DOKEZO Wenye Hospitali binafsi wakataa kuwahudumia wateja wa NHIF kutokana na vifurushi vipya

DOKEZO Wenye Hospitali binafsi wakataa kuwahudumia wateja wa NHIF kutokana na vifurushi vipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Siwahelewi kabisa NHIF bima za wanangu wametumiatoka wakiwa wachanga picha ila mwezi sasa wanazifungia eti nilete picha mpya na nilipie 20000 cash kwa kila kichwa nimechoka kweli kwanini wasikate kwa salary na sisi ni watumishi
Ww utakuwa Mwalimu [emoji23]

Sasa picha za vichanga now watu wazima ukiambiwa ubadirishe unalalamika nn?, Kwan nn maana ya kuweka picha kwenye KITAMBULISHO??

Wakati unaajiriwa kadi si unapewa bure?

[emoji1745][emoji1745]
 
hata hivyo bado hospital za private nyingi nu matapeli tuuh....... haiwezekani tunaenda dirisha la dawa unaambiwa usaini lakini dawa anakuambia hamna kanunue hii ni haki kweli ?
 
Umoja wa Watoa Huduma Sekta ya Binafsi APHTA, Mashirika ya Dini (CSSC), na Bakwata wanapenda kutaarifu umma kuwa mazungumzo yaliyokuwa yakifanyika baina ya umoja huo na Wizara ya Afya. Kamati ya Waziri na NHIF yameshindwa kupata muafaka katika suala zima la kitita cha bei mpya zilizopendekezwa na Wizara kupitia kamati iliyoundwa na Waziri.

Kwa kuwa Wizara pamoja na NHIF wameamua kudharau maagizo yaliyotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya namna bora ya kumaliza suala hilo na kuamua kutangaza kitita hicho bila maridhiano, basi umma unatangaziwa kuwa vituo binafsi vya huduma za afya vitashindwa kutoa huduma hizo kwa wanachama wa Mfuko huo kuanzia tarehe 1 mwezi Machi 2024.

Ili kuepuka usumbufu, wanachama wa NHIF wanaombwa kuwasiliana na Mfuko wapi wataweza kupata huduma hizo.

Suala la hili limekuja baada ya Wizara ya Afya kutoa barua ya kuendelea na vifurushi vyao kwenye barua iliyoandikwa 27/02/2024.

Barua ilisema "Hivyo, Mfuko unapenda kukufahamisha kuwa utatumia Kitita cha Mafao cha Mwaka 2023 kuanzia tarehe 01.03.2024. Vilevile, unafamishwa kuwa, orodha ya huduma na bei katika Kitita hicho zinapatikana katika ofisi zote za Mfuko, tovuti ya Mfuko na kupitia mfumo wa Service Porta/. Aidha, Mfuko utaendelea kupokea maoni, ushauri na mapendekezo mbalimbali yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma bora za matibabu kwa wanufaika wake na kuendelea kuishauri Serikali ipasavyo."
View attachment 2918961
View attachment 2918951


Pia soma - APHFTA: Tutasitisha huduma za NHIF kuanzia saa sita usiku, wagonjwa mahututi tutawaongezea saa 48
Kila sehemu ni problems tu dah
 
Kwa mema huwa anasahau haraka, ila kWa mabaya utakuja kuniambia

Unafahamu kwamba watanzania wanachukia matajiri? Na wenye hospital binafsi ji matajiri?

Unafahamu kwamba wamatumbi tuna ubaguzi? Na kitendo cha hospitals za wenzetu waasia kujiunga kupinga nhif inaweza kuonekana ni hujuma?

Si unafahamu hao wenzetu waasia hata kwenu bishara ya dawa huonekana wanaihujumu na kuna some supportive evidence?

Na unakumbuka kwamba anayeumia hapa ni masikini na sio NHIF au hospitali za taifa?

Mwisho kabisa… enzi za magu mngegoma?

Tusiongelee kodi, fraud za overdHarding na usanii wa overkill

Wallahi hii kitu itawasumbua sana
Najiandaa kwenda hindumandal kunbe sitapokelewa? Wap naweza kupokelew
 
Back
Top Bottom