Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Kibishi tu sasa hivi nikimtazama huwa naona kama Bro wangu hana noma, Mara ya Mwisho ananipiga ilikuwa niko Darasa la nne, alikuwa yupo safarini ila asubuhi aliniita chumbani akanipa majukumu ya kufanya, Nimeamka tu nikaenda kusakata kabumbu nikijidai Maradona hadi saa 12 jioni ndipo Maradona anarudi nyumbani akamkuta baba yake kafika hakuna kazi yeyote iliyotendeka.

Kipigo cha Kufa Mbwa kikamhusu Maradona, Kilichoniokoa niliona nikiendelea kulia na kupiga kelele nitakufa kwa ngumi na makofi ya Baba yake Maradona basi Nikajidai nimezima anapiga sitikisiki wala kugeuka kapiga kama dakika 1 kashituka, akajua Maradona Kafariki, alikuwa na buti moja chini limeandikwa Base akanikanyaga nalo duh maumivu yale yalimtoa chini Maradona akasepa mwendo wa Kimondo kuelekea kusikojulikana.

Tangu Siku hiyo hakunipiga tena.

mkuu wa
Raphael wa Ureno naomba kumtunuku mzee wako vyeo vyake
 
Awa wazee wetu yani wao kupiga mtoto ni sifa kubwa kwao tena utakuta wanakaa kwenye vijiwe vyao wanaadithiana kwamba wanajua kupiga .Haya mambo yakupigwa pigwa ovyo bila sababu yalinijenga kuwa na tabia ya uwoga,hasira na roho ya chuki (nashukuru Mungu nilijtambua nkazpinga izo roho) kwn mzee alkua anapenda kuogopeka kuliko kuheshimika.Mbali na kupgwa wazee wanakuaga na kauli mbaya sana juu yetu tukiwa wadogo utakuta mzee anakuambia yan ww ata ukisoma vp hutokuja fanikiwa maishani na stokuja kula ata shiling yako halafu baadae anakuja kukulia eti uyu ndio mwanangu mpendwa msomi.
Asee unenigusa penyewe[emoji106]
 
Mshua alinichapaga viboko mbele ya demu wangu alikuja kusuka.
Dingi amekuja mchana kula chakula akakuta hakuna maji hata ya kunawa mikono, kubabake alinichapa sticki hizo.
Demu wangu alikua nje anasukwa na dada yangu, dingi ananichapia sebuleni.
Kwa kuwa nilikua sitaki demu wangu ajue kama nachapwa, nikawa najikaza sipigi kelele.
Dingi akajua viboko havini umizi, akaanza kunipiga na mavibao, kubabake nilivimbaga mikononi.
Mara Paaaap nikatoka na mindoo kwenda kuchota maji, mialama ya viboko kwenye matako, mgongoni, mikononi.
2001 hiyo Kiloleni Tabora
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Dah. Nimecheka sana. Mungu awarehemu madingi wote waliotangulia.
 
nakumbuka mwaka 2001, kaka angu alikuwa anachezea kiberiti. basi akaenda kuchoma bafu, mzee alipo rudi alimfunga miguu akamning'iniza miguu juu, alichezea stiki vibaya mno.
 
Mtoa mada ushawah kufungiwa kwnye kibanda cha mbwa.....tena sio wa kipolepole????
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu malizia mm nikiwa na miaka saba nimelala nje mno mno, kosa umefanya asubuhi anajifanya hajui subiri aende kunywa akirudi usiku saa nne au sita ujue kipigo na kulala nje nimelala mno kwa majirani, anajari mifugo kuliko binadamu ole wake akute mifugo yake ina njaa ujue hapo ni msala mkubwa km kuna mtu amefariki,
 
Mzee alikua anasema kama unajiona upo vizuri njoo tuzipange.

Alikua hapendi mtu anyoe kipara, kaka yangu akawa mbishi siku hiyo karudi home na kipara. Mzee akamwambia kimbia ukiona upo mbali sema tayari.

Jamaa akakimbia mzee anaona mdau anasogea tu hasemi tayari, akamuungia. Dakika kadhaa mbele tunaona kaka anarudishwa kabebwa begani.
Kufika home akaambiwa tuzipange, ghafla jamaa kapiga magoti analia anaomba msamaha.

