Wenye 'sheli' waiba mafuta ya wateja

Wenye 'sheli' waiba mafuta ya wateja

Invisible

JF Admin
Joined
Feb 26, 2006
Posts
16,286
Reaction score
8,380
Imeandikwa na Halima Mlacha;
Tarehe: 15th December 2009
HabariLeo

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imebaini kuwa, baadhi ya pampu katika vituo vya mafuta zinato mafuta pungufu kuliko kiasi kilichokusudiwa.

Ewura imefunga pampu 15 , Dar es Salaam, baada ya kubaini kuwa wahusika 'wamezichezea' ili zitoe mafuta pungufu.

Mamlaka hiyo kupitia kitengo cha Wakala wa Vipimo imefanya ukaguzi wa kushtukiza katika vituo vya mafuta kuanzia Ubungo hadi Chalinze mkoani Pwani na kubaini kuwa baadhi ya vituo hivyo vimekuwa vikiwaibia wateja.

“Tumeanza ukaguzi huu jana (juzi) na ni wa kushtukiza na tumebaini kuwa kuna udanganyifu mkubwa unaofanyika katika vituo hivi hali ambayo inatupasa tuchukue hatua kudhibiti udanganyifu huu,” amesema Mkuu wa Operesheni katika eneo la Ubungo, Wilbard Kimaro.

Kati ya pampu 15 zilizofungwa, 13 ni za kituo cha mafuta katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo (UBT).

Kwa mujibu wa Kimaro, pampu nyingine zimefungwa katika kituo cha BP kilichopo Kimara Suka baada ya wakaguzi kuwakuta mafundi wakizitengeneza na EWURA hawakuwa na taarifa.

“Hata hivyo tumeamua kuwa tutakuwa tunafanya ukaguzi huu wa kushtukiza kwa kuwa vituo vingi vimekuwa vikichezea pampu hizi baada ya wakaguzi kupita na mihuri kuwekwa” amesema Kimaro.
 
Serikali imekua ikicheka na hawa, wamekua wakinufaika sana na michezo hii, hebu kumbuka wale waliokamatwa wakichanganya mafuta ya diesel na mafuta ya taa walifanywa nini, unawatoza milion 5, aah upuuzi. haiwaumizi kabisa, kesho wanarudia uharifu wao.

Sasa huo mchezo wakuibia wateja kwenye Petrol station ni jambo sugu nnchi nzima , hawaogopi kwasababu faini zao ni mchekea,

Ningeshauri jambo moja la msingi, kama wakikamatwa wanafanya fraud hizo, kwanza meneja wa kituo anaenda jela, fundi mkuu wa kituo jela, unamaliza na mmiliki. Kisha unafunga kituo na shughuli zao hapa nchini....inahitaji maamuzi magumu sana, kula jongoo yataka moyo.
 
Kuna kampuni inaitwa Shell ambayo jina lake limerithiwa na kufanywa ndilo jina la kila kampuni yenye kituo cha mafuta.
 
Wanawakamata, wanahongwa, wanawaachilia!...Kwani ni nani aliyefungwa kwa makosa ya aina hiyo...Hawa wakaguzi wanafanya mradi kwenye ukaguzi huu!..Kuna vituo kama vi3 hapa Arusha ambavyo kwa jinsi wanavyoiba, inabidi wanunuzi waende na galonni, maana ukiwekewa kwenye gari moja kwa moja jua utapata 3/5 ya lita, na hakuna anayewagusa!
 
Haya ndio madhara ya ufisadi, nchi inaendeshwa kifisadi, biashara zinaendeshwa kifisadi wananchi na serikali yao wanaishi kifisadi, wanawaza kifisadi, wanakula kifisadi. Kuiba umeme, maji, sasa mafuta..........etc. ili mradi ubabaishaji tu

We need to clean this house otherwise mambo yatazidi kuharibika.
 
Broda..are you serious with this thread?
There is a company with the name Royal Dutch Shell, pulled out of Tanzania in late 80's or somewhere erlier 90's and came back end of 90's to operate in the mining as fuel supplier. Gapco, BP, GBP etc vituo vyao sio shell...ni filling station za hizo specific companies. Shell jina lao linatukuzwa tu wakati wao hawana hata kituo kimoja.
 
Ndio maana heading ikaandikwa wenye 'sheli' kwa lengo tu la kuweka msisitizo kwani ndio neno tunalolitumia zaidi Tanzania likiwa na maana ya kituo cha kuwekea mafuta(filling station)
 
Haya ndio madhara ya ufisadi, nchi inaendeshwa kifisadi, biashara zinaendeshwa kifisadi wananchi na serikali yao wanaishi kifisadi, wanawaza kifisadi, wanakula kifisadi. Kuiba umeme, maji, sasa mafuta..........etc. ili mradi ubabaishaji tu

We need to clean this house otherwise mambo yatazidi kuharibika.
Bila kufanya hivyo tusahau maendeleo.Inabidi kuwa na jitihada za makusudi ambazo zifanywena watanzania wote ambao ndio wahusika ili tuirudishe nchi yetu kwenye mstari.Tukiharibikiwa itakuwa tumeharibikiwa wote bila kujari nani ni nani.
Kwa mfano Hitler alipoanzisha vita ya pili ya dunia ni wajerumani wote waliopata shida mambo yalipowageuka bila kujari walikuwa wanamsupport au la. Taratibu tunaelekea kwenye shimo na kama mwendo wenyewe ndio huu ipo siku tutafika deepest of the deep.
 
