Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Dingi angu huwa sio mchapaji ila ana sauti kama ya radi, mweusi tii na giant kiasi. Nikikosea akipiga biti nlikua najikojolea bila kuchapwa

Akirudi home kutoka kwenye mishe zake watoto tulikuwa wapole, tunaona amani imetoweka home

Mtaani tuliheshimika na watoto korofi, tulikuwa hatuchokozwi kwa sababu watoto wa mtaa walimwogopa mzee wetu mno

Kinachonishangaza ni kwamba, mzee sio katili na sio rahisi kwake kumchapa mtoto ila sisi tulimwogopa tu

Cha kushangaza zaidi, mpaka leo sijazoeana sana na mzee wangu... Mungu ampe maisha marefu!
 


hahaha hv hao wazee miaka hii wamepoteleaga wapi jaman!hv kuna mtu ana mume mkali km mababa zetu jaman !hahaha waume wa siku hiz kutwa kubet na kurud hom usk mkali !utamjuaje sasa mzaz wako !lol !wapo softyyy had kero ! nimecheka eti sauti ya radi hahhhhhhhhhh
 
Duh wazee wa zamani kiboko... Mimi kwa bahat mbaya wazaz wangu walifariki ningali mdog mnoo RIP MAMA na BABA. Ila nimelelewa na mama yangu mdg jamani alikua anachapa kosa dogo tuh anakuchapa had majilan wanamuachanisha lkn wapi.

Nakumbuka Christmas ya 2007 cku iyo aliandaa maandaz sasa alipanga yatumike wiki nzima kama mjuavyo ckukuu chakula kinapikwa watu wanakula na kufurahiaa nakadhalika watu wote waliondoka nyumban nikabaki mimi pekeangu, akaja mama mmoja na mmewe wakaniomba chakula nikawapa wakala wakat wanataka kuondoka nikawachotea maandaz kdg kwenye mfuko wakaondoka. Jion mamdg alivolud aliona maandaz yamepungua akaniuliza nan kagawa maandaz nikajib n mimi mamdg alinichapa nusu kuniua
Sitasahau aisee kile kipondo kwa bahati mbaya bado hajabahatika kupata mtt labda ni vile hajui uchungu wa mwana maana dah stakaa nimsahau mamdg wangu.
 
Hahahahhaha tulipigwa hadi tukawa sugu.
 
haha
haahaahahaahaa hatari sana
 
My ribs jamani, nimecheka mno mpaka watu walionizunguka wakawa wananishangaa
 
Nikianza kumuelezea mdingi wangu, afisa wa jeshi mstaafu, kwa hakika hata sasa hivi nikiendaga home nikiskia tumekaribishwa menu ni either ninyuti chumbani hadi amalize kula na mimi ndio niende mezani au niwahi fasta mezani nipakue nikalie chumbani. Huyu mzee ni babiloni sijawahi ona dunia hii. Alishawahi kuja shule enzi hizo makongo niko form3 akaongea na hedmasta kipingu akaitisha folen ya shule nzima nikalambwa stiki shule nzima ikishuhudia na mzee wangu, aisee sitasahau.
 
Sitasahau ile kichapo ya mzee baada ya
Kuchoma moto zizi kwa lengo la kuandaa mishkaki
 
Yaani toka jana nlikuwa staki kufungua huu uzi.....hapa nimecheka mpaka wakukuu wananshangaa.....muonekano wangu km le kibamiaazz imagine hilo cheko
 
Hahaha basi kumbe dingi ako ukauzu wake una afadhali.

Madingi makauzu/watabe hata kwa watoto wao kike hawawezi kwenda kabisaa achilia mbali kulala mpk asubuhi.Mtu yuko radhi aje kama ni dar ana inshu zake afikie hata kwa mdogo wake au lodge lkn sio kulala kabisaaa mpk asubuhi kwa binti yake.
 
Vinginevyo mkuu ungekua unashinda mortuary kule vitongoji

Sent from my SM-N910V using JamiiForums mobile app
 
Tulivyoishi na mzee wangu mpaka sasa nimekua mtu mzima na kaa nae meza moja tunakula wote bia bado siamini. Mzee wangu ni among the meanest daddies in the world. Nafkiri labda na ujeda nao kwa kiasi kikubwa ulichangia. Alikua na matukio mengi tu, nakumbuka siku moja wakati niko mdogo tunaishi molemu monduli, alinichukua akanipeleka saluni town nikaenda kunyolewa vizuri nikapendeza nikawa smart. Alivyonirudisha home ye akaenda zake maeneo ya resort kupata UGIMBI kidogo. Mimi kubaki home si nikachkua mkasi nijiweke 'wei' kwenye panki langu? Alivyorudi nakunikuta vile, nilikula kipondo then akanambia si unataka kuweka wei? Kaa nikuweke wei vizuri, basi akachukua mkasi na kiwembe .. alivyoninyonyoa kama kifaranga cha kuku nikawa sitaminiki, ilibidi kaka mmoja alikua jirani yetu animalizie upara kwa kiwembe aisee. Kuna moja hiyo ya niliharibu tape yake ya radio na nyinginezo daaah..... sema mpaka saivi hua tunazinguana kiaina ila ananikubali na mimi namkubali. I'm indeed, my father's son..

Sent from my SM-N910V using JamiiForums mobile app
 
Vinginevyo mkuu ungekua unashinda mortuary kule vitongoji

Sent from my SM-N910V using JamiiForums mobile app
Wacha kabisa broo, alikuja kumwambia bi mama ndugu zako kama wakija hapa kwangu hawaswali basi waambie wasije hapa. Nyumba hii lazima watu waswali, kudaadeki maza wadogo wote wakawa wakija lazima waswali japo kumzuga lakini swala ni lazima
 
baba yake sio mtata... analala mpaka alipoolewa mwanae...

wazee makauzu hiyo kitu ni mwiko


 
Wacha kabisa broo, alikuja kumwambia bi mama ndugu zako kama wakija hapa kwangu hawaswali basi waambie wasije hapa. Nyumba hii lazima watu waswali, kudaadeki maza wadogo wote wakawa wakija lazima waswali japo kumzuga lakini swala ni lazima
Hahaha, chief umeish sana pemba? Nimefanya kazi Al-Khamis Camp
 
Hahaha, chief umeish sana pemba? Nimefanya kazi Al-Khamis Camp
Miaka mitatu tu mkuu nlikuwa naishi mkoani flats za mapinduzi pale na wazee, wazee wakanihamisha maana nlikuwa sisikii ajabu mpaka mwalimu nilimpiga mawe siku moja kwa sababu alinichapa kosa halikuwa langu. aisee mzee wangu amefanya kazi kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…