Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,043
Kupungua kwa mawasiliano ya kijamii kati ya wanajamii (socialization), na hasa kwa vijana na wanawake waliokulia katika maeneo ya mijini. Yote ni athari zinazochangiwa na matumizi ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii kama Twitter (X), TikTok, na Instagram, na jinsi zinavyochangia kuporomoka kwa socialization katika jamii yetu.
Imeonekana kuwa matumizi ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii yamekuwa na mchango mkubwa katika kupungua kwa mawasiliano ya uso kwa uso kati ya watu. Watu wengi sasa wanajikita zaidi katika majadiliano ya mtandaoni kuliko kuzungumza na watu ana kwa ana. Mambo haya ni ya kawaida kwa vijana na wanawake, ambapo wengi wao wanapokuwa pamoja, wanakuwa busy na simu zao au majadiliano ya mtandaoni, badala ya kushiriki katika mazungumzo ya kijamii ya ana kwa ana.
Athari nyingine inayojitokeza ni kwamba watu wengi sasa wanachati hata wanapokuwa njiani, wakiwa wanatembea au wanapoendesha magari, wengine hata kwenye ibada. Tabia za namna hii zinatia wasiwasi, kwani inachangia hatari za usalama na kupunguza nafasi ya kujenga uhusiano wa kijamii wa maana. Hali hizi zinapelekea jamii kuwa kama "mazombi", ambapo watu wanaishi kwa kujitenga na wengine na kupuuza umuhimu wa mawasiliano ya kijamii ya moja kwa moja.
Zaidi ya hayo, katika familia nyingi za kimji na kishua , hali ni mbaya zaidi. Wageni wanapotembelea familia hizo, badala ya kushiriki mazungumzo ya familia, wanajamii wanakuwa busy na simu zao, na wakati mwingine hakuna kabisa mazungumzo ya maana yanayotokea. Haya yanadhihirisha kupungua kwa umoja wa familia na jamii, jambo ambalo linatishia mshikamano wetu kama watu.
Ninashauri kwamba jamii yetu irejee kwenye mawasiliano ya kijamii ya ana kwa ana. Ingawa mitandao ya kijamii na teknolojia zina faida nyingi, ni muhimu kuzingatia umuhimu wa kuungana kama jamii na kujenga uhusiano wa kijamii ulio bora, ulio na maana. Tunaweza kutumia teknolojia kwa manufaa, lakini pia lazima tutambue kwamba mawasiliano ya kweli kati ya wanajamii ndiyo msingi wa mshikamano wetu na ustawi wa jamii.
Tukumbuke umoja na mawasiliano ya kijamii ni maisha yetu ya kila siku.