Wenye Akili tuliandika mno Kupinga Ujenzi wa hovyo wa 'Fremu Lugalo' tukapuuzwa, sasa hata Mama nae Boss wao 'wamekerwa' nao

Wenye Akili tuliandika mno Kupinga Ujenzi wa hovyo wa 'Fremu Lugalo' tukapuuzwa, sasa hata Mama nae Boss wao 'wamekerwa' nao

Zilipaswa zote zivunjiliwe mbali... huwezi kata miti na kuondoa ule uoto w aasili kia ma frem.... Frem zenyewe zimejengwa hovyo hovyo... aibu tupu...

CDF nashauri hizo fremu zote zivunjwe......
 
Jiwe gizani kuanzia JWTZ mpka mmiliki wa Grocery 😂😂
Kweli panatia aibu, na Kuna bwana mmoja kajenga gorofa uchwara kule mwishoni bila kufuata utaratibu; Kwa kulinganisha na hizo frame!! Mipango Miji mpo likizo!?
 
Zilipaswa zote zivunjiliwe mbali... huwezi kata miti na kuondoa ule uoto w aasili kia ma frem.... Frem zenyewe zimejengwa hovyo hovyo... aibu tupu...

CDF nashauri hizo fremu zote zivunjwe......
Hazijakaa vizuri na pia nahisi kila mtu alijijengea Kwa utashi wake, hakuna designs
 
Tatizo hawataki kuwasikiliza nyie wenye akili, ndio maana wanafeli. Hawajui kuwa kuna watu ni WELL TALENTED AND INTELLECTUALLY BLESSED, GAME CHANGER!
 
Niliwahi kuuliza Mabibo jeshini nako vipi? Naona bar zinachipuka tu kama uyoga
 
Huu nao ni udhaifu wa watu ambao tulitumaini watakuwa makini na sehemu tulizowapatia,silaha nzito tulizowapatia kwaajili ya ulinzi.Viongozi wa haya majeshi huwa wana uamuzi wa hovyo mpaka unaweza kushangaa kama wana taaluma ya ulinzi&usalama.
 
Hakika nilishangaa sana baada ya kuona zikijazwa frem kama mvua sehem nyeti kama ilee kama nchi tumefikia pabaya wajitafakari sana.
Akili zetu waTZ zinawaza kujenga mafrem tu kila mahali,kila anayejenga nyumba anafikiria na frem🤔
 
Mh wajeda wapo mule zile flat wanakaa wao na kuna kibao kbs cha tahadhari
Mabibo jeshin hazikuwa zikimilikiwa na jeshi, ni nyumba za NHC Kama za magomeni
Wajeshi walipewa kukaa miaka hiyo baadae ziliuzwa na aliyepewa nafasi ya kununua ni mpangaji aliyekaa muda mrefu zaidi, awe mjeshi au hawara wa mjeshi.
Kule sio makao ya wajeshi tena...labda tuwe tunatofautiana eneo tunalozungumzia ila ni hii mabibo ya kuingilia via soko la ndizi toka Moro road ama luhanga toka Mandela road
 
Mabibo jeshin hazikuwa zikimilikiwa na jeshi, ni nyumba za NHC Kama za magomeni
Wajeshi walipewa kukaa miaka hiyo baadae ziliuzwa na aliyepewa nafasi ya kununua ni mpangaji aliyekaa muda mrefu zaidi, awe mjeshi au hawara wa mjeshi.
Kule sio makao ya wajeshi tena...labda tuwe tunatofautiana eneo tunalozungumzia ila ni hii mabibo ya kuingilia via soko la ndizi toka Moro road ama luhanga toka Mandela road
Aisee unamaanisha nini? Kwamba ile kambi ya jeshi la anga pale sio eneo la jeshi?
 
Endeleeni tu Kupuuza Maandiko yetu hapa JamiiForums na Kuupuza huu Mtandao ila kama kuna Mtandao nyie mlioko Serikalini na huko sehemu Nyeti za Umedani (JWTZ) na Unjaguni (TISS) mnatakiwa muwe mnauheshimu na Kuufuatilia ili kuwa Bora katika Utendaji wenu basi ni huu wa JamiiForums.

