Wenye nyumba mnataka mtumalize sasa. Hela ya Tahadhari Mwezi Mmoja ndio nini sasai?

Miezi sita ni mingi sana, sio fair. Kama ikibidi basi miezi mitatu tu inatosha.
 
Hii ipo mkuu. Sema kibongo bongo naona malandlord kuturudishia pesa ya security lazima iwe vita, lazima watutafutie sababu ili wabaki nayo
Aisee tunaumia sana mkuu. Bora vichakaekweli ila mtu anakuja anasema rangi?
 
Nakubali. Ila siku ya mwisho najua itakua vita. Nimepiga picha nyumba nzima nitaona siku ya kuhama.
 
Kuna wapangaji jau.. akitoka, nyumba, chumba ama frem haitamaniki, naunga mkono hilo, ila kwanini ikitokea hakuna uharibifu usirudishiwe hapa ndipo utata unakuja
Ni wazo zuri mchawi implementation. Vitu kama rangi, kutu kwenye mabomba, nk. Ila wale watata wanaopikia jiko la mkaa ndani au kupasua vioo nk sawa hela isirudishwe.
 
Ni wazo zuri mchawi implementation. Vitu kama rangi, kutu kwenye mabomba, nk. Ila wale watata wanaopikia jiko la mkaa ndani au kupasua vioo nk sawa hela isirudishwe.
Yes.. kuna uchakavu na uharibifu hivi vitu viwili vitenganishwe..
Kuna mmoja kwenye frem alikata gypsum board, sijui hata alikuwa anatafuta nini huko, ukuta ukuta una mashimo mashimo ya misumari kama chujio.
 
Hakuna namna, huo ndio utaratibu wa sasa, bahati ni kuwa hiyo system inaenea TZ yote na hasa Dar.

Weka hela ya tahadhari, likitokea jambo mnamalizana bila kusumbuana. Pamoja na ugumu wa maisha lwa wapangaji, kujenga sio mchezo.
 
Hizi hela wapangaji wenyewe hutoa kwa kujipendekeza wenyewe. Hela inayotakiwa kutoa ni kodi ya nyumba tu, toa hiyo hela haitakataliwa, hizi zingine ni wizi tu
 
Sisiemu njooni muwatetee wanachama wenu huku wanalalamika hovyo TU πŸ˜‚ hela hawana
 
Nakubali. Ila siku ya mwisho najua itakua vita. Nimepiga picha nyumba nzima nitaona siku ya kuhama.
siku ya kuhama unatakiwa mwezi mmoja kabla hujahama unampa taarifa huku na yeye akijipanga. nikianza ujenzi wa nyumba zakupangisha ndio formula hii nitatumia. 3 month bank statement na 1 month bond

kwamba kila mwisho wa mwezi nikiwa baa sitaki kusikia mzee unajua sijaenda kazini kwaiyo kodi nivumilie, hii story naimaliza kwa bank statement maana hata asipoenda kazini mshaaara unaingia, mwingine ni mchwa kaamia nyumba mpya baada yakuhama unasema hii nyumba niyamwaka 70 kumbe mteja yeye nikuvunja tuu kila kitu, story hii namaliza na 1 month bond
 
Huu ni upumbavu,
Kuchukua kodi ya miezi 6 halafu kudai na pesa ya tahadhari juu ni wizi mtupu, pesa ya tahadhari huwa inawekwa kama mtu analipa mwezi mmoja mmoja.
 
Sehemu nyingi duniani kodi huwa I alipewa kwa mwezi mmoja mmoja.
 
Dah labda Mbweni mkuu
 
Kumbe kamanda una mjengo kabisa πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…