Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Halafu experiments za foolish age na balehe mnaziletaje kwenye jamvi la wazee?
Kuna formula ya utamu wa mwanamke kwa kulinganisha umbile lake la nje, nani aliconlude hilo?
Kweli leo nimeamini kuwa kuna baadhi ya wanaume hadi wanaota vipara vya mvi na kupinda vibyongo, bado hawamtambui mwanamke!
Unawezaje kutia sifa ya jumla ya udhaifu wa hisia za ubongo wako kwenye kadamnasi?
Mwingine anaoa amiliki sauti ya mhusika tu. Hiyo biashara ya matege ukimletea mtaelewana?
Umbile lolote lile la mwanamke ni 'tunu' kwa mwanaume.
Ni kama yalivyo mavazi. Chukulia mfano wa mavazi aina aina, ndiyo utaelewa maana halisi.
Usilolipenda wewe, utakuta mwingine kalivaa na limemtoa "chicha"!
Sasa hapo unaweza ukasemaje?
Ifikie mahali muelewe kuwa mwanamke unayemuona wewe wa nini, mwingine anafikiria atampatapataje?
Hahaha
Mzee alikua anasema kama unajiona upo vizuri njoo tuzipange.

Alikua hapendi mtu anyoe kipara, kaka yangu akawa mbishi siku hiyo karudi home na kipara. Mzee akamwambia kimbia ukiona upo mbali sema tayari.

Jamaa akakimbia mzee anaona mdau anasogea tu hasemi tayari, akamuungia. Dakika kadhaa mbele tunaona kaka anarudishwa kabebwa begani.
Kufika home akaambiwa tuzipange, ghafla jamaa kapiga magoti analia anaomba msamaha.

Mzee akamwambia adhabu yako utakua unapaka kiwi kichwa hadi nywele ziote.
 
Nyie watu acheni kuwasingizia wazee wenu ukoloni, dingi yangu ndo mwenye cheo chake kwa matimbwili yake haya....
1. Mama yangu hadi ana miaka hamsini lakini akizingua dingi anampa kichapo heavy, afu mtu ajifanye kuingilia atakiona cha moto.
2. Nusu ya watoto wake tumeoa na kuolewa lakini ukienda kijijin kusalimia mwisho kuingia kwake ni saa 12 vinginevyo unachezea za chemba.

3. Kila siku asubuhi lazima umpigie simu na kumwambia shikamoo.

4. Aliwahi kunikosa panga, kama si kaka yangu kumzuia leo ngekua marehemu, na huyo kakangu alilazwa wiki nzima akiwa hajitambui hospitalini

5. Kuna mke wa mshikaji kitaani alikua ananishobokea sana nkaona isiwe taabu nkamtia neno tukaanza kufanya yetu, basi siku moja tukazinguana nkamtishia ntamsema kwa mumewe kwamba ananitaka kimapenzi, yule dada akapaniki akajua ni kweli akaenda nigeuzia kibao kwa mumewe kuwa namtaka kinguvu, wacha jamaa aje kunisemea kwa faza, siku hiyo dingi alirudi usiku alichofanya ni kunihamishia bavuni na kunimwagia ndoo ya maji akalock mlango, asubuhi nafunguliwa mlango kucheki jamaa huyu hapa na mke wake....... akamuamuru jamaa anichape viboko kadiri atakavyo mbele ya mkewe.........
 
Bahati mbaya sijaishi na baba kwa muda mrefu, lakini kwa mtazamo Mzee wangu ni Mkali kiasi siyo sana na akizingua na mm nina mzingua tu, si unajua watoto wa siku hizi katika malezi bora tuliyopitia. [emoji1] [emoji3]
Tabia mbaya
 
Mimi nakumbuka siku ya mwisho dingi kunichapa.....alinikuta nasoma saa sita usiku yeye yuko nzwiiiii......akaniuliza kwa nini sijalala, nikamjibu huoni nafanya nini.....akajaa povu....akafuata fimbo kwani alikuwa anaziweka sehemu......akaanza kunitandika......nilitulia tuu, ila ikafika wakati nikasema leo lazima nimuonyeshe huyu mzee......niliikamata ile fimbo na nikaivunja vipandevipande.....kulikuwa na music system ya Phillips niliifuata na nikaivunja vipande vipande.......nikaenda kwenye kabati la vyombo....nililiangusha na almost vyombo vyote vya udongo vilivunjika.......ndio ilikuwa mwisho wa mzee kunichapa......
Ulichemka sana kuvunja vitu vya home
 