Mzee akamwambia adhabu yako utakua unapaka kiwi kichwa hadi nywele ziote.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mshua alinichapaga viboko mbele ya demu wangu alikuja kusuka.
Dingi amekuja mchana kula chakula akakuta hakuna maji hata ya kunawa mikono, kubabake alinichapa sticki hizo.
Demu wangu alikua nje anasukwa na dada yangu, dingi ananichapia sebuleni.
Kwa kuwa nilikua sitaki demu wangu ajue kama nachapwa, nikawa najikaza sipigi kelele.
Dingi akajua viboko havini umizi, akaanza kunipiga na mavibao, kubabake nilivimbaga mikononi.
Mara Paaaap nikatoka na mindoo kwenda kuchota maji, mialama ya viboko kwenye matako, mgongoni, mikononi.
2001 hiyo Kiloleni Tabora
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hi I Kali nimecheka balaa
 
amefariki mwaka jana akiwa na miaka 79.. ila mpaka uzee wake hadi wajukuu walikuwa wanamuogopa.. anacheza nao ila akiamua anawatia viboko..

kuna mjukuu aliua kuku wa nyama... mama anafuga kuku sasa kuna siku wanawapa kuku dawa kuna mjukuu akaenda kumkamata kuku wa nyama bahati mbaya akamnyonga mzee alikuwepo jirani akaenda mtia fimbo mjukuu hadi mama yake mke wa kaka akataka kulia... bro akamwabia kama unataka kulia kalilie chumbani maana mzee akikuona unalia hapa anaweza anzisha ugomvi mzito na usikanyage tena hapa
(RIP mzee)....
Huyu natamani hata kuona picha yake
 
nyinyi nyote trella... dingi yangu maarufu sana maeneo ya yombo kila mtu hadi majirani wanamuongelea enzi zake.. kuwa alikuwa hatari...

enzi hizo dar bado wenyeji wengi mitaa ya uswahilini kuna ngoma za wamakonde na wazaramo kibao....

kuna siku wazaramo walipita na kigodoro chao mchana nje ya ukuta dingi alikuwa anapalilia majani... wazaramo kibao kama 200 hivi.. dingi akawasimamisha.. na kuwauliza hivi kila kabila hapa likisema lipige ngoma yake si itakuwa balaa.. akawaambia ngoma za wazaramo kwa mchaga, mkurya, mnyakyusa, mhehe etc ni usumbufu.. kama wanataka ngoma wakapigie kwao msanga huko ambapo hakuna makabila mengine... wazaramo wakacharuka si unajua wanaongea sana wakaanza msuta dingi... mzee akajifanya amezidiwa.. akawaambia amependa hoja zao wamsubiri awaletee zawadi ya mwali wao...

wale wazaramo walivyo wajinga wakamsubiri kweli... dingi kazama ndani.. chumbani kwake kachukua gobole lake... kilichotokea ilikuwa story yombo mzima hakuna ambaye haijui..... dingi alivyotoka tu nje na gobole wakaanza kimbia na wapiga ngoma wakaacha ngoma zao.. dingi akazigeuza zile ngoma ni mafunzo ya kulenga shabaha... zile ngoma kubwa akazitia risasi zote.. na gobole lina kelele balaaaaa... mtaa mzima ndanii.. yeye anazitia shaba tu.

hawakurudi tena na ngoma zote zikawa zinapita mtaa wa pili.. hazipiti njia ya kwetu wanaogopa mwanajeshi mstaafu

dingi alikuwa anatubondaaa hadi mama analia yeye...

anakwambia ndani ya nyumba rafiki yake mke wake tu.. ana gari lake land rovee ukiingia humo huruhusiwi kukaa kiti cha mbele ni cha mke wake tu mama yetu.... na hata ukikaa siti ya nyuma ukipigwa wimbo mzuri huruhusiwi kutikisa kichwa anakushusha... enzi hizo watoto wake alikuwa anatushusha kwenda kanisani eti tunatikisa kichwa kwenye gari lake tukisikia mziki mzuri.. so kanisani inabidi twende kwa mguu.. yeye na mama ndio kwenye gari
[emoji23] [emoji23] uwiii nimecheka sn
Aisee
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] lol
 
Ngoja nami niandike mambo kadhaa ambayo yamenifanya niamini hakuna mzee kama mzee wangu.

