Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,753
- 10,747
Habari wanajanvi, napenda kutumia fursa hii kuwasalimu, Moja kwa Moja niende kwenye Mada nimefungua uzi huu ili tupeane uzoefu wale ambao tunapbana na tatizo hili.
Mimi ni muhanga wa tatizo hili shinikizo la juu la damu - Hypertension kwa zaidi ya mwaka sasa.
Tatizo langu lilianza hivi, siku moja nikiwa kaenye shughuli zangu ghafla kichwa kiliniuma sana, nikapaatankizunguzumgunkikali sana nipata pamoja na macho kuona kama marue rue hivi, nilienda hospital kupata matibabu baada ya vipimo mbalimbali nilikutwa shinikizo la damu likiwa juu ilikuwa ni 168/110 pamoja na Colesterol ilikuwa juu sana.
Dr alishauri nianze dawa za pressure pamoja na Colesterol , binasfi sikuhafiki sana ushauri wa Dr, Pamoja ya kuwa nilichukuwa dawa nilimeza siku moja tu,sikuwahi kumeza tena baada ya kushauriana na Dr ambaye awali alishawahi nishauri nianze kudhibiti pressure yangu, mpaka leo sijatumia dawa niliamua kuanza diet na mazoezi.
Nilianza safari mpya ya kubadilisha mfumo wangu wa maisha hii sio kazi rahisi hasa ukizingatia inahitaji kujibana na kubadilisha mind set kwenye mambo uliyazoea, mimi ni mtumiaji sana wa pombe nakunywa bia sana, kwa wale wanywaji wanajua pombe inavyoshabiana na ulaji wa Nyama choma, Kitimoto na supu kwa wingi.
Maisha haya yalichangia sana kuwa na uzito uliopitilza kwani uzito ulifika kg 86 wakati urefu wangu ni 1.7m, hivyo uwiano na uzito na urefu ikawa nipo kwenye obesity line.
Baada ya kuanza hii safari mpya ya maisha miezi 2 iyopita maendeleo kidogo naona sio mbaya sana ingawa bado nahitaji kuendelea kupambana, nimepunguza uzito kutoka kg 86 - 82, na BP imeshuka mpaka 141/98 na wakati mwingine inashuka mpaka 133/89.
Nimeacha matumizi ya Carbs kwa sehemu kubwa, nimepunguza pombe nakunywa kwa wiki mara 1 au 2, nakula mboga za majani kwa wingi na matunda najitahidi angalau kwa wiki nafanya mazoezi ya kukimbia na kutembea angalau 1h au 2hrs kwa wiki mara 3-4, lengo ni kuburn calories angalau 4000kcl kwa wiki, wataalamu wansema ukiweza kuchoma calories 7700kcl kwa wikk maana yake unaweza kupunguza kg 1 ya uzito, Pia nimepunguza chumvi na niacha kutumia vitu byenye sukari na sukari kabisa.
Mgmfumo huu nataka niufanye kwa miezi sita huku naangalia maendeleo natumaini Mungu atanisaidia
Changamoto ninazokabiliana nazo, awali ilikuwa ngumu sana maana kuacha pombe inabidi upunguze marafiki, utafute activities za kufanya ule muda ambao ulikuwa unautumia kunywa hasa wikiend, nikifanya majarinio kadhaa mara tatu ya kuacha nikashimdwa jaribio la nne ndiyo nikafaulu
Upande wa maazoezi pia nilipata changamoto sana, kwanza ilinilazimu kuamka mapema sana 11 asubuhi nianze mazoezi au jioni saa 12:30 jioni baada ya mlo wa jioni, kudumisha ratiba hii ilikuwa ngumu awali lakini kwa sasa nimefaulu kwa kiasi chankuridhisha, Lakini pia awali nilipata shida ya goti kwasababubya mwili kuwa mzito hali iliyopeleka kukaa zaidi ya mwezi mmoja kuuguza goti, awali nilikuwa nakimbua sana kumbe ndiyo nikazua tatizo la goti.
Changamoto nyingine ni chakula wakati mwingine kama familia kuwa na special diet kwaajili yako inakuwa ngumu sana, inabidi ule chakula kilichopo.
Diet yangu najitahidi iwe hivi, Asubuhi, Aidha yai 1-2, kuchemsha au kukaangwa, ndizi mbivu 1, chai isiyo na sukari na punje mbili za kitunguu saaumu, maji kwa wingi.
Mchana, Matunda na mbogamboga na kaugali kadogo saba au tonge 6 an 8 ya kawaida au napiga desh nakunywa maji na ndizi 2
Jioni mbogamboga, magarage, tunda, na kama ni wali kidogo sana, kama kuna nyama nayo kidogo, maji chai ya moto na kitunguu saaumu then naenda mazoezi.
Najua wengine mnauzoefu tofauti naomba tushare wote.