Wenye uzoefu wa ujenzi wa nyumba tafadhali ushauri wenu

Wenye uzoefu wa ujenzi wa nyumba tafadhali ushauri wenu

davetz28

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2017
Posts
543
Reaction score
624
Tafadhali naomba mchango wa mawazo kwa wale wenye uzoefu wa ujenzi wa nyumba za makazi.

Ninataka kujenga nyumba ya vyumba vitatu vyenye sitting, dinning, store na kitchen pamoja na public toilets je gharama ya ujenzi inafika shilingi ngapi kwa nyumba ya kawaida?

Nataka nijenge nyumba walau kwa awamu lakini wachora ramani na kampuni kadhaa nilizowasiliana nazo wananipa mahesabu yanayopishana Sana. Asanteni kwa ushauri wenu

1590656726529.png
 
Kwa uelewa wangu mdogo hakuna changamoto ngumu kama kuweka budget ya ujenzi.. ksb kuna vitu ambavyo huwa havipo kwenye makadirio na vinakula hela nyingi na ndivyo vinapelekea kuharibu budget....

Ushauri jipange anza na budget msingi maji cement mchanga mawe nenda budget ya kuapndisha ukuta ... ring beam kenji bati. then rudi kenye finishing
 
kwa uelewa wangu mdogo hakuna changamoto ngumu kama kuweka budget ya ujenzi.. ksb kuna vitu ambavyo huwa havipo kwenye makadirio na vinakula hela nyingi na ndivyo vinapelekea kuharibu budget....

Ushauri jipange anza na budget msingi maji cement mchanga mawe nenda budget ya kuapndisha ukuta ... ring beam kenji bati. then rudi kenye finishing
Ni kweli fundi wa mwisho aliniambia kwa picha hiyo mfano gharama yake ni mil 55 tofauti kabisa na wengine.
Nadhani ushauri wako ni mzuri sana , ngoja nione wadau wengine wanasemaje
 
Upo mkoa Gani ..nikuandalie Quotations zote free ila kwa makubaliano ya kunipa kazi ya ujenzi
Malipo kidogo kwenye uandaaji wa Ramani
 
Kwa nyumba ya kuishi, nakushauri nunua material kama mawe, mchanga, nondo, cement, tofali na mbao za kufungia mkanda. Vitu vyote hivi hakikisha unavitunza vizuri kwenye kibanda chako au kwa jirani kisha vuta bomba la maji kwa ajili ya ujenzi, baada ya hapo simamia mwenyewe hakika utaokoa 35% ya gharama ya nyumba yote
 
Kwani unavyouliza gharama ya nyumba nzima unataka uijue ili utafute hela yote ndo ukaanze ujenzi? Kama ni hivyo utajikuta unachelewa sana kuanza unless unajenga kiprofesheno kwa kumkabidhi ujenzi injinia au kampuni, lakini kama utaamua kujenga kwa kutumia mafundi wa mtaani basi ingia site hata kama una hela ya msingi tu fanya kwa awamu ila uwe makini sana kwenye usimamizi. Ishu ni kuanza mengine yatafata baadae
 
Nashukuru sana, wakati mwingine naogopa kuanza ujenzi ambao siwezi kualiza. Kuna rafiki yangu alinza kujenga msingi tu kumaliza akagundua kuwa nyumba ni kubwa na hawezi kuimaliza, akaishia kuuza kabisa aanze kujipanga upya. Na kwa bahati mbaya akauza kwa hasara kubwa so unajua tunajifunza kwa makosa ya wengine?
 
Nakubaliana na wewe kwamba ni vizuri kuijua gharama ya jumla ili ujue kama utaweza kuimudu, lakini huo mfano wako wa mtu aliyefeli badala ya kukupa ujasiri unaweza ukawa unakupa woga tu mkuu...chukua na mifano ya waliofanikiwa kwa njia hiyo ili uwe inspired, ujenzi ni mgumu lakini inawezekana kwa kwenda mdogo mdogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maanat nimekuja hapa ili walifanikisha kwa namna yoyete wanipe uzoefu halafut na mimi nitachanganya na zangu
 
La kwanza na muhimu kuliko yote ni kuwa na subira!

Unless utumie mkandarasi kukujengea. Ila kama utatumia hawa mafundi wetu wa kienyeji...jiandae kisaikolojia kukabiliana na kila aina ya ushenzi....
Asante mkuu kwa ushauri, niwe na Subira ili iweje hujafafanua.Sunira hadi niwe na pesa kamili ya kumaliza mradi wote? Hapa sijaelewa
 
Izo quotations unazitoa kwa kina nani kwani? Nakushauri tafuta Qs mzuri akuandalie BoQ yako hutojutia hao wamekaa darasani kusoma hizo mambo achana na hao fundi kanjanja.
A qs estimate has an error of + or - 5% to the actual cost of the project nothing more nothing less.
 
Tupo makundi mawili
Wale wanaoenda kujenga wakiwa na budget yote ya nyumba

Na wale wa kuwa na kianzio kidogo

Wewe unataka ujenge kwa awamu hiyo nirahisi zaidi. Ili ujenge bila stress hakikisha budget ya msingi inakamilika ambayo lazima unayo,,

Then unganisha budget ya kupandisha ukuta na kupaua

Kwa nyanda za juu kusini hatua hiyo 18m napiga bati ya alaf G30. Hatua za mbele zitajiseti zenyewe.
 
Izo quotations unazitoa kwa kina nani kwani? Nakushauri tafuta Qs mzuri akuandalie BoQ yako hutojutia hao wamekaa darasani kusoma hizo mambo achana na hao fundi kanjanja.
A qs estimate has an error of + or - 5% to the actual cost of the project nothing more nothing less.
Asante mkuu, nilikuwa nasikia tu hizo BOQ sikujua maana yake.
 
Last weekend nilimvuta pembeni fundi wa kampuni fulani anisaidie kufanya makadirio, aisee nilijuta sijajua alinitisha sana au ni mimi tu ndio sina hela. Bado nakusanya maarifa hapa.
Bila sote tutakifunza kwa sababu tayari Kuna maoni yametolewa hivyo tutaweza kupata njia ya kuanzia
 
Nashukuru sana, wakati mwingine naogopa kuanza ujenzi ambao siwezi kualiza. Kuna rafiki yangu alinza kujenga msingi tu kumaliza akagundua kuwa nyumba ni kubwa na hawezi kuimaliza, akaishia kuuza kabisa aanze kujipanga upya. Na kwa bahati mbaya akauza kwa hasara kubwa so unajua tunajifunza kwa makosa ya wengine?

Ebwana hapo jifunze kweli maan ukishaweka msingi kwenye kiwanja kuuza inakuwa ishu sana.
 
Back
Top Bottom