Natamani nichangie ubandidu wa mzee wangu ila sioni hata kimoja, alikuwa hana noma mzee wangu..R.I.P Dad
 
Muuza ubuyu, uyo jamaang n askar wa kutulza ghasia (FFU), mkoan Irnga uko, cpat picha kma jamaa karith element za babake
 
Nouma Sana, mpaka Leo sina mazoea ya kumtext ama kumtumia text WhatsApp, napiga simu nikiwa na shida maalumu tu.

Anakwambia,siwezi kupiga simu kama sina suala la msingi
[emoji23] [emoji23] hatari sana
 
nyinyi nyote trella... dingi yangu maarufu sana maeneo ya yombo kila mtu hadi majirani wanamuongelea enzi zake.. kuwa alikuwa hatari...

enzi hizo dar bado wenyeji wengi mitaa ya uswahilini kuna ngoma za wamakonde na wazaramo kibao....

kuna siku wazaramo walipita na kigodoro chao mchana nje ya ukuta dingi alikuwa anapalilia majani... wazaramo kibao kama 200 hivi.. dingi akawasimamisha.. na kuwauliza hivi kila kabila hapa likisema lipige ngoma yake si itakuwa balaa.. akawaambia ngoma za wazaramo kwa mchaga, mkurya, mnyakyusa, mhehe etc ni usumbufu.. kama wanataka ngoma wakapigie kwao msanga huko ambapo hakuna makabila mengine... wazaramo wakacharuka si unajua wanaongea sana wakaanza msuta dingi... mzee akajifanya amezidiwa.. akawaambia amependa hoja zao wamsubiri awaletee zawadi ya mwali wao...

wale wazaramo walivyo wajinga wakamsubiri kweli... dingi kazama ndani.. chumbani kwake kachukua gobole lake... kilichotokea ilikuwa story yombo mzima hakuna ambaye haijui..... dingi alivyotoka tu nje na gobole wakaanza kimbia na wapiga ngoma wakaacha ngoma zao.. dingi akazigeuza zile ngoma ni mafunzo ya kulenga shabaha... zile ngoma kubwa akazitia risasi zote.. na gobole lina kelele balaaaaa... mtaa mzima ndanii.. yeye anazitia shaba tu.

hawakurudi tena na ngoma zote zikawa zinapita mtaa wa pili.. hazipiti njia ya kwetu wanaogopa mwanajeshi mstaafu

dingi alikuwa anatubondaaa hadi mama analia yeye...

anakwambia ndani ya nyumba rafiki yake mke wake tu.. ana gari lake land rovee ukiingia humo huruhusiwi kukaa kiti cha mbele ni cha mke wake tu mama yetu.... na hata ukikaa siti ya nyuma ukipigwa wimbo mzuri huruhusiwi kutikisa kichwa anakushusha... enzi hizo watoto wake alikuwa anatushusha kwenda kanisani eti tunatikisa kichwa kwenye gari lake tukisikia mziki mzuri.. so kanisani inabidi twende kwa mguu.. yeye na mama ndio kwenye gari
DAA MKUU KAMA NI KUPIGA KURA NAONA DINGI YAKO KASHINDA
 
