Wenye Nissan Dualis nawatamani sana hamjui tu

Wenye Nissan Dualis nawatamani sana hamjui tu

Hiyo inaongoza Kwa kuungua...utalia ukinunua halafu iungue unaiona
Mkuu, mbona tokea huu mwezi uanze sijasikia kama kuna Nissan ilmeungua? Suala la kuungua linaweza likawa ni ajali kama ajali zingine. Kama zingekuwa na tatizo sana, Serikali ingezipiga marufuku kuingizwa nchini. Maadam TBS imeziridhia, amini ya kuwa ni bidhaa bora.

Muhimu ni kuzingatia maelekezo ya mtengenezaji na wataalam wengine wa magari.
 
"Brother ukiona kitu umekitamani hasa ujue hiyo ni ishara tosha kuwa unaweza kukimiliki regardless mazingira yanayokuzunguka yalivyo"
.....ishi kwenye ndoto zako Kwa gharama yoyote.
Mimi gari yangu ya kwanza kuinunua na kujifunza ni Subaru legacy Bl sport na sijawahi jutia uamuzi wangu licha kukutana na washauri lukuki mara ooooooh!...inakula wesee.... Oooh...spare zake gharama....oooooh....zipo chini sana..ila Brother nadunda nayo kama kawaida.
"Maisha ni yako, ndoto ni zako ukizubaa tutakuteka uishi kwenye zetu"
Uko sahihi mkuu!
 
Jamani mie napenda Harria nyeusi tako la nyani balaa, nna 20 .wenye lililo ktk hali nzuri anicheki.
Ipo kwa Sossy hii..
20231024_164323.jpg
 
$AVING ~i
Nimeanza kukusanya hela saizi nina 3000/= nimeitia kwa kibubu
Afu tatu hadi sasa....
Nina wasiwasi hadi kuja kufikia bajeti ya kuvuta hii Ndinga 19-23Mil, Dualis inaweza kuwa imepotea sokoni, ukakutana na kitu kingine, anyway hapo mchawi pesa endelea kuzichanga huenda ukaja kutana na kali zaidi by then kwa saved amount!
 
Wabongo utaskia nissana sio gari sasa ni nini. Mmezoea kuhujumu magari hamuyapi service na mnayatumia vibaya sana. Alafu wengi wetu hatuma magari tunabaki kuskiliza stor za vijiweni tu. Magari kibao mazuri ila uoga wetu na umaskini unafanya tuyatafutie sababu
 
Leo nimeanza kujichanga ninunue Dualis nissan.

Siwezi sema kiasi gan naitamani hii gari ila mjue tu nikiiona akili yangu huwa inataka kuweuka.

Mimi sina gari,

Sijui kuendesha ( siyo 0 kabisa no)
Sikuwaga na interest za magari
Ila sasa kuna hii gari imetokea inaitwa ……

View attachment 2783004
View attachment 2783006

View attachment 2783007
Yaan kiasi kwamba niki Nikimuona mtu anaendesha hii gari naona ANAISHI KWENE ndoto yangu kabisa. Namtamani ningekua ndo mimi naimiliki[emoji848]
nipeni ushauri nisije nikajikuta nimeuza had kabanda kangu kisa kutafuta milion22 za hii gari[emoji3064]

$AVING ~i
Nimeanza kukusanya hela saizi nina 3000/= nimeitia kwa kibubu
Hakikisha tuu una moyo wa spare
 
Wabongo utaskia nissana sio gari sasa ni nini. Mmezoea kuhujumu magari hamuyapi service na mnayatumia vibaya sana. Alafu wengi wetu hatuma magari tunabaki kuskiliza stor za vijiweni tu. Magari kibao mazuri ila uoga wetu na umaskini unafanya tuyatafutie sababu

mkuu wewe una gari gan
 
kwene kupata moto hapo!! huwezi kwenda nayo masafa marefu.
Lets say mbeya hadi Arusha haifiki?
Wanakutisha tu. Matukio ya magari kuungua moto ni jambo la kawaida na hutokana na hitilafu za kiufundi na uzembe wa kitozishughulikia kwa wakati.

Humo barabarani huwa tunakutana na RAV4, klugger, Pajero etc zinaungua mbona hazipigwi vita.

Kuna watu wakiogopa au wakiwa na hofu ya jambo fulani wanataka kuambikiza wengine hiyo hofu.

Hizi gari zingekuwa ni tatizo then zingekuwa 10 tu hata Tanzania. Ila umeshakaa barabarani ukahesabu hizi gari zipo ngapi?

Hivi hata kama akili yako haiwezi chuja ukweli ni upi na uongo ni upi hadi macho yako yamefeli kuona na kujipa majibu, yaani la kuona na kushuhudia kwa macho liwe uongo la kuambiwa ndilo liwe ukweli? [emoji848]

Nenda tu hapo bandari kaulize wale wanaoingiza magari wakupe data, hii ni gari ya tatu kama sio ya pili kwa kuongoza kuagizwa. Zinaingia nyingi kupita maelezo.

So kama roho yako ipo kwenye kuinunua hiyo gari usiwaze wewe chukua. Izo technical issues utashughulika nazo bila shida maana zinajulikana.

All the best and good luck. Ukinunua utuletee hapa tuione.
 
Sasa insulator imewekwa pale kwaajili ya kuzuia joto kupenya ukiwa utaondoa si ndio balah zaidi ?
Shida ya wabongo, wanafanya modification ambazo zinakinzana na standards za kiwandani then wanalalamika gari mbovu. Sasa unatoa kitu ambacho kiwandani walikiweka kwasababu ili iweje?
 
Back
Top Bottom