Wenye Nissan Dualis nawatamani sana hamjui tu

kwene kupata moto hapo!! huwezi kwenda nayo masafa marefu.
Lets say mbeya hadi Arusha haifiki?
Swala sio kupata moto mkuu. Kama uko dar kwani hujazishuhudia hata mara moja unakuta tu imetoka tu hata mwenge kwenda posta hapo katikati magomeni ikashika moto.

Masala marefu inaenda tu vizuri na unaweza kwenda na kurudi nayo vizuri na ikawa Salama. Mimi nimesafiri nayo Dar to mbeya ilivyofika. Na nikarudi nayo siku nyingine Dar na nikarudi nayo mbeya na mioto yangu sio ya kitoto.

Cha ajabu kuna siku nimetoka nayo kyela kurudi mbeya,ni kama km 100 ikashika moto hapo katikati. Kyela to mbeya inaweza ikawa chalinze to posta dar. Hapo katikati ikashika moto.

Nilianza kusikia kama harufu kitu kinaungua,kufika sehemu moja brake zikapotea. Kila nikipamp hamna brake. Kufika mbele kama km 3 hivi harufu ikazidi,mwanzo nilijua ni harufu ya loli lilikuwa mbele yangu. Nikafanya kulipita. Harufu bado kali kitu kinaungua. Nikapack pembeni ile kufungua bonet daah moshi ulioibuka hapo. Wakatokea washikaji hapo piga piga maji na mchanga kumbe wanapiga sehemu ya engine kwa juu. Moto ulikuwa kwa chini pale karibia na pipe za mafuta ya brake. Jamaa mmoja akachungulia ndio akauona moto mdogo tu kwa pale. Na ile harufu ilikuwa ni yale mapamba kama mblanket hivi yale,kumbe yanasaidia sana yale.
Mwisho ilipona ila wakati wanapiga maji kwa wingi wakaisukuma rubber iko pembeni ya control box ya gear box. Yenyewe kwenye hizi gari iko mbele ya engine pale pembeni ya battery. Kwa hiyo baada ya pale kuna fundi akaiweka sawa nikafika mbeya vizuri tu. Sasa kuanzia hapo gear zikaanza kugoma kuingia. Kwa hiyo niligharamia control box tu na wakaweka sawa pale moto unapoanzia
 
Ok vizuri sana
 

kwaiyo ukaiuzaa
 
Waoooooo

Haya nami ngoja niweke dreams za Vitz
Mungu anipe
Amin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…