Wengine huwa hatupashi viporo

Wengine huwa hatupashi viporo

Ukiachana na mtu achana nae,huwezijua huko alikoenda kabeba nini,halafu unakuja kupasha tu kipolo.Ni hatari sana,magonjwa mengi sana.
 
Kuna binti nilikua na mahusiano nae sasa ikafikia muda nikaona haendani na mitazamo yangu maana anajifanya mjuaji sana.

Sasa nilikua nimepanga nae mambo mengi nikamuahidi sitomuachaga, sasa tukawa tunapishana sana ugomvi hauishi na kununiana nikaona huyu sasa jambo na yeye limefika mwisho.

Mimi nikaamua kuachana na huyo binti bila kumwambia, yaani nikawa nawasliana nae kawaida ila simpi ushirikiano wa mapenzi, mpaka ikafikia hatua akaamua mwenyewe tuachane.

Akanimbia mwenyewe nimechoka kila mtu angalie ustarabu wake, nikamjibu sawa. Akakaniambia huna lolote umenipotezea muda tu[emoji23].. nikamjibu sawa , maana me nikiachana na mtu huwa naachana kistarabu.

Kuanzia hapo nikafuta namba na kila kitu chake, zikapita siku 2 akanitafuta sikujibu sms zake, nikaa wiki akanitumia sms sikujibu, akaanza kunilaumu et namchukia bila sababu maneno mengi nikamjibu tumeachana sitaki kuwasliana na ww tena nikampiga tofali.

Akawa ananitafuta kwa namba tofauti tofauti nikigundua ni yeye nampa kitofa mpaka akanisahau yule pimbi.
 
Back
Top Bottom