Nimelelewa na Baba mdogo ila mtata kinoma,kuna siku alisafiri huku nyuma mi nkaacha kwenda chuo(madrasa),mama akiniambia niende chuo namwambia 'kausha' basi siku aliorudi akaambiwa taarifa zangu,mzee akaniita akiwa na gunia la bakora,akaniambia nivue nguo zote,baada ya kusaula alinipa kichapo ambacho siwez sahau,baada ya kunichapa sana akawa ananizungusha mtaani mm mbele yeye nyuma huku akiniteremshia mvua ya bakora tena akawa ananiambia niwe naimba hv,mm cna akili,mm mwehu,mm kichaa nisiependa chuo,basi alinikimbisha mchaka mchaka wa bakora mtaa mzima,nilvyoona hali mbaya na yeye hana dalili za kuniacha nkakimbilia msikitini maana ilikua mida km ya saa 2 hv usiku,mzee nkajitosa msikitini mzima mzima nliwakuta na wanakimu kwa ajili ya kuaza swala,hapo ndo ikawa ponea yangu maana wazee wa msikiti walimuona anisamehe japo alikua mgumu kunisamehe lkn mwisho akakubali kunisamehe,yy alitaka aendelee na lile zoezi usiku kucha,basi asubuhi yake nkaamka nkiwa na vidonda vya haja,alafu mtaan ikawa gumzo kila nnapopita nachekwa tena hadi na madem zangu,alafu pale mwanzo alipokua ananiamuru nivue nguo ile chupi nkawa cjaiweka chini,maana nlipovua chupi tu kichapo kikaanza kwa hiyo nkakosa nafasi ya kuiweka chini,hivyo mda wote wa mchaka mchaka wa mateso ile chupi nlikua nayo mkononi,(tena kipindi nakimbizwa na fimbo kulikua na kundi la watoto walikua wameunga ule mchakamchaka huku wakishangilia mm nnavyoadhirika) sasa baada ya kuingia msikitini wale mashekhe wakanitoa nje ili waongee na mdingi ili anisamehe,sasa mdingi alivyofika tu akanichapa bakora ya mkono tena ule mkono nlioishika ile chupi,kutokana na mshituko ile chupi ikaniluka na ckujua imelukia wapi kwa wakat huo,kumbe ile chupi ilirukia juu ya paa la msikiti,asubuhi yake watu(hasa watoto wenzangu) wakaiona juu ya bati basi ikawa stori tena kila nkipita nachekwa na kukejeliwa juu ya kile kichapo na chupi yangu kuwa juu ya paa la msikiti,ile chupi ilifanya tukio langu lisisahaulike haraka halafu ikanishangaza ilikua haianguki hata mvua iminyesha kias gani,ilikaa zaidi ya mwezi mmoja pale juu hadi ilipodondoka ndo nkaanza kua na amani maana watu wakaanza kusahau kile kipondo changu,hadi leo nmebaki na makovu km kumbukumbu ya lile tukio,USIOMBE YAKUKUTE
Pole mkuu.. lakini vipi baada ya hapo ulibadilika? ulianza kuhudhuria madrasa?
 
Hakuna mtu alikuwa na dingi mkali kanda ya kati kama mimi.

Yani Tabora, Dodoma na Singida nna uhakika mzee wangu ndio alikuwa mzee mkali kuanzia miaka ya 1976 mpaka alipofariki mwaka 1997.

Mzee alikuwa fundi umeme, ndani alikuwa na nyaya za umeme za kutosha siku ukifanya kosa anachukua nyaya anaikunja mara mbili anaanza kukupa kichapo. Ukishika umefuta

Maumivu ya nyaya ya umeme yasikie ndugu, ya mkanda yanasubiri sana. Maumivu ya nyaya nadhani ilibaki kidogo yafikie kwenye maumivu ya mapenzi (hahaha, joke)

Tulikuwa na choo na majani, siku moja nikawa nachezea kibiriti nikachoma choo then moto ukaenda kugusa kenchi za nyumba ashukuriwe Mungu majirani waliwahi kabla moto haujapamba lakini aliporudi mzee chamoto nilikiona, nilikuwa siwezi kukaa wiki nzima mfululizo kalio zimevimba balaa.

Pamoja na yote lakini nakukumbuka sana mzee wangu (RIP).

We mzee wako alikuwa mkali? tupe story


naweza sema mzee wangu yuko the same but nilimchukia sana r.i.p tulikuwa kama simba na chui ilibidi nikasome nje ya nchi japo tulikuwa tunawasiliana fresh but nilikuwa na hate izo brutality nilikuwa napata na alijua ivo. I miss the good about him but that is not how to raise kids alifeli sana mzee aliprove a failure and exmple of a rogue leader and the way pia alivokuwa anamzibua bimkubwa asee ilikuwa hatari yani familia yako mzee ulivokuwa unaikuza imenifunza sana kama mwanaume kwakuelewa athari hiyo kwa familia yangu haijawai pata shida yoyote na mistreatments zozozte cos I have seen and learnt from the worst example.

THANK GOD SINA ILO PEPO MANINA!
 
Back
Top Bottom