Wenye mtaji Njoo tuwekeze huku kwenye migodi ya dhahabu

Ninavyowajuwa vizuri Wabongo mchongo wa kweli wa kupiga pesa hakwambii ng'o ila sehemu ya kwenda kuangamiza pesa yako ndio unatangaziwa fursa.

Wazungu wanajuwa sehemu zote zenye utajiri, ingekuwa rahisi hivyo wazungu wangeshachukuwa vitalu na kuingia mitambo ya kisasa.

Hizi ni hadithi tu.
 
Wakuu kama unajiona una mtaji kuanzia m2 hivi njoo nikusaidie ujipatie eneo la mgodi ujiingizie m3 hadi nne kwa siku hiyo ni baada ya kuwekeza ndani ya mwezi mmoja

Kikubwa ambacho nitakusaidia kukuunganisha na ml mwenye eneo atakupa eneo kwa makubaliano haya 3% ya faida utayopata itaenda kwa mwenye eneo nikimaanisha kama mgodi wako utatoa mifuko kumi kwa siku, mfano yenye ghamu 30 mwenye eneo yake mifano mitatu ww utabaki na 7

Mimi nitakusaidia kukutafutia vijana wewe utasimama kama mzamini

Kama upo tayari njoo utengeze pesa sio unamtaji alafu unakaa nao tu hujui cha kufanyia

Watu ambao nitawasaidia ni wale wenye mitaji na wenye lengo la kuwekeza kwenye dhahabu

Kama hujanielewa uliza swali nitakujibu ila kuna vingine siwezi kuviweka hapa

Location: Msumbiji
Hakuna ujanja ujanja wala utapeli lengo vijana wa kitanzania tupige hatua

Na kama unajiona huna mtaji tafuta vijana wenzako watatu hadi wa nne ambao mnajua kupiga kazi yaani kazi sio mabishoo njooni huku ila kikubwa mjue kujizamini ishu kubwa huku ni misosi,maigreshen, yaani kodi ya kichwa kila jmos 5000 kwa kila mchimbaji ukiweza hayo wee njoo upige pesa mapori kibao yanataka watu kulala maskini kuamka na tumilion kazaa kawaida kuhusu kulala usiwaze mwanaume hashangai pakulala gest zipo matulubai ya kujengea kambi yanauzwa
Kikubwa jizile sio unakuja huku anawaza hom

Kwa wale wapenda starehe huku ndio kuzimu utawakanyaga mpaka urud bila pesa kwenu kikubwa ujue kuziotea
Si unakuja huku na gundu lako utasota mpaka unione mbaya osha nyota alafu njoo

Kama unajiona huna nia wala lengo usiwakatishe tamaa wenzako kwa swaga za utapeli,mana ukizingua nitakuzingu sipo hapa kwaajili ya kukupeti pet, sifa ya mtoto wa kiume ni kukaza mafanikio sio kutuma buku ushinde m3 mtoto wa kiume kazaaaa

Karibu
Mliopo msumbiji, deal hilo hapo japo halitofautiani na betting
 
Ni mpakani na ukanda wa ziwa nyasa ila hauvuki ziwa kuna barabara inaingia hadi huko huko kwa kupitia wilaya ya mbinga hata watu wa upande huo mahitaji yao yote wanachukulia mbinga/ruvuma , maana machimbo yalipo hadi ufike Msumbiji yenyewe ufanye kaz kidogo coz hakuna usafiri wa kwenda huko kutokea hapo machimbo na hakuna barabara ya maana ya kusema itapita gari kubwa ni mwendo wa milima
Huku ndio Kuna mlima unaitwa "KAZA PUMBU" au sio mkuu
 
