Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,061
- 16,753
Ninacho kiona mimi Majenerali wa jeshi la Ukraine watampindua Zelensky kuliko kuendelea kumuunga mkono huku nchi Taifa lao likiendelea kuteketezwa na kupoteza wanajeshi wengi pamoja na raia wasio na hatia,kumbuka Majenerali wengi wa Ukraine wanajuana na Majenerali wa jeshi la Urusi kutokana na kwenda kwao kwenye shule za kijeshi kwa pamoja enzi za iliyokuwa Soviet Union, hivyo tusione ajabu wakikubali ku-surrender kwa jeshi la Urusi ili kuinusuru Ukraine na baadae kuelewana na Russia,najuwa America haitaunga mkono jeshi la Ukraine kujisalimisha,lakini kumbe wafanyeje maana wanakuwa kwamba wanao angamia ni Waukraine na si Wamerikani - kumbe Waukraine wafanyeje ili wanusuru Taifa lao na raia ni wazi watakata shauri kujisalimisha na kuhacha kuendelea kufuata ushauri potofu wa utawala wa Merikani.Mrusi kushinda hii vita itakuwa ni tusi kubwa sana kwa US na mataifa makubwa barani ulaya.
Haya mataifa makubwa yameshaonyesha wazi wazi kuwa yapo nyuma ya Ukraine, ila wanajificha tu kwenye mwamvuli wa kuisaidia Ukraine silaha, ila wapo deep sana kwenye hii vita.
Ni kweli Ukraine itakuwa magofu matupu na mpaka sasa imepoteza wanajeshi wengi sana, ila mrusi kushinda vita hili halitotokea. Naiona hii vita ikichukua muda mrefu sana kumpata mbabe.
Vigumu kuelewa Zelensky anawaza nini!! Yeye masaa yote ni kuomba kuongezewa silaha pamoja na fedha, hataki kumaliza vita kwa njia ya mazungumzo - ubabe ubabe na ujeuri tu, huku Taifa lake na maelfu ya raia wasio na hatia pamoja na wanajeshi wakiuwawa kwa wingi,yeye hana habari anawasikiliza washauri wake wa Mataifa ya magharibi US in particular,who have nothing to loose wanawatumia wa Ukraine yao ya siku nyingi
ya kutaka kuishambaratisha Urusi kwa njia ya colour revolution/regime change kama ilivyo tokea huko Ukraine.