Wenye uzoefu wa ujenzi wa nyumba tafadhali ushauri wenu

Wenye uzoefu wa ujenzi wa nyumba tafadhali ushauri wenu

Asante sana kwa ushauri wako nitawekea msisitizo wa namna ya kuchagua ramani nafuu kwangu
nyingine hii
Screenshot_20200602-195940.jpg
 
yangu ilizidi milioni 55 kutokana na mbwembwe zangu mwenyewe lakini milioni 55 ndio gharama standard.

Yaani unakuta ukienda dukani kuna materials unakuta zina bei tatu tofauti sasa mimi nikawa nachagua za bei ya juu makusudi kumbe mwisho wa siku inaleta muonekano ule ule tu.

Kingine pia usimamizi pamoja na bei za mafundi lazima uwe makini.
Mafundi huwa hawana bei maalum ya kujenga,ni wewe mwenyewe jinsi unavyopatana nao.

Ukipatana nao vizuri mwisho wa siku haitazidi pesa hiyo milioni 55.
Dah umeniacha hoi hapo kwenye materials, kama ulikua unachukua materials za bei juu kwa kulenga muonekano si ni bora ungechukua materials za mchina tu...mana ni bei ya chini na unakuta mounekano ni mzuri sema tu ni famba. Mi nilidhani ulikua unachagua materials za bei juu kwa kulenga ubora

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hivyo nilikuwa naambiwa na mafundi kwamba ukichukua vya bei ya juu vitaleta muonekano tofauti na pia ubora utakuwa juu lakini sasa hivi nagundua hata huo ubora walioniambia siuoni maana nyumba ilianza kuchubuka rangi kabla hata sijahamia,na baadhi ya kuta zimeanza kutoa alama za nyufa,gypsum nayo inaanza kuachia baadhi ya sehemu.

Na ndio maana sioni utofauti na wale walionunua materials ya bei rahisi upande wa ubora na hata muonekano.

Niliongea kifupi lakini nilimaanisha hivi
Dah umeniacha hoi hapo kwenye materials, kama ulikua unachukua materials za bei juu kwa kulenga muonekano si ni bora ungechukua materials za mchina tu...

Maana ni bei ya chini na unakuta mounekano ni mzuri sema tu ni famba. Mi nilidhani ulikua unachagua materials za bei juu kwa kulenga ubora

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Garama za ujenzi hazifanani, hata kama kwa ramani ile ile, kwanza inategemea ardhi sehemu unafanyika.

Mfano kwa wanaishi Dar, mtu anaejenga kuanzia kimara mpaka kibamba, mbezi mwisho mpaka goba, mbezi mwisho mpaka kinyelezi.

Hawezi kufanana garama za ujenzi na mtu aliejenga nymba kigambo, temeke Gongolamboto, chamanzi, kitonga, msongola, frem 10, mbagara.

Hata wakitumia ramani moja. Hivyo garama za ujenzi hukadiliwa kwa kuona ramani pamoja na eneo la ujenzi.
Kabisa, udongo haufanani, eneo la milima au tambarare, ujenzi wake tofauti...

Everyday is Saturday........................ 😎
 
Niliwahi mfuata Architech anichoree ramani akanichaji laki nne .. nikageuza fasta .. nikamcheki jamaa yangu akanipa ramani yake free of charge nikapiga jengo.
 
Nyumba ya vyumba vitatu ambayo in flat au ndogo ya kuishi inakuwa hivi,
Msingi utagharamia mfano

Mawe 90,000Tzs /au tofali za kulaza za inchi 6 kwa 150,000Tzs
Mchanga Lori mbili 200,000/= unabaki tena. Nunua ule wa Mawe Mawe na mwembamba kidogo wa zege.

Cement nunua mifuko 15 @ 13000Tzs weka
Mbao za kushikilia msingi pembeni zile za 1 by 10 hizi nunua used 50,000Tzs au azima.

Pesa ya Fundi na kibarua 100,000Tzs isizidi kwa msingi.
Mpaka hapo msingi tayari.

Njoo kupandisha tofali,
Nunua tofali 3500 za kuchoma bei 1,500,000Tzs au 900,000Tzs kutegemea na ulipo.

Nunua cement nyingine mifuko 25 hata kwa ajili ya kujengea tofali pia lenta na nondo za Laki 6 kwa ajili ya lenta na nguzo ya baraza.

