Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 505
- 872
WENYE MAJUKUMU YA KAZI BIASHARA NA FAMILIA JIUNGENI CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA
Kama wewe ni mtu ambaye una majukumu ya kazi, biashara au ya kifamilia na unapenda kujiendeleza kielimu, njoo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ndipo mahali pake. Chuo hiki cha umma kinaendeleza watumishi wa umma na binafsi kuanzia ngazi za Certificates, Diploma, Shahada, Shahada za Umahiri na Uzamivu.
Chuo kina mifumo wezeshi ya kukufanya usome ukiwa huko huko ulipo. Mifumo hiyo ni MOODLE Platform, mihadhara mbashara kwa ZOOM, mafunzo ya ana kwa ana kwa vipindi maalumu, masomo ya jioni (evening programs), masomo ya Executive, mafunzo ya vitendo, maktaba mtandao, na What's App Kimbwetta. Kupitia mifumo hii utasoma vizuri sana na utapata maarifa na ujuzi wa kutosha katika eneo lako la ubobezi.
Dirisha la kufanya maombi lipo wazi kwa ngazi zote. Tuma maombi yako kupitia www.out.ac.tz popote pale ulipo. Chuo kina matawi kila mkoa na vituo vya uratibu Unguja, Pemba, Kahama na Tunduru. Karibu sana ujiendeleze kupitia Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Wasio na majukumu pia wanaruhusiwa kujiunga na wakati wanaendelea na masomo wataweza kuanza kufanya shughuli zao kama kilimo, ufugaji, biashara katika kujiajiri au kuajiriwa.
Na.
Dkt. Mohamed Maguo
Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania