Wenye madaraka na mamlaka tendeni haki

Wenye madaraka na mamlaka tendeni haki

bnhai

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2009
Posts
2,832
Reaction score
2,390
Haya yanayozungumzwa juu ya ukosefu wa haki yanatia doa na dosari nchi yetu.

Jeshi la polisi limekuwa ni mtuhimiwa namba moja kwa ajili ya uonevu.

Ipo mifano hai huko barabarani jinsi rushwa ilivyotamalaki. Lakini pia kuna vituo km Oysterbay na Central DSM, kule wamejaza mali za watu kama magari na pikipiki ambao wamiliki hawana Kesi isipokuwa wanazungushwa ili rushwa itoke.

Ni wakati sasa tubadilike.
 
Nilinde nikulinde.Police na ccm wanalindana kupora haki zetu.
Mmoja anatupora kura, mwingine anatupambika kesi, rushwa.
Nilinde nikulinde
 
Polisi ya Tanzania wanakitumikia chama dhalimu-CCM badala ya kuwatumikia wananchi,sasa unategemea waache kuwa madhalimu?
 
Polisi waongezewe mishahara ili waondokane na rushwa
Hakuna dawa ya rushwa tofauti na uadilifu na kufuata misingi ya kazi yako.

Mishahara mikubwa si dawa ya rushwa. Mtu anakupa rushwa mfano ya Milioni 12 usindikize mzigo wake ambao huujui kwa mshahara wako wa laki 9 utakataa kisa tu umeongezewa laki moja kwenye mshahara wako.

Uadilifu ni kitu cha kwanza na uzalendo.
 
haki ni neno pana sanaaa, itakuwa vyema ilikichambuliwa na kuchambuka ka biriani la ijumaa
 
Huu mfumo wa utoaji haki kwenye maeneo yote ni muhimu upitiwe. Watu wangapi wanadhulumiwa na polisi na hata mwendazake aliyafanya haya sana.
 
Gaidi hatendewi haki dawa ya gaidi ni kumlima shaba
Magaid wameuana
JamiiForums683344064.jpg
 
Back
Top Bottom