Wenye miaka zaidi ya 30, kitu gani unajutia kufanya/kutofanya kabla ya kufikisha miaka 30?

Wenye miaka zaidi ya 30, kitu gani unajutia kufanya/kutofanya kabla ya kufikisha miaka 30?

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,319
Reaction score
3,097
Mimi najutia nilifanya investment badala ya kufanya savings.

Mwisho wa siku biashara zimekufa sina savings hata moja.

Najutia kutonunua viwanja pesa yote nikaweka kwenye miradi ambayo yote imekufa.

Ongezea tujifunze
 
Y
Ni kuchelewa kupata mtoto ..

Nimepata mwanangu wa kwanza nikiwa na 30 kamili

Nilitamani kuwa na mtoto tuliepishana hata miaka 25

Lakini sijui nilichelewa wapi?

Yaani sinui kwakweli nilikuwa nafanya nini huo umri
Shukuru hata kwa huyo uliyempata wengine tunaelekea 40+ na bado hatuja jaariwa kupata mtoto
 
Nafurahia zaidi nimekwepa mambo yanayowakumba vijana wenye 20s
  • Nimelala kituo cha polisi ila nashukuru siijui jela (vijana wengi kwenye 20s huishia jela kwa tamaa, makundi, vurugu za kutaka kuonekana miamba, n.k.
  • nilipenda ngono kwenye 20s umri wenye matamanio na nguvu zaidi ila nashukuru nilijitahidi kujilinda (vijana wenye 20s huishia kuungua na uti, magono, ukimwi, n.k. kwa kusukumwa zaidi na miili kuzidi akili)
  • nimewahi kujaribu bangi nikiwa natamani kwa muda mrefu kuyajua yaliyomo ila nashukuru niliacha (bangi ya Tz ni 50/50 waweza kuwehuka, huogi, hujijali, n.k.)
  • sina mtoto wa nje ya ndoa
  • n.k.

Nachojutia zaidi nimewahi kuwe kwenye mahusiano ya kumpenda mtu ambae hanithamini (kufosi), kuwa na marafiki wa ovyo, kupoteza muda mwingi mitandaoni bila faida, n.k.

Wengi sana wanaharibu maisha wakiwa kwenye 20s sababu ya ugeni wa mapenzi, ugeni wa uhuru, kutaka vitu wasivyoweza kuvimudu (tamaa) , n.k.
 
Back
Top Bottom