Wengine huwa hatupashi viporo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Kwa kweli sisi wengine tukiachana ndio tumeachana moja Kwa moja. Hakuna kitu ambacho kinaniudhi na kunifanya niwe mkali kama binti niachane naye halafu baada ya miaka miwili aniletee shobo na pigo za kipumbavu pumbavu. Tukishaachana tumeachana, mazoea ya kujifanya sijui marafiki sijui ushkaji sio kwa watu kama sisi.

Wapo wanawake ambao nimewaweka kwenye kundi la marafiki na dada wa hiyari, wewe kama nilikuweka kwenye kundi la mpenzi tukashindwana elewa kuwa ndio nafasi pekee niliyokupatia. Nawe ufanye vivyohivyo, wala sitajali kwa sababu ni maamuzi yako.

Kupasha kiporo kwa kweli ni mwiko. Wanasema kurudia matapishi. Sijajua ni allergy au ni nini, lakini hiyo iko hivyo.

Kuna wale umezaa naye mtoto halafu mkaachana. Ukipiga simu eleza ishu za mtoto hayo mengine sijui ya maisha yanaendaje hayakuhusu, mbona mimi sikuulizi.

Dakika mbili zinatosha kutoa taarifa ya mtoto. Kama ni pesa itatumwa. Mtoto amekua mkubwa, atajieleza mwenyewe nikiongea naye.

"Oooh, nimekumiss, ooh bado nakukumbuka!" Who cares, inahusu nini, inamaana gani kwa muda huu?

Tafuta mtu mwingine, au kaa mwenyewe, fresh! Umekuwa mke au mchumba wa mtu kwa nini kunisumbua sumbua na kujifanya unanijua sana, pumbavu!

Viporo wengine ni mwiko kuvipasha! Yaani watoto kibao wazuri wamejaa huko mitaani halafu nipashe kiporo. Huyo labda sio mimi.

Tukishaachana;
1. Futa namba zangu na usinitafute kabisa. Unanisalimu salimu nini, uliambiwa wanawake wengine hawawezi kazi hiyo?

2. Choma picha zangu na zile za kwenye simu futa zote ili usinikumbuke.

3. Ikiwezekana delete faili langu kwenye ubongo wako kama mimi nilivyofanya.

Oooh, sijui nitakukumbuka, mara sitapata mwanamke mwengine kama wewe, hivi aliyekwambia nitatafuta mwingine kama wewe ni nani?

Imebaki stori, kila mtu apite kivyake. Kufuatana fuatana wengine hatutaki. Tukiachana tunamaanisha tumeachana. Full stop.

Nawatakia Sabato njema

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Huwa sipendi kuwa na attachments na mwanamke, ili hata akija next time niwe huru kumtafuna bila stress kwamba tuliachana.

Wengine tunachosema ndicho tunamaanisha.
Na chochote atakachosema ndicho tutajua anamaanisha.
Nikisema sikutaki jua sikutaki.
Akisema hanitaki basi nami ninayachukua maneno yake hivyohivyo.
 
MWANAMKE UNAWEZA ENDA ISHI NAE KATIKATI YA MSITU WA AMAZON MKIWA PEKE YENU NA BADO AKAKUSALITI.

ATAKUSALITI EIDHA KWA WANYAMA KAMA MBWA AU MATUNDA KAMA NDIZI NA TANGO

Sio kweli.
Kwenye suala la Mapenzi. Mwanaume ni msaliti mara elfu zaidi ya Mwanamke.

Wanawake ni waaminifu Kwa wanaume wanaowapenda.
Ila wanaume siku zote Sisi sio waaminifu hata Kwa Wanawake tunaowapenda. Tamaa ya miili yetu tunaiendekeza mpaka tunawasaliti Wake zetu.
 
Sasa badala ya kuwachana live, unakuja kulalamika huku JF

Wanaume hatuna hizo, maneno kidogo action kubwa
 
Sasa badala ya kuwachana live, unakuja kulalamika huku JF

Wanaume hatuna hizo, maneno kidogo action kubwa

Nafikiri bado uko shambani, au Akili yako iko Gizani. Hujui hata Dunia Ipo wapi na wapi inaenda.
Na pengine hujui hata Kwa nini umejiunga huku mtandaoni.

Kwa Lugha rahisi tunasema wewe ni mjinga katika hayo niliyoyataja
 
Safi kabisa. Hiyo pia itakuepushia na magonjwa.

Mnaachana mkiwa wazima. Mwenzako kaenda huko kaukwaa, anakuletea. Bila kuchukua tahadhari, unalizagamua kwa kisingizio ni salama kama ilivyokuwa awali.

Unaukwaa, unasambaza kwa familia yako.

Iweni na msimamo. Kama mmeshindwa, pimeni kabla ya kupashana..
 

Nakuambia hivi, wengine tukiachana ndio tumeachana Kabisa.
Mazoea ya kijingajinga hatutaki.

Nafurahi Kwa sababu Warembo ambao niliwahi ku-date NAO ni type yangu, yaani mkiachana ndio mmeachana, hakuna tena mazoea.
Kama kuna ishi ya michoho ya Pesa atapiga,
"Hello Bob! Bado unaendelea na Ile kazi yako, naomba Huduma Fulani, au kuna mchongo wa Pesa unaokuhusu"
Biashara inafanyika kisha kila MTU hamsini zake
 
Viporo vikijipendekeza wengi hula, ila inamadhara Sanaa kuliko saana.
 
Kweli kabisa hii.
Ila ubaya ni kua mwanamke akikusaliti penzi linakua hatarini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…