Wenye pikipiki wateka mamia Nigeria

Ndugu Buhari amefeli labda sababu ni Uzee

Matatizo ya kiusalama kuanzia uhalifu na kukosekana amani yapo juu mno kuliko kipindi chochote

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Achana na propaganda za kitoto hizo na zilizopitwa na wakati ambazo si za waislamu.
Uislamu ndio daraja kubwa la maendeleo ya dunia kwa sasa na watafiti wote wa mwenendo wa elimu wamelithamini hilo.
Kabla ya kushuka Qur'an na kupewa utume Mtume Muhammad s.a.w kulikuwa na elimu na kwa sababu elimu ni maumbile ya Mwenyezi Mungu.Lakini mara baada ya kushuka Qur'an na baada ya kufariki Mtume s.a.w elimu katika dunia ilipata nguvu kubwa sana.Hii ilitokana na ufunuo uliomo katika Qur'an ambapo aya ya mwanzo ilihimiza kusoma na haikubaguwa elimu unazoita wewe za dunia na kwengine unakokujua.
Ndani ya Qur'an kumehimizwa kusafiri kutafuta elimu kwa kujionea maumbile ya Mwenyezi Mungu.Kuna aya nyingi zinazohusu kupeleleza mbingu na vyakula tunavyokula.Hadithi za Mtume s.aw zikahimiza watu kusafiri kutafuta elimu na kwamba kufanya hivyo kuna malipo makubwa ambayo yatamfanya mtu kuwa sababu ya kuingia peponi huko akhera.
Kwa kufuata mafunzo hayo waislamu wengi waliingiza kimatendo wakapeleleza na Mungu akawaongoza,wakasafiri na wakaona mengi waliyoyakushanya pamoja.Kutoka kaskazini ya Afrika wakaingia Ulaya wakati watu wa huko wako giza kabisa.Wakajenga vyuo vikubwa na utafiti mkubwa ukafanyika kwa juhudi hizo elimu zote zikafika mbali mpaka China na Urusi.Hivyo unapoona Urusi yote imejaa waislamu na kumbukumbu zake si kitu kilichozuka tu.
Kule Iraq kulijengwa maktaba kubwa ya watu kusoma na nzuri kabisa iliyodumu miaka mingi mpaka ilipovunjwa na wafuasi wa ukristo na kuchoma moto vitabu kwa mamilioni.Vichache vilivyopatikana ni maajabu matupu.Inaonekana wakristo wamechelewesha maendeleo ya kisayansi ya dunia.Kama si wao hizi ndege na intaneti inaonekana mababu zetu wengi wangeyakuta.
Nchini Mali pekee na huko huko Afrika maktaba iliyobaki Timbuktu kumepatikana maandishi ya waislamu kuhusiana na mahesabu ambayo watafiti wa kifaransa wamekiri wanafunzi wengi wa vyuo vikuu vya sasa hawawezi kuyakokotoa.
Mdomo wa kusema kuna watu wanapinga elimu ya dunia mumeupata wapi iwapo si propaganda za kitoto zinaganda kwenye alili za kitoto.
SOMA HAPA na uliza zaidi usiwe mvivu kwa kujifunza.
 
Sijasoma....ndefu sana
 
Buhari aliwahi kuwa rais kabla ya hapa. Tatizo la Nigeria ni connection, kilaza yeyote anaweza ongoza nchi mradi ulaji wa watu wachache unakuwepo. Unavyoona Wanaijeria ni matapeli duniani hata viongozi wake matapeli vilevile, jeshi lote wezi.

Buhari mzembe tu hana maajabu yoyote ni kama hayupo. Mageuzi gani kaleta, mbona Umar Yar Adua alikaa muda kidogo kabla hajafa ila heshima yake hadi leo ipo. Na alikuwa civilian, sasa huyu Buhari jenerali mzima hana mbinu mbadala za usamala.
 
Tatizo la kinachoitwa ugaidi na ujambazi na utapeli Nigeria kwa kweli si tatizo la kijeshi sana.Isipokuwa linahitaji kiongozi shupavu atakayetumia majeshi kumaliza ujinga na nchi ikarudia heshima yake kama mkubwa wa Afrika.
Ninaposema si tatizo la kijeshi ni kwa vile upande wa ugaidi na kinachoitwa Bokoharam ni ujinga na sifuri kabisa.Kiongozi akisema sitaki tena kusikia habari hizo linaisha na itabaki ujambazi na utapeli.Kumaliza habari za Bokoharam ni kila mtumiaji mitandao ya kijamii na mitandao ya kimataifa akiripoti habari hizo ashikwe atoe ufafanuzi hatua kwa hatua wapi alipopata taarifa zake.Watu wa Bbc na wenzao wakiripoti bila ushahidi wapigwe faini au wizara ya mawasiliano wafungie mashirika hayo kuripoti kutoka Nigeria.Wale wananchi wa ndani washtakiwe na wafungwe.Nchi nyingi zimewahi kufungia mashirika ya habari ya kimataifa wanapoona mashirika hayo yanaingilia maslahi yake na kuleta uchochezi katika ripoti zao.Sijawahi kusikia Nigeria ikichukua hatua hizo.
Upande wa utapeli na ujambazi wafanye kama China akishikwa mnigeria kafanya utapeli nje arudishwe ashtakiwe na adhabu iwe ni kifungo cha maisha au kifo.Hatua hizo ni za dharura kwani heshima na uchumi wa nchi na usalama unategemea maamuzi magumu kama hayo.Na nitoe tahadhari hatua zote hizo iwe kwa uadilifu na ushahidi isije ikapelekea kuadhibiwa wasiohusika mfano wenye ndevu au asili fulani au anachukiwa na fulani aliye madarakani.
 
Ina maana wamewateka na kuwapakia kwenye pkpik wanafunzi wote 800? How
Je wameingia na hizo pikpk huko msituni?
Hii Nigeria sasa haieleweki kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…