Wengi wenye vitambi walipata utapiamlo utotoni

Wengi wenye vitambi walipata utapiamlo utotoni

Kinyume chake ni kweli.
Watoto waliokula kupita kiasi hasa vyakula vya sukari mfano maziwa ya ng'ombe wako kwenye hatari kubwa ya kupata unene ukubwani.
Unene ni dalili ya ugonjwa unaoitwa insulin resistance. Na huu ni ugonjwa huanza wakati wa utoto ila unaweza usijitokeze hadi ukubwani.

Unene uliopita kiasi hausababishwi na kula sana,mtu anaweza kula kidogo tu na bado akanenepa kama ana ugonjwa huu wa insulin resistance.
Hata magonjwa kama kisukari hayasababishwi na unene kama tunavyoambiwa.Kisukari pia ni dalili ya ugonjwa wa insulin resistance.
What is Insulin resistance??
 
Bora mimi nilizaliwa mnene ila nimekua nmekua mwembamba, mama kila akiniona analalamika kwamba katika watoto wake woote mimi ndio alinizaa nikiwa mnene ila wengine walikua na uzito mdogo sana, sasa nmekua wenzangu wamekua mabonge mimi bonge wa utotoni nmekua mwembamba, vice versa is true
 
Unene ni dalili ya ugonjwa unaoitwa insulin resistance.

Kisukari pia ni dalili ya ugonjwa wa insulin resistance.

Aisee...!!

Kuna haja ya kurudi darasani na kujifunza magonjwa zaidi na zaidi..

Huu ugonjwa sikuwahi kuusikia wala kujifunza
 
Habarini wakuu sana. Ipo namna hivyo. Watu ambao hawakupata lishe ya kutosha utotoni huwa wanapoteza uwezo wa kuchakata msosi. Yaani mwili wake unavyotumia chakula ni tofauti na mtu ambaye alipata lishe ya kutosha. Sasa mtu huyu akipata pesa au uhakika wa msosi ukubwani, anajikuta anakula kuliko uwezo wa mwili wake kuchakata msosi. Jambo hili linapelekea tatizo la obesity, kitambi, kisukari na magonjwa mengine yatokanayo na ulaji mbaya.

Ni vema tujitahidi wapate mlo kamili utotoni, maziwa na nyama ni muhimu sana. Na kama hukupata chakula kamili utotoni na ukapata udumavu, punguza ulaji usio na afya.
Mbona watoto wa Masaki na Obay kwenye uhakika wa msosi ndiyo wanaongoza kwa vitambi kuliko wale wa Tandika na Mbagala?
 
Mbona watoto wa Masaki na Obay kwenye uhakika wa msosi ndiyo wanaongoza kwa vitambi kuliko wale wa Tandika na Mbagala?
Hiyo ni obesity ya utotoni. Inatokana na kula kupita kiasi, hasa mafuta na sukari. Mtu ambaye hakupata chakula kamili utotoni, yaani ana utapiamlo. Akiwa mtu mzima na akaanza kula kupita kiasi anakuwa kwenye hatari ya obesity na utapiamlo kuliko aliyepata mlo kamili utotoni.
 
Back
Top Bottom