Ndio maana heading ikaandikwa wenye 'sheli' kwa lengo tu la kuweka msisitizo kwani ndio neno tunalolitumia zaidi Tanzania likiwa na maana ya kituo cha kuwekea mafuta(filling station)
Ok mkubwa tuko pamoja. nimekuelewa
 
Shell jina lao linatukuzwa tu wakati wao hawana hata kituo kimoja.

Hahahahaha bila shaka wewe umeondoka long time Bongo land, Shell ni kwa kiswahili Shelli hivi vituo vya kujazia mafuta kiwe BP, Oryx, Gapco, Lake Oil, Oil com vyote tunaviita Shelli kwa kiswahili mkuu.
 
Imeandikwa na Halima Mlacha;

Kwa mujibu wa Kimaro, pampu nyingine zimefungwa katika kituo cha BP kilichopo Kimara Suka baada ya wakaguzi kuwakuta mafundi wakizitengeneza na EWURA hawakuwa na taarifa.

Hivi kina BP kimara Suca??????? acheni kuchafua biashara za watu
 
Haya ndio madhara ya ufisadi, nchi inaendeshwa kifisadi, biashara zinaendeshwa kifisadi wananchi na serikali yao wanaishi kifisadi, wanawaza kifisadi, wanakula kifisadi. Kuiba umeme, maji, sasa mafuta..........etc. ili mradi ubabaishaji tu

We need to clean this house otherwise mambo yatazidi kuharibika.
HAKUNA wakumfunga paka kengele, vituo vyote vinamilikiwa na mapapa wa ufisadi ....hebu kumbuka vituo vya TIOT vilikua vinauza mafuta bei rahisi kuliko vituo vyote hapa nnchini, baada ya kamatakamata ya vituo vyenye kuchanganya Dizeli na mafuta ya taa, mara ghafla kimekua kituo chenye mafuta aghali zaidi TanZANIA,
 
Imeandikwa na Halima Mlacha;
Tarehe: 15th December 2009
HabariLeo

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imebaini kuwa, baadhi ya pampu katika vituo vya mafuta zinato mafuta pungufu kuliko kiasi kilichokusudiwa.

Ewura imefunga pampu 15 , Dar es Salaam, baada ya kubaini kuwa wahusika 'wamezichezea' ili zitoe mafuta pungufu.

Mamlaka hiyo kupitia kitengo cha Wakala wa Vipimo imefanya ukaguzi wa kushtukiza katika vituo vya mafuta kuanzia Ubungo hadi Chalinze mkoani Pwani na kubaini kuwa baadhi ya vituo hivyo vimekuwa vikiwaibia wateja.

“Tumeanza ukaguzi huu jana (juzi) na ni wa kushtukiza na tumebaini kuwa kuna udanganyifu mkubwa unaofanyika katika vituo hivi hali ambayo inatupasa tuchukue hatua kudhibiti udanganyifu huu,” amesema Mkuu wa Operesheni katika eneo la Ubungo, Wilbard Kimaro.

Kati ya pampu 15 zilizofungwa, 13 ni za kituo cha mafuta katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo (UBT).

Kwa mujibu wa Kimaro, pampu nyingine zimefungwa katika kituo cha BP kilichopo Kimara Suka baada ya wakaguzi kuwakuta mafundi wakizitengeneza na EWURA hawakuwa na taarifa.

“Hata hivyo tumeamua kuwa tutakuwa tunafanya ukaguzi huu wa kushtukiza kwa kuwa vituo vingi vimekuwa vikichezea pampu hizi baada ya wakaguzi kupita na mihuri kuwekwa” amesema Kimaro.
hii khabbari imeniskitisha sana hii. nitahakikisha waziri husika anajiuzulu. fuatilieni sana taarifa za khabbari. senksi sana mleta mada kwa kufichua huu uzembe dume.
 
nijuacho mimi ni kua zaidi ya asilimia 60 ya wafanyabiashara wa mafuta wanahusika na magendo katika mambo yote yanayohusu biashara hiyo Tangu vibali,uagizaji,ulipaji ushuru/kodi na leseni zingine hadi mafuta yanapouzwa, ni wizi-wizi mtupu.
 
Mwenye nacho ndiye anayemiliki serikali; hii dhambi ilizaliwa kule Marekani ...mambo ya soko holela na midubwasha kede-kede. I'm beginning to dislike America so much!
 
Kuna kampuni inaitwa Shell ambayo jina lake limerithiwa na kufanywa ndilo jina la kila kampuni yenye kituo cha mafuta.

SHELL ndiyo ilikuwa kampuni ya mwanzo mwanzo kabisa kusambaa hapa nchini nafikiri kabla ya BP na nyinginezo hivyo waswahili walitohoa neno la SHELL na kufanya kama ndiyo kituo cha mafuta
 
Back
Top Bottom