Elections 2010 Wengi wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutopiga kura 2010


Pia wakati huo ratiba/karenda za vyuo zilionesha siku ya kupiga kura vyuo vingekuwa vimefunguliwa.Hizi ni mbinu zao!
 
Mi si mlaum sana Maghembe, mi nalia na hizi serikali za wanafunzi tangu mwanzo kabla kufungwa kwa vyuo taarifa zilikuwepo kuwa wanafunzi watarudi baada ya uchaguzi,mi najuuliza tangu wakati huo walikuwa wapi? hadi leo zimebaki siku 26? "viongozi bora ni wale wanaoweza kuzia jambo kabla halijatokea na si kusubiri litokee ndo unashutka ala kumbe kuna hili"!
 
Huyu Magembe Nilidhani amenikera mimi tu ; kumbe kawaudhi watu wengi-Haonyeshi kabisa kama ni mtu aliesoma na kuelemika!
 
Narudia tena jamani wanafunzi waende mahakamani kudai haki yao. Wakiweza wa block uchaguzi mpaka NEC iseme itawasaidiaje kupata haki yao ya kikatiba? Kwani hakuna sababu ya kutoa matangazo na kubembeleza watu wajiandikishe kupiga kura kwa pesa nyingi na kisha kuwazuia kupiga kura kwa hila. Huu ni umafya
 
Kwani sababu ya kuchelewesha kufungua chuo siyo za kisiasa? au kuna sababu nyingine ambayo mimi siijui? sasa kama sababu ni siasa kwa nini wasihusiswe na siasa?
 
Jamani kwani wanafunzi wanatarajia nini toka kwa huyo Maghembe??? Mi naliangalia suala zima hili kwa mtazamo tofauti kiasi kama ifuatavyo. Vyuo vikuu vya serikali vipo chini ya wizara ya elimu, wizara hii haihusiani na masuala ya uchaguzi. Uchaguzi uko chini ya tume ya uchaguzi ambayo inahusiana na waziri mkuu au na rais moja kwa moja. Walioandikisha wanafunzi sio wizara ya elimu, ni tume ya taifa ya uchaguzi. SAsa nionavyo mimi sehemu muafaka ya kulalamikia ni ofisi ya waziri mkuu kupitia tume ya uchaguzi, wao wana mamlaka ya kutoa muongozo nini kifanyike kwa wale wote watao kuwa hawapo katika vituo walivyojiandikisha kupiga kura. Katika kuliangalia hili pia tusisahau kuwa muda uliopo ni mfupi saana, na kwa maamuzi yote yalochukuliwa ya kutofungua vyuo yanalengo maalumu, hata kama wanafunzi wataenda mahakamani, bado delaying tactic inaweza chukua mkondo wake na wasiweze pewa haki hii ya msingi. Rejea kesi ya Mtikira juu ya mgombea binafsi ilivyoamuliwa!!!!!. Kitu nachokiona ambacho kinaweza okoa hali hii, ili kuvuruga malengo ya serikali ni kwa wale wote walio hatarini ya kukosa kupiga kura kutokana na kuwa hawatakuwa vyuoni ni kuamua kufanya jambo moja zito lakini muhimu. Nalo ni kujitolea pamoja na ukata unaowakabili, wajilipie nauli wafike katika vituo walivyojiandikishia siku ya kupiga kura waweze kupiga kura. Kwani kutokuwepo kwa wanafunzi vyuoni hakutafanya vituo walivyojiandikishia visiwepo, maana kuna wafanyakazi na pia watu wanaoishi maeneo ya jirani na vyuo hivyo wataenda kupiga kura kama kawaida. Haki huwa haitafutwi kirahisirahisi tu, hufikia wakati mwingine mtu akalazimika kujitolea, mali yake, wakati wake, muda wake nk. Serikali iliamua kuchukua uamuzi wa kutofungua vyuo mapema ili kusevu hasahasa majimbo yaliyopo hapa Dar. Wajua ukiongea Dar unaongea Ubungo (UDSM, Chuo cha usafirishaji, chuo cha maji); Temeke (DUCE, Uhasibu,); Ilala (IFM, CBE); Iringa mjini (MUCE); Dodoma mjini (UDOM). Sasa idadi ya wanafunzi waliopo katika vyuo hivyo, inatosha kabisa kubadili matokeo ya majimbo hayo. Tukumbuke majimbo haya hayajawahi kuchukuliwa na upinzani toka 1995 ukiacha jimbo la temeke.. So wito wangu kwa wanafunzi, na wale wote wenye nia njema ni kujaribu kuitumia option hii ya kujigharimia na kufika vituoni kupiga kura. Mungu atawalipa zaidi kwa kujitolea kwenu huko.
Babayah
 
