Wenye mtaji Njoo tuwekeze huku kwenye migodi ya dhahabu

Ninavyowajuwa vizuri Wabongo mchongo wa kweli wa kupiga pesa hakwambii ng'o ila sehemu ya kwenda kuangamiza pesa yako ndio unatangaziwa fursa.

Wazungu wanajuwa sehemu zote zenye utajiri, ingekuwa rahisi hivyo wazungu wangeshachukuwa vitalu na kuingia mitambo ya kisasa.

Hizi ni hadithi tu.
 
Mliopo msumbiji, deal hilo hapo japo halitofautiani na betting
 
Huku ndio Kuna mlima unaitwa "KAZA PUMBU" au sio mkuu
 
Kama una hela yako ya mboga,usieke kwenye dhahabu.UTAKUJA KUNISHUKURU BAADAYE.
Wakati nikiwa mdogo jirani yetu alianza biashara mdogo mdogo anaongeza gari mojamoja, mpaka nafika form 2 alikuwa na gari 15. 12 za kazi 3 za kutembelea. Kuna mjanja akamtonya kuna biashara ya dhahabu msumbiji. Akauza sehemu kubwa ya biashara zake. Magari ndio aliuza yote yakabaki mawili. Akaingia kwenye biashara ya madini huko msumbiji. Alifilisika kabisa mpaka akawa hataki kurudi nyumbani. Baadae ile gari aliyokuwa anaitumia kule ikawa inabeba abiria dereva anamletea malengo jioni. Mpaka nayo matairi yakaisha. Vijana waliokuwa wafanyakazi wake ambao walikimbilia huko machimboni baada ya tajiri yao kufunga biashara, ndio wakawa wanampa buku 5 za kula kila siku. Akawa anapiga pombe za kienyeji hatari. Baadae familia yake walienda kumbeba na kumrudisha nyumbani. Akakaa miezi kadhaa akarest in peace. Kutoka kumiliki magari 15 aliyoyatafuta kwa miaka 14 hivi, akawa maskini ndani ya miezi kadhaa tu. Madini sitaki kuyasikia kabisa. Kwanza kuna kutoa sana kafara, kwa hiyo kama huamini kwenye uganga usiende.
 
Jamaaaa nipe location ili niweze fika au nitumie nambaako ya sm ilinukupugie unielekeze njia niweze Kuja..umesema ni mpakani mwa ziwa nyasa kwa kupitia mbinga hujaainisha ukifika mbinga unapenda usafiri wakwenda eneo gani
 
Ukiitwa kwenye fursa na masikini jua unaenda ibiwa
 
Kuna ambao walikuwa wauza uji mgodini ila kwa sasa ni matajiri wa kutupwa....biashara ya madini ina sehemu mbili...inaweza kukutoa mpaka kila mtu akashangaa na kutamani kuwekeza kwenye madini na inaweza kukufilisi mpaka ukawa chizi...nina mifano hai kabisa...
 
Kaka nikifika mbinga nachukua usafari wa Kuja wapi ni full location mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…