DOKEZO Wenye Hospitali binafsi wakataa kuwahudumia wateja wa NHIF kutokana na vifurushi vipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwahiyo ndiyo serikali ifanye wanavyotaka wao! Si wagome tu.
 
Kwa kweli tuombe Mungu atusaidie hawa Private hospitals na NHIF wafikie muafaka

Wagonjwa wenye Bima ya Afya ya NHIF wanataabika sana

Mungu wa Mbinguni utusaidie!
Yap..
Kuna wagonjwa wamelazwa wanaendelea na tiba muda huu kwa kutegemea hiyo hiyo NHiF, imagine waambiwe kuwa kuanzia kesho huduma hakuna!
 
Safi sana,

Hii wizara kwa sasa inaongozwa kwa propaganda mtupu.

NHIF ipo taabani kila siku na jumbe za kuhuisha uanachama hata kama expiry date kwenye card bado miaka miwili.

Ni ubabaishaji tu na kusumbua watu zoezi lenyewe ni makao makuu ya mikoa tu.
 
Hao wanaokataa na wafanye kama hao wahindi sijui kelele za nini kwanza kila hospital inaingia mkataba kivyake na NHIF kwahiyo anayetaka kufanya kazi na NHIF afanye anayekataa akatae.
Kila hospitali inaingia mkataba kivyake ila zote zinakuwa chini ya Umoja wao..

Na hivyo hivyo hata kila daktari anasoma kivyake na anafaulu kivyake ila wote wanakuwa Chini ya Baraza la madaktari nchini na ndo wanaotoa leseni..

Sasa mantiki yako sijaielewa tangu mwanzo..
Nini hasa Hoja yako?
Kwamba watu waendelee kuface unyanyasaji wanaofanyiwa?
Kwamba wenyewe wapate hasara kwa kuifaidisha serikali?

Kwa mujibu wa Takwimu zangu za Haraka Hospitali 80% ni za Private na Serkali ina 20% tu ya Hospitali zote..

Sasa sijajua kwako wewe unatetea nini Hasa kwamba Wakubali unyanyasaji kwa manufaa ya nani hasa?

Nipo tayari kuweka mjadala na wewe wa wazi kama uko tayari kutumia takwimu na facts
 
Kwahiyo ndiyo serikali ifanye wanavyotaka wao! Si wagome tu.
Hapana ila serikali hii katili haijali kuhusu maisha ya watu. Mkuu kuendesha hospital ,zahanati au kituo cha afya si lelemama ni gaharama kubwa naweza sema biashara ya afya ina kodi nyingi na running cost kubwa..
1.TRA
2.Kibali cha wizara kwa mwaka
3.Kibali cha maabara kwa mwaka
4.Osha
5.Fire
6.Kodi ya manispaa ya leseni.
7.Kodi ya jengo ya TRA
8.Kodi ya mwenye nyumba kama umepanga.
9.Tozo mbali mbali za mtaa/ Kata au halmashauri
10.Mishahara ya wafanyakazi tena hapa wanataka kila kada uwe na watu angalau wa tatu wakati wao hospital zao unaweza kuta hata mtoa dawa hamna au zahanat haina daktari na safi tu.

Hapo bado hujanunua vifaa tiba na dawa.
 
Wizara ya afya inafanya kazi kubwa sana kusaidia Wanachama wa Mfuko wa Bima ya afya unakua na manufaa kwao bila kuasiri uhai wa Mfuko. Maboredho hayo yameongeza huduma nyingi Muhimu na dawa ambazo hazikuepo awali.
Kumbuka hao wanachama wanakatwa hela zao.
 
