Wenye LINE nyingi za simu mnakera sana..!

Wenye LINE nyingi za simu mnakera sana..!

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
5,771
Reaction score
17,849
Binafsi nakerwa sana na watu wenye "line" lukuki za simu. Unakuta mtu ana line ya voda, tigo, airtel, zantel nk. Zote izo za kazi gani?? Matokeo yake kila ukimtafuta mtu utasikia mara..

"Nicheki kwenye airtel hiyo Voda haina chaji.."

"Nipigie namba ya tiGo, airtel nimeacha nyumbani"

"Hela umetuma mpesa? Aaargh hiyo line siko nayo sasa mpaka nirudi home.."

"Namba iliopo WhatsApp ni ile ya Zantel.."

" Unasemaje sijakupigia, kwani hukuona namba ya tiGO imeku miss call..?"

"Mimi si ndio nilikupigia kwa namba ya TTCL, mbona hujapokea.....?"

Jamani..! Mimi nnaposave namba yako, nasevu kwa JINA sio kwa mtandao uliopo. So ata sijui namba ya zantel inafananaje?

Ukiniambia nikucheki airtel yaani unanipa kazi ya ziada kuanza kutafuta namba za airtel hua zikoje ndio nijue ni ipi?

Mi nachoka sana..
 
Si ajabu wewe ndio tukushangae kwa nn hutaki kuendana na uhalisia wa mitandao yetu bongo,Binafsi nina laini zote na kila moja hua inakua na msaada wake tu kwa wakati usiotegemea ,Kampuni hiz zisizo na usawa bora wa huduma afu niwe na laini moja? Siwezi
 
Mimi nna laini 1 ya voda nilinunua mwaka 2000 na sijawahi kuwa na laini nyingine wala sijawahi kubadilisha namba. Mbona sijapata shida yoyote? Nyie mnachokitafuta kwenye kila mtandao ni kitu gani hasa?
 
Sababu kubwa ya hii mitandao mingi ulaji mkubwa wa data hauendani na matumizi ndio mana watu wamekuwa wanahama kila siku nimetumia tigo,voda nikahami halotel mitandao yote hii data zinakata fasta sasa nipo na Airtel naona wanaunafuu
Sasa ukiwa na line zote hizo mtu anakutafuta vipi, au mtu atajuaje saizi upo mtandao gani.? Na je kila ukihama mtandao ina maana na watu wote unawaambia sasa nimehamia airtel au unawaacha kule voda?
 
Wenye namba nyinginyingi hata wasikupe pressure especially kama sio business partners. Infact kama ni “watu baki” tu, wewe save namba yao moja tu inatosha. Acha wao ndio wakutafute na kila siku wakipiga watapaswa kujitambulisha
 
Mimi huwa nasave namba moja tu ya mtu. Mimi mwenyewe nina simu moja tu yenye line 2 tu. Sitaki masimu mengi mengi.
 
Mimi nna laini 1 ya voda nilinunua mwaka 2000 na sijawahi kuwa na laini nyingine wala sijawahi kubadilisha namba. Mbona sijapata shida yoyote? Nyie mnachokitafuta kwenye kila mtandao ni kitu gani hasa?
Huwa kwenye mishemishe zako unaendaga mikoani? Hivi unajua Kuna maeneo hapa hapa nchini Voda haikamati mpaka uwe na Halotel?
 
Huwa kwenye mishemishe zako unaendaga mikoani? Hivi unajua Kuna maeneo hapa hapa nchini Voda haikamati mpaka uwe na Halotel?
Naelewa mkuu. Ila kuna watu wapo hapa hapa mjini hawajawahi kwenda popote na wana line 4. Hao ndio wanaonichosha mimi
 
Back
Top Bottom