Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Inaonekana humu wengi wazee wetu hawapo nasi duniani. Kwa heshima zao R.I.P our lovely ones. Baba angu alikua anaogopewa mtaa mzima japo hakua na shida na mtu hata marafiki walikua hawaji kwetu. Sema baba alipanda hewani halafu black wa ukweli jicho jekundu kwa sbb ya kilaji. So watu walijjua mtiti wake hatari kumbe walaa hata fimbo hajawahi kutuchapa. Ila sitasahau nilifeli hesabu nikiwa drs la tatu alinipa kofi moja niliona nyota nyota na kukaa chini bila kutoa sauti yoyote alijua kanimaliza akaondoka kimya kimya akarudi night akiwa njwiiii. Mie shavu limevimba mpk vidole vyake vimetokea toka siku ile nilikua kipenzi chake.
 
Kumbe we we wa kishua..mlikuwa na simu ya mezani wakatio huo,sisi kwetu tulikuwa na radio moja ya mkulima.
Mwaka 99, enzi hizo simu ya mezani, alikuja mgeni akaomba simu apige hapo simu inakaa chumbani, nikamwambia dingi mgeni anaomba simu, dingi akaguna tu nikajua kakubali nikatoa simu mgeni kaongea alivoondoka mweh!!!!
Nlichezea kichapo heavy yani mvua ya stiki..... Apumzike kwa amani mdingi
 
Kibishi tu sasa hivi nikimtazama huwa naona kama Bro wangu hana noma, Mara ya Mwisho ananipiga ilikuwa niko Darasa la nne, alikuwa yupo safarini ila asubuhi aliniita chumbani akanipa majukumu ya kufanya, Nimeamka tu nikaenda kusakata kabumbu nikijidai Maradona hadi saa 12 jioni ndipo Maradona anarudi nyumbani akamkuta baba yake kafika hakuna kazi yeyote iliyotendeka.

Kipigo cha Kufa Mbwa kikamhusu Maradona, Kilichoniokoa niliona nikiendelea kulia na kupiga kelele nitakufa kwa ngumi na makofi ya Baba yake Maradona basi Nikajidai nimezima anapiga sitikisiki wala kugeuka kapiga kama dakika 1 kashituka, akajua Maradona Kafariki, alikuwa na buti moja chini limeandikwa Base akanikanyaga nalo duh maumivu yale yalimtoa chini Maradona akasepa mwendo wa Kimondo kuelekea kusikojulikana.

Tangu Siku hiyo hakunipiga tena.
Pamoja na kujifanya umezimia bado akakumalizia na buti ha ha ha
 
dingi yangu alikuwa mkoloni sana, kipindi nakua nimechezea sana mikanda ila nashukuru ilinitoa ujinga na kunipa ujasiri kiasi kwamba mpaka leo sitetereki, dah r.i.p Dady
 
Leo ni miaka 57 imepita dingi kafariki kaniacha Nina miaka saba tu sasa shuruba na mateso niliyoyapata kwa walezi wangu siwezi kusimulia huwa nalia nikikumbuka binadamu wabaya sana ni wazuri tukiwa tumelala kwenye makaburi tu
Duuh walikutesaa sanaa mzee mpaka useme kauli nzito hivyo..!?? umeshindwaa hata kusamehee
 
Mi mshua wangu hakua mkatili kiivyo sema ile akikukamata bora ukimbie tu pia anaweza kukuungia sasa mwanae mim dish liliyumba kitambo nikawa namkimbiza mitaa yenye watu wengi kwa heshima aliyokua nayo basi alikua anavunga tu Mimi kichapo nmechezea kutoka kwa mama daaah ilifika stage najiuliza huyu n mama angu kweli daaah
 
Back
Top Bottom