Wenye mamlaka tuwaokoe hawa watoto kabla ya kutokea maafa

Hapo hakuna njia wao ndio wanalazimishaa iwe njia kufupisha safari
 
Hii ni hatari sana kwa watoto wetu, hasa kipindi hiki cha mvua.

Hapa ni maeneo ya Banana - Ukonga.

Chukueni hatua mapema.
View attachment 3286118
Waambie wazazi wachukuwe hatua kwa kudai uchaguzi huru na mfumo mzuri wa uongozi wenye kuwajibika. Kila siku mnaimba ''mamlaka chukuweni hatua'', tangu lini umeona hizo mamlaka zikijali. Wabongo bwana. Kila kitu mamlaka, mamlaka, wakati nyie ndiye wenye mamlaka.
 
Kwanini hawapiti juu ya hilo daraja?
Kwanini nyie wakubwa hamuwazuii watoto wasipite mnachukua picha tu?
Hili pia ni tatizo kubwa mkuu, hii video sijaichukua mimi lakini pia nimeshangaa kuona watu wazima wanashindwa kuwazuia watoto kufanya wanachokifanya.
 
Hao watoto huwezi kusema wanayatafuta matatizo wenyewe.
Kwa akili yao hawaoni hatari wanahitaji kusaidiwa kutambua hatari kwa kuwazuia na kuwapeleka ilipo njia salama.
Sio watoto hao wakubwa wanao wapitisha iyo njia na hao walio waftwa shule hawaoni ilo kama ni tatizo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…