Kama siasa haziwahusu, waliwaandikisha kwa minajili gani?
Hivi huyu maghembe ni profesa kweli au ndo yahaya mwingine tena?
Reasoning yake ipo below average na uwezo wa kufikiria hauna tofauti na mzee wa kudizz jukwaani


JE WAZIRI HAIHESHIMU HATA KATIBA?????? AU PIA HAIJUI?????? HUKU NIKUJIFANYA mungu MTU, POLENI SANA WAPIGA KURA WA MWANGA , HUYU NI KIPOFU LAZINMA AWAINGIZE MASHIMONI WANA MWANGA NA TAIFA KWA UJUMLA.
 

Mbona CCM ina matawi vyuoni, e.g. UDOM, UDSM? CCM inajikanyaga sana
 
Mie hata simlaumu, ni yale mashavu na tumbo ambavyo havipo propotional ndo maana anaongea vitu vya namna hiyo....ile miwani alirithi kwa babu wa babu ayke ndo maana akisoma nyaraka anziona mbilimbili...tangu lini mtu akaitwa Maghembe ( Hoe)
 
Ushauri wangu kwa wanafunzi ni kujitolea kwa hali na mali. Wajilipie nauli wafike vituoni walikojiandikisha wapige kura. Maana pamoja na kufunga vyuo, lakini vituo havitafungwa. Ikiwezekana kwa vyama vya upinzani kushirikiana kulifanikisha hili. Najua kuna Takukuru, lakini wanaweza kutumia njia muafaka, kuwawezesha wale wote watakao kwama kipesa kuweza fika vituoni mwao wakapiga kura. Uamuzi wa kuwazuia wanafunzi haujachukuliwa kwa bahat mbaya, la hasha bali ni mpango maalumu wa kuyalinda hasahasa majimbo matatu ya Ubungo (UDSM, Chuo cha maji na chuo cha usafirishaji), Kinondoni (IJSM),Ilala (IFM, CDE, DAR TECH) na Temeke (MUCE) labda pia na majimbo ya morogoro mjini (SUA) Iringa mjini (MUCE) na Dodoma mjini (UDOM). Wanafunzi waliopo katika vyuo hivi wanatosha kabisa kubadiri mwelekeo wa matokeo katika majimbo hayo. Pamoja na kuwa wapo pia wana CCM katika vyuo hivyo, lakini kwa kiasi kikubwa wanafunzi wengi na hasa wale watoto wa walala hoi wanamtazamo hasi juu ya CCM. Hivyo wito wangu kwa wanafunzi ni kujitolea nauli zenu japo ni za taabu mkavifikia vituo vyenu mkapiga kura. Kumbukeni kwenda Mahakani kwa muda uliopo hamtopata haki yenu, kumbukeni keshi ya mgombea Binafsi ilivyofanywa na hao tunaowaita majaji wasomi. Kamwe majaji hawataenda against serikali hasa katika suala hili la uchaguzi.
Babayah
 
Mie hata simlaumu, ni yale mashavu na tumbo ambavyo havipo propotional ndo maana anaongea vitu vya namna hiyo....ile miwani alirithi kwa babu wa babu ayke ndo maana akisoma nyaraka anziona mbilimbili...tangu lini mtu akaitwa Maghembe ( Hoe)
hahaha maelezo yako yameniacha meno yote arobaini na sita nje.

Kama vyuoni si sehemu ya siasa, mbona ccm imewekeza matawi huko?

Wakulu tuoganaiz kuwaleta vijana town waje kupiga kura.
 
Kuna uwezekano mkubwa wa wasomi wetu hapa nchini hasa wale wa elimu ya juu ( universities) kukosa nafasi ya kushiriki kupiga kura mwaka huu, na hii inatokana na vyuo kufunguliwa baada ya uchaguzi huku idadi kubwa wamejiandikisha wakati wakiwa chuoni...

hii nikumnyima mwananchi haki yake ya msingi kwa makusudi kabisa.

TUME,WANASIASA,WANANCHI TULIKEMEE HILI SWALA KURA ZA WATU ZINAPOTEA,HIZO NDIZO ZITATUSAIDIA KUTUPATIA VIONGOZI WANAOFAA,KURA YA MSOMI MMJA INAWEZA IKABADILISHA MAISHA YA TAIFA.
 
thithiemu πŸ˜›reggers:πŸ˜›reggers:πŸ˜›reggers:
 
Ndugu zangu si dhani kama wizi ni kuchukuatu kile kisichokua chako bila idhini ya mwenye nacho, hata kumzuia anestahili kukipata kutokukipata pia umeiba.

Nasema haya nikihusianisha na suala la viuo vikuu kufunguliwa baada ya octoba 31 (siku ya kupiga kura). Kma tunavyojua wengi kama sio wote wa wanfunzi wa vyuo vikuu wanasifa za kupiga kura, na ni dhahiri kua ni mpango wa ccm kutokufungua vyuo vikuu kabla ya 31 oktoba ili wanafunzi hawa wasipige kura kwani kama wakipiga kura nyingi hazitakwenda CCM. Mfano kwa pale ubungo, nyingi zitakwenda kwa Mnyika (ubunge) na Dr Slaa uraisi.

Ushauri: Wanaharakati, vyama vya siasa, taasisi za haiki za binadam na sisi tulio na uchungu na nchi kwa nini tusiungane kutafta suluhu ya hawa vijana kupiga kura??
 
Tumpe dr.slaa kura ya ndiyo...............kiwete (kikwete amechemka), aliisha ambiwa na nyerere jk wa ukweli kuwa "kwa mtu mwaminifu kabisa kabisa ikulu ni mzigo".......kikwete hauwezi mzigo wa ikulu aondoke hatumtaki watz wamesema hapana..........
 
Tumpe dr.slaa kura ya ndiyo...............kiwete (kikwete amechemka), aliisha ambiwa na nyerere jk wa ukweli kuwa "kwa mtu mwaminifu kabisa kabisa ikulu ni mzigo".......kikwete hauwezi mzigo wa ikulu aondoke hatumtaki watz wamesema hapana..........
Punguza munkari. JK uchaguzi ushamshinda ilaanatimiza wajibu wake kitaifa.
 

hizo ni akili finyu za makamaba and the lot in ccm, kwangu mimi nawaona hawa vijana kuwa potentially hazardous against ccm huko mitaani, vijijini na na kwingineko waliko sasa hadi tarehe 31 oktoba 2010 kuliok kama wangeruhusiwa kuwa vyuoni mwao.

kutokana na miscalculationa za ccm, chadema and the opposition ita benefit kwa kupata wasemaji na wawakilishi in different parts of the country. Nina uhakika mkubwa kuwa hata sasa wanachangia kwa kiwango kikubwa kuhamasisha watu kujazana katika mikutano ya kampeni ya dr slaa, watatumika kuwahamasisha watu kujitokeza kupiga kura na kulinda kura za wagombea wa chadema huko waliko.

ndio maana nathubutu kutamka kwa ccm imeishiwa fikra. Hivyo na na sisi wengine tuache kuwaiga ccm kulalama tu, lets seize the opportunity kwa kuwahamasisha hao vijana kulipa visasi vya kupokwa haki zao za kupiga kura kwa kuwahamasisha watanzania popote walipo washiriki kikamilifu kuleta mabadiliko mwaka 2010 kwa kujitokeza kupiga kura kwa wingi sana na kuwachagua wagombea wa chadema kwa wingi.

kwa kufanya hivyo watakuwa wametio mchango mkubwa kwa taifa hili unaozidi kura zao moja moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…