Mwisho njoo pau kwa mbao za million 2 paa la wastani na bati za million 3.5 nzuri
Fundi mlipe milioni na laki tano mpaka kupaua.

Madirisha milango hizo ni cost nyingine madirisha 8 ya security laki 9 na aluminium ukiweka itaeza kula milioni 1.4 pamoja na milango yote .
Piga hesabu angalia vizuri unapata nyumba
Maji sijaweka na mfumo wa Maji taka pia bado.

Nicheki unipigie 0678502276 nikupe ushauri.
Mkuu hiyo ya fundi ni kuanzia msingi hadi juu au kufunga paa tu?.
 
Nitafute nikuandalie schedule of material tu kwa nb nijue unajenga wapi.
 
Niliwahi mfuata Architech anichoree ramani akanichaji laki nne .. nikageuza fasta .. nikamcheki jamaa yangu akanipa ramani yake free of charge nikapiga jengo.
Kuna mwenzako kaleta uzi analalamika jengo lina ufa, hii tabia ya kutotumia wataalam itawa cost sana.

Sasa wewe umeona laki 4 ni kubwa ila siku yakija kukuta utaanza kulalamika huna ela ya kuziba ufa.

Rahisi ni gharama.
 
Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
Hata ukitumia wataalamu ufa unaweza kujitokeza vilevile.usikariri eti coz umetumia mtaalamu haweze fanya makosa.either ni fundi kitaa au mtaalamu yeyote yule anaweza kwa uzembe kusababisha ufa japokuwa makosa kwa mtaalamu huwa sio mara nyingi kama fundi wa mtaani.

Tumejenga so tunashuhudia vyote mkuu
 
Mahesabu yangu kwa kuanzia nifikie hatua ya kuezeka, kuweka milango ya nje na kuhamia 25 million haiwezi kunifikisha kwa ramani hiyo? Halafu mengine taratibu?
Sasa wewe unatakiwa utambue kwanza malengo yako ya kujenga.

1. Kama unajenga kwaajiri ya kuhamia sasa hivi kutokana na pressures za kimaisha then inakubidi ubadili mbinu za ujenzi kwa maana kama budget yako ipo 25 million, then punguza cost za ujenzi kama kupunguza idadi ya vyumba, mfano hapo weka vyumba viwili tu vya kulala hizo sehemu zingine zitabaki kama zilivyo, tengeneza ramani za kisasa ambazo ni za budget nafuu. Kwa milioni 25 unatengeneza nyumba ya vyumba viwili ya kisasa na chenji itabaki.

2. Kama ni swala la kutokuwa na pesa ya kutosha unaweza subiria upate zaidi au anza kwa kuipandisha kidogo kidogo ila kwa muda huo huo uwe unatafuta pesa ya kuandaa kuendelea na steji zilizobakia.
 
haiwezi kutosha kabisa.
Kujenga pagale/boma peke yake inachukua kama milioni 10 hivi,na kuezeka bati ya msauzi pia inakula milioni 10 kwa hiyo kwenye milioni 25 utakuwa umebakiwa na milioni 5 tu hapo hujajaza kifusi ndani,hujaweka zege ndani,hujapiga plasta,hujaweka magrill lazima ukwame
Mmmmmmhmn inategemea na ujenzi, mafundi uliowapa kazi, eneo, na kadhalika. 25 million ni bajeti ya kueleweka kabisa bona kufanyia maisha.
 
Dah umeniacha hoi hapo kwenye materials, kama ulikua unachukua materials za bei juu kwa kulenga muonekano si ni bora ungechukua materials za mchina tu...mana ni bei ya chini na unakuta mounekano ni mzuri sema tu ni famba. Mi nilidhani ulikua unachagua materials za bei juu kwa kulenga ubora

Sent using Jamii Forums mobile app
Babu materials za ujenzi tena uchukue za kichina china....
 
Ndio hivyo nilikuwa naambiwa na mafundi kwamba ukichukua vya bei ya juu vitaleta muonekano tofauti na pia ubora utakuwa juu lakini sasa hivi nagundua hata huo ubora walioniambia siuoni maana nyumba ilianza kuchubuka rangi kabla hata sijahamia,na baadhi ya kuta zimeanza kutoa alama za nyufa,gypsum nayo inaanza kuachia baadhi ya sehemu.