1. Siku moja tumeenda kwenye ngoma masikini nikaongozana na dada zangu kwenda huko mzee alikuwa yupo safarini akarudi akakuta milango yote imefungwa na kuku wapo nje yaani full tafrani hapo nje, wazee wa ngoma tukaingia kwa mbwembwe shikamoo baba!!! Hahahha tukafungua mlango kuku wakaingia ndani msosi ukapikwa na watu wakala.

Dingi yupo kimya tu anasoma mchezo nikamaliza kula nikawa naenda kulala kidume nikaitwa njoo hapa unaenda wapi nikamjibu kulala akasema toa godoro lako likunje, nikakunja godoro vizuri nikamaliza akasema liweke chumbani kwangu nikapeleka chumbani godoro haya nenda ulale. Bwana wee Kitanda cha chuma hakina kitu nikafika kidume nikalala kwenye vyuma kwa usimamizi wake hadi majira ya saa 8 hivi nagalagala kwenye vyuma, ngozi imeweka alama kama nimechapwa bakora aiseeee. Wale dada zangu wenyewe walifungwa juu ya kenchi usiku kucha hadi asubuhi, Asubuhi niliamka poa tu nikakanda mwili vizuri nikaendelea na majukumu ya utoto.

2.Kuna mdogo wangu alikatwa masikio.

3.Vikojozi walikuwa wanalala kwenye mfuko, wanaingizwa humo usiku kucha watatolewa asubuhi.

Hakuna kusema neno NITAKUPIGA hata kama ni kwa mdogo wako akisikia hilo neno ni kipigo Heavy kwa aliyesema "alikuwa anadai yeye ndiye mwenye uwezo wa kupiga kwenye ule mji".

Ukizira kula jiandae kula kwa lazima na chumvi ikizidishwa maradufu kwenye mboga chini ya usimamizi wake.

Kuchomwa kwa mvuke ilikuwa kawaida sana kwetu.

Ukipigwa haja kubwa isitoke shukuru Mungu kipigo cha siku hiyo.

Aliwahi kukunja mzazi mmoja ngumi hadi kwenda polisi (ila hiii sisemi).

Nilikuwa nafata maji usiku saa mbili kisimani ambapo ni zaidi ya km 2 pekee yangu nikiwa under 10 years.

Nipo safarini nikifika nitawaambia watu wa Tanga nipokeeni hapo stand. Nipo kwenye basi la Simba Mtoto natokea Isamembwe.
[emoji23] [emoji23] [emoji87] [emoji87] kwny kenchi mpk asubuhi[emoji15]
 
Awa wazee wetu yani wao kupiga mtoto ni sifa kubwa kwao tena utakuta wanakaa kwenye vijiwe vyao wanaadithiana kwamba wanajua kupiga .Haya mambo yakupigwa pigwa ovyo bila sababu yalinijenga kuwa na tabia ya uwoga,hasira na roho ya chuki (nashukuru Mungu nilijtambua nkazpinga izo roho) kwn mzee alkua anapenda kuogopeka kuliko kuheshimika.Mbali na kupgwa wazee wanakuaga na kauli mbaya sana juu yetu tukiwa wadogo utakuta mzee anakuambia yan ww ata ukisoma vp hutokuja fanikiwa maishani na stokuja kula ata shiling yako halafu baadae anakuja kukulia eti uyu ndio mwanangu mpendwa msomi.
Kabisa maneno mabaya,makali...ema vile tu tunatakiwa kusamehe la sivyo sijui kwakweli
 
Siku moja mimi na dogo tulirudi saa mbili na nusu hivi na hiyo ilikuwa 1999, akatuuliza kama tumeswali swala ya ishaa, tukamwambia ndio. akatuuliza kaswalisha nani na amesoma sura gani?? kudaadeki akatubana. aiseee tulikula kichapo mpaka leo sikisahau, alitufunga kamba za katani na kututandika nyaya za umeme ajabu, kipindi hicho tunaishi Pemba kwenye nyumba za serikali na ni ghorofani sasa, kutoka mbio tulishindwa halafu alivyokuwa mkaksi, alimfungia bi mother mlango kwa nje kwanza ili asije kuamua ugovi. Siisahau iile siku, but we a re who we are because of him otherwise tungekuwa ganja mtu sasa hiv. Akili yangu kipindi kile ilikuwa inaniambia dingi anatuchukia but now I understand he was/is the best dad ever in this world. Thank you papaaa
 
Back
Top Bottom