dar es Salaam katika kongamano lililohusisha wanafunzi hao.

Manyanga alisema kauli hiyo inatokana na hofu yao kwamba wanafunzi wa elimu ya juu takriban 60,000 watakosa haki ya kupiga kura ikiwa vyuo vitafunguliwa baada ya uchaguzi mkuu.

“Wanafunzi wengi walijiandikisha kupiga kura ndani ya vyuo vyao wakati wa uboreshaji wa daftari la kupiga kura… na fedha nyingi ilitumika kwa ajili ya kazi hiyo, sasa vyuo vikifunguliwa baada ya uchaguzi, haki ya wanafunzi kupiga kura haitoonekana, tunaiomba serikali isikie mwito wa kufungua vyuo kabla ya uchaguzi,” alisema Manyanga.

Alisema, anaamini kuwa vyuo havijakosa fedha za uendeshaji hadi wasogeze muda wa kufungua mpaka baada ya uchaguzi na kuwataka wanafunzi wa vyuo hivyo popote walipo kutafuta kura zaidi ya moja na iwe kura ya mabadiliko.

Manyanga alisema, katika kura hiyo ya mabadiliko, kila mwanafunzi anatakiwa kutoa elimu ya uraia kwa wananchi na kuwahamasisha kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa na vya upinzani ni kwa ajili yao ili wapige kura katika vyama vinavyolenga kuwakomboa wao.

Mjumbe wa kamati hiyo, Joshua Massaba aliwataka wasomi wakumbuke wajibu wao wa kutengeneza viongozi wazuri kwa manufaa ya taifa na kuongeza kwamba wana imani na mgombea ubunge wa Chadema katika Jimbo la Ubungo, John Mnyika na wako tayari kwa hali na mali kuhakikisha anapata ushindi.

Akizungumza katika kongamano hilo, pamoja na mambo mengine Mnyika alisema baada ya kufanya makosa mawili ya kisiasa mwaka 2005, wameanza kuandaa mawakala wakati wakiomba kura.

Alisema hadi sasa, vijana wa vyuo vikuu wameunda mawakala wa ulinzi kwa wa kura siku ya kupiga kura na kwamba katika jimbo hilo dalili zote zinaonesha wananchi wako tayari kwa mabadiliko.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), John Kiravu aliliambia gazeti hili kuwa, kuanzia Julai mosi hadi Julai 10, 2010 tume hiyo ilitoa muda kwa wale waliotaka kuhamisha taarifa zao katika daftari la wapiga kura, wafanye hivyo ili wapige kura katika eneo walilopo.

“Suala la wanafunzi wa vyuo vikuu mimi silijui, Nec inahusika na wapiga kura kwa ujumla, hivyo kama watapiga kura ama la sijui,” alisema Kiravu.
 
Mgombea ubunge jimbo la Ubungo, Dar es Salaam, kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika akizungumza na wanafunzi wa elimu ya juu wakati wa kongamano lililoandaliwa na chama hicho kuhusu uchaguzi mkuu
 
Hii kitu ilitangazwa miezi kadhaa iliyopita, wenye macho waliona na wakapiga kelele kidogo hapa JF kama kawaida. Mnakumbuka shuka alfajiri.

Lieni na wizara ya elimu ya juu sio tume ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi inahusikaje, itabadilisha sheria ngapi kukidhi matakwa?
 
Mkuu hapa issue sio kupiga kura,bali kiasi cha wanafunzi watakao pata mkop wa Elimu ya Juu kitapungua kwa kiasi kikubwa sana na ni kwa mara ya kwnza tangu kuanzishwa kwa ESBL.
Kwa maana hiyo kama wanafunzi wange fungua shule mapema ingekuwa issue, suala la kukosa mkopo inge kigharimu CCM.
Wakifungua vyuo baada ya uchaguzi itakuwa poa.
 
Hii ni mbinu iliyokuwa imepangwa tayari kuwazuia wasipige kura maana wanawajua wazi hawa sio watu wa ccm. Analysis ya matokeo ya uchaguzi wa 2005 uliwaonesha wazi kwamba wanafunzi wa vyuo vikuu hawawapi mafisadi kura.

