Invisible
JF Admin
- Feb 26, 2006
- 16,286
- 8,380
Imeandikwa na Halima Mlacha;
Tarehe: 15th December 2009
HabariLeo
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imebaini kuwa, baadhi ya pampu katika vituo vya mafuta zinato mafuta pungufu kuliko kiasi kilichokusudiwa.
Ewura imefunga pampu 15 , Dar es Salaam, baada ya kubaini kuwa wahusika 'wamezichezea' ili zitoe mafuta pungufu.
Mamlaka hiyo kupitia kitengo cha Wakala wa Vipimo imefanya ukaguzi wa kushtukiza katika vituo vya mafuta kuanzia Ubungo hadi Chalinze mkoani Pwani na kubaini kuwa baadhi ya vituo hivyo vimekuwa vikiwaibia wateja.
Tumeanza ukaguzi huu jana (juzi) na ni wa kushtukiza na tumebaini kuwa kuna udanganyifu mkubwa unaofanyika katika vituo hivi hali ambayo inatupasa tuchukue hatua kudhibiti udanganyifu huu, amesema Mkuu wa Operesheni katika eneo la Ubungo, Wilbard Kimaro.
Kati ya pampu 15 zilizofungwa, 13 ni za kituo cha mafuta katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo (UBT).
Kwa mujibu wa Kimaro, pampu nyingine zimefungwa katika kituo cha BP kilichopo Kimara Suka baada ya wakaguzi kuwakuta mafundi wakizitengeneza na EWURA hawakuwa na taarifa.
Hata hivyo tumeamua kuwa tutakuwa tunafanya ukaguzi huu wa kushtukiza kwa kuwa vituo vingi vimekuwa vikichezea pampu hizi baada ya wakaguzi kupita na mihuri kuwekwa amesema Kimaro.