LAMBOFGOD
JF-Expert Member
- Aug 12, 2016
- 1,561
- 1,319
Kibishi tu sasa hivi nikimtazama huwa naona kama Bro wangu hana noma, Mara ya Mwisho ananipiga ilikuwa niko Darasa la nne, alikuwa yupo safarini ila asubuhi aliniita chumbani akanipa majukumu ya kufanya, Nimeamka tu nikaenda kusakata kabumbu nikijidai Maradona hadi saa 12 jioni ndipo Maradona anarudi nyumbani akamkuta baba yake kafika hakuna kazi yeyote iliyotendeka.
Kipigo cha Kufa Mbwa kikamhusu Maradona, Kilichoniokoa niliona nikiendelea kulia na kupiga kelele nitakufa kwa ngumi na makofi ya Baba yake Maradona basi Nikajidai nimezima anapiga sitikisiki wala kugeuka kapiga kama dakika 1 kashituka, akajua Maradona Kafariki, alikuwa na buti moja chini limeandikwa Base akanikanyaga nalo duh maumivu yale yalimtoa chini Maradona akasepa mwendo wa Kimondo kuelekea kusikojulikana.
Tangu Siku hiyo hakunipiga tena.
mkuu wa
Raphael wa Ureno naomba kumtunuku mzee wako vyeo vyake