GENTAMYCINE pamoja na Members wachache hapa tulijitoa Mhanga kuanzisha Mada za Kupinga Ujenzi wa hovyo na wa Kienyeji wa Fremu za Biashara katika Fensi za Kambi yenye Heshima Kimedani nchini ya Lugalo na Kufafanua kuwa Kiusalama na Kiulinzi ilikuwa ni Hatari na Kosa Kubwa tukapuuzwa hadi Kudhihakiwa ila nashukuru kuwa kumbe hata Mama na Boss wao wamechukizwa na Kilichofanyika.

Za ndani kabisa nilizozipata kutoka kwa Watu wa karibu Unjaguni na Umedani zinasema kwamba hizo Fremu zitabakia ila mita chache (kwa nyu.ma) kutajengwa Ukuta mkubwa ili Kuzitenganisha ili kuendelea Kuilinda Kambi hiyo tofauti na ilivyo sasa ambapo hata Mimi GENTAMYCINE naweza kuingia muda wowote kwa kupitia ilipo Grocery mpya ya Giraffe iliyopo katika Fremu hizo hizo na nikajua nini kinaendelea kwa ndani na kutoka nje bila tatizo lolote.

Vile vile nimetaarifiwa kuwa baada ya Hayati kuruhusu huo Ujenzi ili wana Medani na Kambi zao wawe Wanajipatia Vipato aliyeko sasa (Mama) ameamua Kuusitisha huo mpango kwani ameona utakuwa ni Hatari na Kuwafanya Wananedani Kuwekeza Akili zao katika Mitonyo (Fedha) badala ya 24/7 kuwaza jinsi ya Kupambana na akina M23 na Wachokozi wengine wa Ardhi yake.

Hivyo basi Mama ameamua kuwa atarudisha zile Ruzuku zao za kila Kambi (Kikosi) kama ilivyokuwa huko nyuma wakati wa Kipindi cha Mstaafu wa Pwani tofauti na ambavyo Hayati aliamua na kufanya kwani ni Hatari na huenda alishauriwa vibaya nae akaingia Kichwa Kichwa.

Haya wale mliotutukana na Kutuona hatuna Akili njooni mtuombe Msamaha kwani Sisi tuliolikemea na Kupinga leo tunaenda kuwa Washindi kwani tuliamua kutumia Uzalendo wetu kwa Tanzania na Wananedani wetu kwa Kupinga Ujenzi wa Fremu za Kambini Lugalo (eneo la Kawe) hasa kwa sababu za Kimkakati (Ulinzi na Usalama) kitu ambacho kutokana na Uvivu wenu wa Akili na kwa kutokuwa Security Concious Kwenu wala hamkuliona lile ambalo akina GENTAMYCINE wenye Maono ya mbali tuliliona.

Mwenye hiyo Giraffe Grocery hapo katika hizo Fremu hongera kwa kutuwekea Mziki mkubwa, Vibinti Vifidodido (Vyembamba kama Fito) na Wines za uhakika, ila jitahidi katika hiyo Flash yako uwe na Nyimbo nyingi za Bendi ya Wenge Musica BGBG yake JB Mpiana, Koffi Olomide na Werrason kwani naona una Nyimbo nyingi za Vijana wa sasa na huwa hazichangamshi pale Vodka na Smart Gin ikiwa inashuka Makooni mwetu tayari kuanza Kutulewesha ili tutongoze hao Wahudumu wako wa Kike hapo sawa?
Zilianza kufumuka baada tu ya hayati kuondoka. Hizo zitakuwepo na zitaendelea kujengwa kika mahali. Nenda kule external na kitunda utaona zinavyoota fremu.
 
Kwanza ukifika pale mwanzoni utaona vibao huruhusiwi kukatisha Ile njia ya miguu baada ya saa kumi na mbili..Sasa hizo frem zikianza kutumika means lugalo yote itachangamka watu watakuwa wanakatisha sana kwenda mwenge na itakuwa busy njia....fremu zenye nyingi Sana na zimejengwa vibaya na kiholela Sana...imagine zote zifunguliwe na kuwebusy pale itakuwa hatari Sana kwa jeshi...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom