Kalpana
JF-Expert Member
- Jun 16, 2017
- 32,603
- 62,269
Inaonekana humu wengi wazee wetu hawapo nasi duniani. Kwa heshima zao R.I.P our lovely ones. Baba angu alikua anaogopewa mtaa mzima japo hakua na shida na mtu hata marafiki walikua hawaji kwetu. Sema baba alipanda hewani halafu black wa ukweli jicho jekundu kwa sbb ya kilaji. So watu walijjua mtiti wake hatari kumbe walaa hata fimbo hajawahi kutuchapa. Ila sitasahau nilifeli hesabu nikiwa drs la tatu alinipa kofi moja niliona nyota nyota na kukaa chini bila kutoa sauti yoyote alijua kanimaliza akaondoka kimya kimya akarudi night akiwa njwiiii. Mie shavu limevimba mpk vidole vyake vimetokea toka siku ile nilikua kipenzi chake.