Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

hahaa, na vocha ikiisha inabidi ujiunge umpigie au ndio imetoka?
 
Amenifinya sana masikio
Na kunichapa pia

Ila ni zamani mno nikiwa mdogo.
Kwa wazazi lazima mmoja awe ndio mbabe, mtata, mkali na mwengine ndio awe kimbilio
Kwako inaelekea baba ndio alikuwa kimbilio , mama akaona yeye ndio avae jukumu la kuwa mtata
 
Poleni sana..
Baba angu hakua mkali..
 
Kwa wazazi lazima mmoja awe ndio mbabe, mtata, mkali na mwengine ndio awe kimbilio
Kwako inaelekea baba ndio alikuwa kimbilio , mama akaona yeye ndio avae jukumu la kuwa mtata
Huwa nammiss sana mzee wangu.
Hakuwahi nipiga hata siku moja.

Maza sasa[emoji16][emoji119]
 
Mimi mwonekano wangu wanasema nanuka"ukali" hata nikitembea njiani au nikienda sehemu...na ni kweli sipendi masihara...hata kuku zikiniona zinaingia bandani ,nna spirit ya mzee alikua anatisha.
 
Huu uzi ni heshima kwa wazee wetu kama magufuli.

Wale walikuwa na aina moja ya malezi
Athari yake ni kumfanya mtoto awe na tabia njema, kwa upande mwingine mtoto anakuwa na hasira, chuki na woga
 
Umenikumbusha kada wa ccm na tajiri who lived CSR to the fullest Cosmas Kadege, Mbeya moja hio R. I. P Mwamba wa kweli mwenye utu na upendo
 
Utafanyaje labda?
Mambo ya Ustawi sio?
Nyinyi ndio chanzo Cha ushoga na ujinga
Kwamba mashoga wote baba zao walikuwa wapole au walikuwa hawapigwi?

Acha kuhalalisha ujinga. Kwanza wanaume wengi wenye tabia hiyo imetokana na ukatili wa wazazi wao maana mzazi ukiwa karibu na mwanao utajua tu ameanza tabia za kijinga.

Kumpiga mtoto is the laziest way of parenting. Wazazi wa zamani walikuwa wavivu kwenye kulea watoto ndo maana walikuwa wanakimbilia kwenye kupiga since it's easy.

Anyway we piga tu mwanao
 
Mzazi akifikia hatua ya kupiga jua huko pote alishapita yaani kashauri ila imeshindikana..
 
Mimi ngoja nikae kimya maana staki nikumbuke kichapo nilichopata mwaka 1991 kisa kudokoa nyama, RIP mzee wangu alikuwa my best friend
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ Ngoja nimu bless Mzee wangu walau kwa Post hii imenikumbusha mabli pia RIP mzee wangu.
1. Ile tabia ya watoto wa zamani siku ya mwaka mpya ile saa sita kamili usiku tulikua tunapiga madebe..wengine wanachoma matairi barabarani..wengine wanapiga mawe batini kwenye nyumba za watu πŸ˜„ yani imradi shamla shamla tu.
Basi bhana mwaka sikumbuki ila ilikua ni saa sita kamili nipo nyuma ya nyumba yetu na bro zangu 2 ile mwaka mpya..na mambo mapya nikarusha bonge jiwe kwenye bati la jirani yetu mzee akasikia wew ile natoka ivi nakutana na mzee uso kwa uso πŸ˜‚πŸ˜‚ kilichotokea usiku huo mpaka leo ndiomaana sijasahau.

2. Vijana wa kanda ya ziwa enzi hizo kuogelea kwa kwenda mbele kikundi chetu cha watoto wa mtaa tilikua na kasumba za kwenda mapumbani kuruka soti tukimaliza tunaenda ziwani kuogelea au kwenye bwawa ivi lilikuwepo, lile bwana inasemekana palikua na majini yale yanaitwa chunusi, ilikua kila mwaka lazima mtu afie mle inasemekana ananyonywa damu na chunusi..basi mzee wetu alitupiga marufuku kuogelea ama kwenda kwenye lile bwawa πŸ˜‚, siku moja mimi na bro angu tukaliunga na camp yetu hao kuogelea kule kule bwawani inaposemekana kuna chubusi Mzee alipotoka job akatuulizie akenda uwanja wa mpira akijua tupo kumbe kuna vijamaa vilikataa kwenda bwawani vikatuchoma sie tumeenda na wengine Ile tunaogelea mzee huyo kaja kule na pikipiki ya kazini πŸ˜ƒ mi na broo tulivyomuona tukazamia chini asituone katuangalia wee hakutuona akasepa ila kajua tupo pale ila tumejificha..kimbembe tuliporudi tuka act tumetokea mpirani kuna bro mkubwa alipotuona akaanza kucheka anatuuliza mbona tumepauka tukasema tulikua mpirani zile vumbi... jion ivi mzee akarudi akafanya kama hana neno nasisi ile tumeingia ndani tu nayeye kaingia akafunga mlango mkubwa akaja chumbani kwetu na kamba akatufunga na bro mdogo wote wawili stick za pale πŸ˜‚πŸ˜‚ mixer makofi na kukanyagwa kama nyoka πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ yeye ndo sababu hadi leo sijui kuogelea wala kuruka soti japo natokea kanda ya ziwa πŸ˜‚πŸ˜‚

3. Hii nayo japo ilikua dk 1 ila sijaisahau enzi hizo picha za kihindi zimenikaa akilini mzee kanituma dukani nikaenda kumletea kitu ile narudi nimpe nikakunja vidole kama namrenga mzee kwa bastola ya mkono ile unakunja vidole afu vidole 2 vinakua kama kicha cha pistol za wahindi afu unafanya dishi dishi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nilikula bao hilo angekuwepo Mithuni chakalaboti angenionea huruma alivyoniponza mpaka leo sihitaji kufundishwa discipline kwa wakubwa maana toka enzi hizo nilifuzu πŸ˜„
 
Mi ningehama kabisa nyumbani. Kipigo gani hicho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…