Kama una hela yako ya mboga,usieke kwenye dhahabu.UTAKUJA KUNISHUKURU BAADAYE.
Wakati nikiwa mdogo jirani yetu alianza biashara mdogo mdogo anaongeza gari mojamoja, mpaka nafika form 2 alikuwa na gari 15. 12 za kazi 3 za kutembelea. Kuna mjanja akamtonya kuna biashara ya dhahabu msumbiji. Akauza sehemu kubwa ya biashara zake. Magari ndio aliuza yote yakabaki mawili. Akaingia kwenye biashara ya madini huko msumbiji. Alifilisika kabisa mpaka akawa hataki kurudi nyumbani. Baadae ile gari aliyokuwa anaitumia kule ikawa inabeba abiria dereva anamletea malengo jioni. Mpaka nayo matairi yakaisha. Vijana waliokuwa wafanyakazi wake ambao walikimbilia huko machimboni baada ya tajiri yao kufunga biashara, ndio wakawa wanampa buku 5 za kula kila siku. Akawa anapiga pombe za kienyeji hatari. Baadae familia yake walienda kumbeba na kumrudisha nyumbani. Akakaa miezi kadhaa akarest in peace. Kutoka kumiliki magari 15 aliyoyatafuta kwa miaka 14 hivi, akawa maskini ndani ya miezi kadhaa tu. Madini sitaki kuyasikia kabisa. Kwanza kuna kutoa sana kafara, kwa hiyo kama huamini kwenye uganga usiende.
 
Jamaaaa nipe location ili niweze fika au nitumie nambaako ya sm ilinukupugie unielekeze njia niweze Kuja..umesema ni mpakani mwa ziwa nyasa kwa kupitia mbinga hujaainisha ukifika mbinga unapenda usafiri wakwenda eneo gani
 
Wakati nikiwa mdogo jirani yetu alianza biashara mdogo mdogo anaongeza gari mojamoja, mpaka nafika form 2 alikuwa na gari 15. 12 za kazi 3 za kutembelea. Kuna mjanja akamtonya kuna biashara ya dhahabu msumbiji. Akauza sehemu kubwa ya biashara zake. Magari ndio aliuza yote yakabaki mawili. Akaingia kwenye biashara ya madini huko msumbiji. Alifilisika kabisa mpaka akawa hataki kurudi nyumbani. Baadae ile gari aliyokuwa anaitumia kule ikawa inabeba abiria dereva anamletea malengo jioni. Mpaka nayo matairi yakaisha. Vijana waliokuwa wafanyakazi wake ambao walikimbilia huko machimboni baada ya tajiri yao kufunga biashara, ndio wakawa wanampa buku 5 za kula kila siku. Akawa anapiga pombe za kienyeji hatari. Baadae familia yake walienda kumbeba na kumrudisha nyumbani. Akakaa miezi kadhaa akarest in peace. Kutoka kumiliki magari 15 aliyoyatafuta kwa miaka 14 hivi, akawa maskini ndani ya miezi kadhaa tu. Madini sitaki kuyasikia kabisa. Kwanza kuna kutoa sana kafara, kwa hiyo kama huamini kwenye uganga usiende.
Ukiitwa kwenye fursa na masikini jua unaenda ibiwa
 
Kuna ambao walikuwa wauza uji mgodini ila kwa sasa ni matajiri wa kutupwa....biashara ya madini ina sehemu mbili...inaweza kukutoa mpaka kila mtu akashangaa na kutamani kuwekeza kwenye madini na inaweza kukufilisi mpaka ukawa chizi...nina mifano hai kabisa...
 
Ni mpakani na ukanda wa ziwa nyasa ila hauvuki ziwa kuna barabara inaingia hadi huko huko kwa kupitia wilaya ya mbinga hata watu wa upande huo mahitaji yao yote wanachukulia mbinga/ruvuma , maana machimbo yalipo hadi ufike Msumbiji yenyewe ufanye kaz kidogo coz hakuna usafiri wa kwenda huko kutokea hapo machimbo na hakuna barabara ya maana ya kusema itapita gari kubwa ni mwendo wa milima
Kaka nikifika mbinga nachukua usafari wa Kuja wapi ni full location mkuu
 
Back
Top Bottom