Unyanyasaji gani unaozungumzia wewe! NHIF wao wanalipa kulingana na bei ya soko lakini nyie kina bwana tamaa na msio na utu mnataka malipo mara dufu.
Unasema sekta binafsi wanamiliki 80% ya hospitali nchini sawa lakini kumbuka zaidi ya 80% hizo hospital zimeanzishwa baada ya kuanzishwa NHIF ili wajipigie pesa na utajiri wa haraka haraka sasa wao wakubaliane na NHIF wasitishe watu kwa sababu manufaa zaidi wanayapata wao kuliko hicho mnachokisema eti wananchi ndiyo watateseka,kwanza jiulize hao wanaotumia bima ya afya ni asilimia ngapi kati ya mamilioni ya Watanzania.
Hawa watu wanatetea matumbo yao na wala hawatetei wananchi.
 
Umenifurahisha hapo,Kwamba kila kitengo kinatakiwa kuwa na mtaalam husika, ila wao Wana upungufu. Ole wako private hospital ikose hata mtaalam mmoja, inakuwa balaa.

Ndiyo maana ni nadra sana Mfanyabishara kuamua kuwa na Hospitali.
 
Mimi ni moja ya watu ambao wame experience vitu vya kushangaza sana nilipokuwa mwanachama wa NHIF ( kupata huduma hafifu) na baadae nikawa mtoa huduma ( nikihudumia wateja wa NHIF) kila nikitumia wastani wa Milioni 1 kuhudumia wateja wao, jamaa wananilipa wastani wa laki 4 hivyo nakuwa nishapoteza laki 6 ambazo nilikuwa nazo mfukoni kabla ya kuhudumia wanachama wao.

Hiyo ni sawa na kusema kila nikitumia 10M kuhudumia wanachama wao, automatically ningekuwa na uhakika wa kupoteza 6M ( confirmed)

Inashangaza sana wa kweli.
 
Serikali imehujumu watoto wa nchi hii, imefuta BIMA toto. Mamilioni ya watoto wanapata tabu.

Rudisha Bima toto NHIF
 
Hapo ilitakiwa mkurugenzi mkuu wa NHIF na waziri wa afya wajiuzulu mara moja kwa kuwachanganya watanznia na kumchosesha kura rais kwenye uchanguzi wa mwara 2025
 
Sawa ngoja tukajipange huko Mwananyamala, Temeke, Mabwepande na Palestina hospitals tukisubiri Huduma za X-ray, Usb, echo, ECG, holter monitor, trademill, MRI, ctscan, dialysis, physiotherapy n.k
 
Umenifurahisha hapo,Kwamba kila kitengo kinatakiwa kuwa na mtaalam husika, ila wao Wana upungufu. Ole wako private hospital ikose hata mtaalam mmoja, inakuwa balaa.

Ndiyo maana ni nadra sana Mfanyabishara kuamua kuwa na Hospitali.
Yaani mkuu tena wanakua wakali kishenzi [emoji16][emoji16][emoji16],imagine kizahanati wanataka uwe na CO watatu wakati wao mmoja tu[emoji706]

Biashara ya afya kwasasa ina mikono mingi ngumu sana utatoboa kwa kupambana mno.
 
Lakini kugoma kuwapa huduma wachangiaji sio utu.Sehemu kubwa ya watoa maamuzi serikalini hawaathiriki na mgomo wenu. Rudisheni kwa wachangiaji halafu mtoe muda wa serikali kukaa na kuzungumza.Anayeumia ni bi shomvi ambaye yupo kule kjjn na mtoto wake ni mwalimu s/m matopeni
 
Upo sahihi mkuu Agakhan hawapokei NHIF nikasema sirudii tena kukata hiyo bima
Strategies ni bonge la bima. Halafu nhif nao wana bima tofauti. Wanayo bima ya viwango hiyo unatibiwa hata aghakhan ila kina najali sijui wezesha hizo zinakua na limits kuna magonjwa hutibiwi.
Hapana Agakhan hawapokei NHIF ninayo timiza nililipia 1m point something nilienda kwa ajili ya meno walinikatalia hawapokei nikaenda Hindu Mandal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…