Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Kwa kweli sisi wengine tukiachana ndio tumeachana moja Kwa moja. Hakuna kitu ambacho kinaniudhi na kunifanya niwe mkali kama binti niachane naye halafu baada ya miaka miwili aniletee shobo na pigo za kipumbavu pumbavu. Tukishaachana tumeachana, mazoea ya kujifanya sijui marafiki sijui ushkaji sio kwa watu kama sisi.
Wapo wanawake ambao nimewaweka kwenye kundi la marafiki na dada wa hiyari, wewe kama nilikuweka kwenye kundi la mpenzi tukashindwana elewa kuwa ndio nafasi pekee niliyokupatia. Nawe ufanye vivyohivyo, wala sitajali kwa sababu ni maamuzi yako.
Kupasha kiporo kwa kweli ni mwiko. Wanasema kurudia matapishi. Sijajua ni allergy au ni nini, lakini hiyo iko hivyo.
Kuna wale umezaa naye mtoto halafu mkaachana. Ukipiga simu eleza ishu za mtoto hayo mengine sijui ya maisha yanaendaje hayakuhusu, mbona mimi sikuulizi.
Dakika mbili zinatosha kutoa taarifa ya mtoto. Kama ni pesa itatumwa. Mtoto amekua mkubwa, atajieleza mwenyewe nikiongea naye.
"Oooh, nimekumiss, ooh bado nakukumbuka!" Who cares, inahusu nini, inamaana gani kwa muda huu?
Tafuta mtu mwingine, au kaa mwenyewe, fresh! Umekuwa mke au mchumba wa mtu kwa nini kunisumbua sumbua na kujifanya unanijua sana, pumbavu!
Viporo wengine ni mwiko kuvipasha! Yaani watoto kibao wazuri wamejaa huko mitaani halafu nipashe kiporo. Huyo labda sio mimi.
Tukishaachana;
1. Futa namba zangu na usinitafute kabisa. Unanisalimu salimu nini, uliambiwa wanawake wengine hawawezi kazi hiyo?
2. Choma picha zangu na zile za kwenye simu futa zote ili usinikumbuke.
3. Ikiwezekana delete faili langu kwenye ubongo wako kama mimi nilivyofanya.
Oooh, sijui nitakukumbuka, mara sitapata mwanamke mwengine kama wewe, hivi aliyekwambia nitatafuta mwingine kama wewe ni nani?
Imebaki stori, kila mtu apite kivyake. Kufuatana fuatana wengine hatutaki. Tukiachana tunamaanisha tumeachana. Full stop.
Nawatakia Sabato njema
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.