Wenye Akili tuliandika mno Kupinga Ujenzi wa hovyo wa 'Fremu Lugalo' tukapuuzwa, sasa hata Mama nae Boss wao 'wamekerwa' nao

Zilipaswa zote zivunjiliwe mbali... huwezi kata miti na kuondoa ule uoto w aasili kia ma frem.... Frem zenyewe zimejengwa hovyo hovyo... aibu tupu...

CDF nashauri hizo fremu zote zivunjwe......
 
Jiwe gizani kuanzia JWTZ mpka mmiliki wa Grocery 😂😂
Kweli panatia aibu, na Kuna bwana mmoja kajenga gorofa uchwara kule mwishoni bila kufuata utaratibu; Kwa kulinganisha na hizo frame!! Mipango Miji mpo likizo!?
 
Zilipaswa zote zivunjiliwe mbali... huwezi kata miti na kuondoa ule uoto w aasili kia ma frem.... Frem zenyewe zimejengwa hovyo hovyo... aibu tupu...

CDF nashauri hizo fremu zote zivunjwe......
Hazijakaa vizuri na pia nahisi kila mtu alijijengea Kwa utashi wake, hakuna designs
 
Tatizo hawataki kuwasikiliza nyie wenye akili, ndio maana wanafeli. Hawajui kuwa kuna watu ni WELL TALENTED AND INTELLECTUALLY BLESSED, GAME CHANGER!
 
Ni kweli kabisa naona za kwenye kona zinabomolewa.
 
Niliwahi kuuliza Mabibo jeshini nako vipi? Naona bar zinachipuka tu kama uyoga
 
Huu nao ni udhaifu wa watu ambao tulitumaini watakuwa makini na sehemu tulizowapatia,silaha nzito tulizowapatia kwaajili ya ulinzi.Viongozi wa haya majeshi huwa wana uamuzi wa hovyo mpaka unaweza kushangaa kama wana taaluma ya ulinzi&usalama.
 
Hakika nilishangaa sana baada ya kuona zikijazwa frem kama mvua sehem nyeti kama ilee kama nchi tumefikia pabaya wajitafakari sana.
Akili zetu waTZ zinawaza kujenga mafrem tu kila mahali,kila anayejenga nyumba anafikiria na frem🤔
 
Mh wajeda wapo mule zile flat wanakaa wao na kuna kibao kbs cha tahadhari
Mabibo jeshin hazikuwa zikimilikiwa na jeshi, ni nyumba za NHC Kama za magomeni
Wajeshi walipewa kukaa miaka hiyo baadae ziliuzwa na aliyepewa nafasi ya kununua ni mpangaji aliyekaa muda mrefu zaidi, awe mjeshi au hawara wa mjeshi.
Kule sio makao ya wajeshi tena...labda tuwe tunatofautiana eneo tunalozungumzia ila ni hii mabibo ya kuingilia via soko la ndizi toka Moro road ama luhanga toka Mandela road
 
Aisee unamaanisha nini? Kwamba ile kambi ya jeshi la anga pale sio eneo la jeshi?
 
Zilianza kufumuka baada tu ya hayati kuondoka. Hizo zitakuwepo na zitaendelea kujengwa kika mahali. Nenda kule external na kitunda utaona zinavyoota fremu.
 
Kwanza ukifika pale mwanzoni utaona vibao huruhusiwi kukatisha Ile njia ya miguu baada ya saa kumi na mbili..Sasa hizo frem zikianza kutumika means lugalo yote itachangamka watu watakuwa wanakatisha sana kwenda mwenge na itakuwa busy njia....fremu zenye nyingi Sana na zimejengwa vibaya na kiholela Sana...imagine zote zifunguliwe na kuwebusy pale itakuwa hatari Sana kwa jeshi...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…