Najiuliza hivi Mbowe na Lisu wameshindwa kuwazuia hawa chawa wao waache kampeni za hovyo, za kijinga, za matusi na za kitoto. Kama wameshindwa jaribio hili dogo tu vipi wanataka tuwape nchi wataweza kweli kudhibiti vyombo vya dola ikiwa chawa wao tu wameshindwa kuwadhibiti. Kama watu wazima na akili zao ndio hizi za kushindwa kujua kuna maisha baada ya uchaguzi vipi watawezaje kuongoza nchi. Yaani hao chawa wa Mbowe na Lisu kati yao ndio wategemewe watoke humo mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, n.k. hapana aisee. Na kati ya Lisu na Mbowe eti mmoja awe amiri jeshi mkuu wakati wameshindwa kukemea chawa wao wafanye kampeni za kistaarabu.
Njia ile ile ya bonde la uvuli wa mauti NCCR, TLP na CUF zilimopita ndio njia ile ile CHADEMA inapita sasa. Kwa jinsi watu wazima CHADEMA wanavyovuana nguo mbele ya vyombo vya habari siioni tena kama CHADEMA itaendelea kuwa chama chenye nguvu hata kama watapita salama kwenye uchaguzi ujao kutokana na kauli zao za hovyo wanazojibishana mbele ya vyombo vya habari.
Ni mtizamo tu