There is nothing like double coincidence. Kwamba tarehe ya kufungua shule iongezwe zaidi ya mwezi halafu wasiwe na alternative ya kupiga ura waliko nyumbani. Take a note kwamba tangu mwezi wa saba hili swala lilikuwa likizungumzwa, na kama Tume ingekuwa inataka hawa wanafunzi wapige kura wangeshatoa suluhisho siku nyingi sana. Ukishaambatana na hili genge la mafisadi hata jinsi unavyofikiria unakuwa kama panzi together with your PhDs. That how it succs. 'Die CCM Die. We need a new country, with new leardership.
 
Serikali imesema haitabadili uamuzi wake wa kufungua vyuo vya elimu mwezi Novemba mwaka huu kama ilivyopanga licha ya kuwepo shinikizo la wanafunzi wanaotaka vifunguliwe ili kuwawezesha kwenda kupiga kura kwa kuwa wengi wao walijiandiskisha vyuoni.
Uamuzi huo wa serikali ulitangazwa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, na kuongeza kuwa vyuo vya elimu ya juu sio taasisi zinazoendesha siasa, bali ni maeneo yanayotumika kufundisha watalaamu wa kada mbalimbali
Profesa Maghembe alihoji ni kwa nini wanafunzi hao washinikize vyuo vifunguliwe kwa madai ya kutaka wakapige kura wakati wao hawahusiani na siasa zozote zinazoendelea hapa nchini na badala yake wao ni wanafunzi wanaohitaji kufundishwa ili wawe watalaamu wa baadaye.
“Chuo kikuu sio sehemu ya kwenda kufanya siasa, bali ni sehemu ya kufundisha watalaam mbalimbali na kwa kweli nashangaa hawa wanafunzi kushinikiza vyuo vifunguliwe,”
CHANZO: NIPASHE

huku ndo kutapatapa kwa ccm au??
 
Kama siasa haziwahusu, waliwaandikisha kwa minajili gani?
Hivi huyu maghembe ni profesa kweli au ndo yahaya mwingine tena?
Reasoning yake ipo below average na uwezo wa kufikiria hauna tofauti na mzee wa kudizz jukwaani
 
This is a complete clap! huyu jamaa anadhalilisha sana status ya Professor! anawezaje sema wanafunzi hawausiani na siasa? Siasa ni maisha, uchaguzi huu ni muhimu si tu kwa wanafunzi bali kwa watanzania wote, maana ni uchaguzi wa kuamua mustakabali wa maisha yao kwa miaka mitano ijayo. kwa wanafunzi ni uamuzi juu ya mikopo yao, ni uamuzi juu ya quality ya elimu yao so kwao uchaguzi huu ni kila kitu. Kama vyuoni ni sehemu ya masomo na sio sehemu ya kufanya siasa mbona hakuwakemea wale wanafunzi 30 wa UDOM waliojitokeza wakati ule kuzungusha fomu za udhamini wa JK? ile ilikuwa ni nini? ni sehemu ya masomo yao? Amesema ni sehemu ya kufundisha wataalamu, hivi unapowazuia wanafunzi wa political science kushiriki siasa unategemea kupata mtaalam gani toka fani hiyo? huu ubabaishai sasa umefika degree ya juu sana! Nafikiri it is a high time now kwa watz wote kuungana sasa na kupaza sauti zetu kulinda haki ya vijana hawa!
 
Kama siasa haziwahusu, waliwaandikisha kwa minajili gani?
Hivi huyu maghembe ni profesa kweli au ndo yahaya mwingine tena?
Reasoning yake ipo below average na uwezo wa kufikiria hauna tofauti na mzee wa kudizz jukwaani
uSILAUMU BWANA HALI MBAYA WWENZIO!!!
 
Profesa Maghembe alihoji ni kwa nini wanafunzi hao washinikize vyuo vifunguliwe kwa madai ya kutaka wakapige kura wakati wao hawahusiani na siasa zozote zinazoendelea hapa nchini
labd siku hizi wanafunzi wamekuwa ni kama majeshi ya ulinzi!!!
 
kumbuka vyuo ni kama majiko ya kupakua wanasiasa-tarajiwa mfano;
  1. kabwe
  2. malisa
  3. bashe
  4. mdee
  5. ongezea...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…