Na ndio maana sioni utofauti na wale walionunua materials ya bei rahisi upande wa ubora na hata muonekano.

Niliongea kifupi lakini nilimaanisha hivi
Jamaa walikupiga. Mafundi sio watu wa kuwaruhusu wakupeleka duka la vifaa vya ujenzi.

Nenda mwenyewe kafanyaje makadilio ya bei kwa kupita window shopping. Baadhi ya mafundi ni matapeli na sio waaminifu.
 
Inategemea una haraka kiasi gani kuhamia,kama una haraka sana ya kuhamia sawa haikufai hii ramani.

Na kingine pia kuna nyumba huwa naziona kwenye matangazo zinauzwa kwa bei kama hiyo zinakuwa zimebakiza hatua kidogo kukamilika ila unaweza kuhamia.
Vinginevyo milioni 25 huwezi kujenga nyumba ya kisasa labda ujenge mgongo wa tembo.
Mimi nawashangaa sana vijana,unakuta mtu ana Mil 12 tu.anasema kuwa ndo bajeti ya ujenzi wa nyumba mpka inakamilika..unamuuliza ni bajeti ya banda au nyumba? Anakuona kama una dharau
 
Niliwahi mfuata Architech anichoree ramani akanichaji laki nne .. nikageuza fasta .. nikamcheki jamaa yangu akanipa ramani yake free of charge nikapiga jengo.
Yeah akili ndio kama hizo. Yaani kuna vitu unatazama na hali ya sasa ya uchumi.

Hivi kweli sisi akina average Joe's uje utuchaji laki nne kwaajiri ya ramani ya nyumba.

Unajua hizi vitu za ujenzi zilikuwapo hata kabla ya huu uchoraji wa kisasa na watu walichora ramani bila kulipa hiyo laki 4.

Sasa why mtu uhangaike na mtu?!
 
Tatizo wakiona watu wamejenga wanajua ni lelemama wanachukulia poa.
wanafikiri kujenga ni kama kwenda showroom kuchukua vitz na kuondoka.
Mimi nawashangaa sana vijana,unakuta mtu ana Mil 12 tu.anasema kuwa ndo bajeti ya ujenzi wa nyumba mpka inakamilika..unamuuliza ni bajeti ya banda au nyumba? Anakuona kama una dharau
 
Niliwahi mfuata Architech anichoree ramani akanichaji laki nne .. nikageuza fasta .. nikamcheki jamaa yangu akanipa ramani yake free of charge nikapiga jengo.
Kumbe alikupa ramani yake kwa hiyo mkaigana bila kuwa na uniqueness ya nyumba,pili hiyo yake alichorewa na mafundi au alichora kwa mtaalamu?

1.Mara nyingi nyumba za kujenga/kuezeka kwa ramani za kubumba kwa mafundi wasio na taaluma ya ujenzi huwa hazivutii hata ufanye finishing ya namna gani itakuwa na muonekano mbaya tu na unaishia kuichukia nyumba yako mwenyewe.Nyumba zote kali unazoziona zina michoro na vice versa.

2.Kununua ramani yako mwenyewe inakufanya kuwa na jengo ambalo halifanani na mwingine kwa hiyo inakuwa ni hatimiliki yako na uniqueness ambayo mtu akipita ataipenda.

3.Kuna wataalamu wa bei za kawaida wa kuchora ramani kuanziaT.150,000/=-Tsh.400,000/= kutegemeana na aina ya mchoro unaotaka wewe.Haingii akilini mtu anajenga jengo lamamilioni eti ashindwe kulipia ramani nzuri kwa tulaki laki huto.Mwisho kama unajenga kwenye plot ramani huwezi kuikwepa maana itakuhitaji kibali cha ujenzi be it umeshaanza kuijenga au hapana lazima ukalipe pesa ya kibali ambayo ni lazima iambatane na michoro ya jengo unless unajenga kwenye squatter.
 
Mimi nawashangaa sana vijana,unakuta mtu ana Mil 12 tu.anasema kuwa ndo bajeti ya ujenzi wa nyumba mpka inakamilika..unamuuliza ni bajeti ya banda au nyumba? Anakuona kama una dharau
Kwahiyo mil12 huwez jenga hata chumba na sebule cha kuanzia life ili uepukane na kelele za upangaji
 
Back
Top Bottom