KERO Wenye magari ya kusomba madini Manispaa ya Iringa tunalipishwa ushuru mara 2

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi ni Wamiliki wa Tipa za kusomba madini ujenzi Manispaa ya Iringa tuna kero yetu, kwa kawaida Ofisi ya Madini Mkoa huchukua shilingi 8,000 kwa kila ‘trip’ moja.

Wakati huohuo Ofisi ya Mkurugenzi huchukua shilingi 300,000 kwa mwaka wakisema ni ushuru pia.

Aidha, Ofisi ya Mkurugenzi huchukua ushuru huo wakiwa hawana sheria ndogo iliyotungwa na madiwani kukusanya mapato hayo, hivyo ofisi hiyo inakusanya kinyume cha Sheria za nchi.

Vilevile, Mashine za EFD zimekabidhiwa kwa wamiliki wa magari ya kusomba madini ujenzi na wana viwanda vya kufyatua tofali, je watakata ushuru kwa trip zote walizosomba? Sio rahisi!!

Mwisho wake, Asilimia 80 ya EFD Mashine ni za Mfanyakazi wa ofisi ya madini ila zimezisajili kwa majina ya watu wengine ili kukwepa utambuzi asijulikane.

Kero hii ni ya muda mrefu, Mamlaka za juu zitambue tunachokipitia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…