Achana na propaganda za kitoto hizo na zilizopitwa na wakati ambazo si za waislamu.
Uislamu ndio daraja kubwa la maendeleo ya dunia kwa sasa na watafiti wote wa mwenendo wa elimu wamelithamini hilo.
Kabla ya kushuka Qur'an na kupewa utume Mtume Muhammad s.a.w kulikuwa na elimu na kwa sababu elimu ni maumbile ya Mwenyezi Mungu.Lakini mara baada ya kushuka Qur'an na baada ya kufariki Mtume s.a.w elimu katika dunia ilipata nguvu kubwa sana.Hii ilitokana na ufunuo uliomo katika Qur'an ambapo aya ya mwanzo ilihimiza kusoma na haikubaguwa elimu unazoita wewe za dunia na kwengine unakokujua.
Ndani ya Qur'an kumehimizwa kusafiri kutafuta elimu kwa kujionea maumbile ya Mwenyezi Mungu.Kuna aya nyingi zinazohusu kupeleleza mbingu na vyakula tunavyokula.Hadithi za Mtume s.aw zikahimiza watu kusafiri kutafuta elimu na kwamba kufanya hivyo kuna malipo makubwa ambayo yatamfanya mtu kuwa sababu ya kuingia peponi huko akhera.
Kwa kufuata mafunzo hayo waislamu wengi waliingiza kimatendo wakapeleleza na Mungu akawaongoza,wakasafiri na wakaona mengi waliyoyakushanya pamoja.Kutoka kaskazini ya Afrika wakaingia Ulaya wakati watu wa huko wako giza kabisa.Wakajenga vyuo vikubwa na utafiti mkubwa ukafanyika kwa juhudi hizo elimu zote zikafika mbali mpaka China na Urusi.Hivyo unapoona Urusi yote imejaa waislamu na kumbukumbu zake si kitu kilichozuka tu.
Kule Iraq kulijengwa maktaba kubwa ya watu kusoma na nzuri kabisa iliyodumu miaka mingi mpaka ilipovunjwa na wafuasi wa ukristo na kuchoma moto vitabu kwa mamilioni.Vichache vilivyopatikana ni maajabu matupu.Inaonekana wakristo wamechelewesha maendeleo ya kisayansi ya dunia.Kama si wao hizi ndege na intaneti inaonekana mababu zetu wengi wangeyakuta.
Nchini Mali pekee na huko huko Afrika maktaba iliyobaki Timbuktu kumepatikana maandishi ya waislamu kuhusiana na mahesabu ambayo watafiti wa kifaransa wamekiri wanafunzi wengi wa vyuo vikuu vya sasa hawawezi kuyakokotoa.
Mdomo wa kusema kuna watu wanapinga elimu ya dunia mumeupata wapi iwapo si propaganda za kitoto zinaganda kwenye alili za kitoto.
SOMA HAPA na uliza zaidi usiwe mvivu kwa kujifunza.