Wenye uzoefu wa ujenzi wa nyumba tafadhali ushauri wenu

Wenye uzoefu wa ujenzi wa nyumba tafadhali ushauri wenu

Tafadhali naomba mchango wa mawazo kwa wale wenye uzoefu wa ujenzi wa nyumba za makazi.

Ninataka kujenga nyumba ya vyumba vitatu vyenye sitting, dinning, store na kitchen pamoja na public toilets je gharama ya ujenzi inafika shilingi ngapi kwa nyumba ya kawaida?

Nataka nijenge nyumba walau kwa awamu lakini wachora ramani na kampuni kadhaa nilizowasiliana nazo wananipa mahesabu yanayopishana Sana. Asanteni kwa ushauri wenu

View attachment 1461440
MAKTABA YA UVIMO

CHANZO CHA WEWE KUMILIKI NYUMBA ISIYO YAHADHI YAKO AU KUTOMILIKI KABISA

Ndugu wadau, katika makta ya Uvimo ya leo, tutajadili sababu za watu wengi kumiliki nyumba ambazo sio hadhi zao au kushindwa kumiliki nyumba kabisa.

Maktaba inakumbusha kuwa Ndoto isiyo na sababu kama kiini na chachu ya kustawisha mafanikio, hufa mapema

Zipo sababu lukuki za kutofanikisha malengo na hatimaye ndoto. Sababu hizi ndizo zimesisimua kushika kalamu kujadilisha haya.

Juma tatu hii ya 27-Sep saa mbili usiku katika group la Uvimo Public Center,

Wasiliana nasi kwa huduma zote za ujenzi

0753927572
0629361896View attachment 1954267
IMG-20210926-WA0006.jpg
View attachment 1954268
 
Ni kweli fundi wa mwisho aliniambia kwa picha hiyo mfano gharama yake ni mil 55 tofauti kabisa na wengine.
Nadhani ushauri wako ni mzuri sana , ngoja nione wadau wengine wanasemaje
Tena hapo iyo 55 M ni makadirio ila ukienda madukan kwa sasa bei ya vifaa vya ujenzi ime shoot sanaa yaan kila kukicha vitu vina panda bei
 
Tutumie wataalamu jamani yaani umeamua kujenga nyumba ya 20+m laki kadhaa haziwezi kukushinda kumlipa mtaalamu.

Quantity Surveyor (Qs) huyu amekaa darasani 4yrs plus uzoefu wa hizi kazi. Atakusaidia yafuatayo;
1. Kukuandalia BOQ kuonyesha ukubwa wa kila kipengele (element) na gharama zake mfano kulingana na ramani yako ukuta ni mita za mraba ngapi na zitagharimu kiasi gani materials pamoja na labour (ufundi).

2. Atakushauri aina za materials za kutumia kulingana na kipato chako bila kuathiri ubora wa nyumba yako.

3. Atakushauri namna bora ya kupunguza gharama za ujenzi.

Mwisho utapata budget yako ya ujenzi kulingana na ramani uliyonayo. Ukihitaji huduma karibu PM
 
Na support kabisa wataalam ni muhimu mno wazoefu sisi tuliojenga Jenga tunafahamu mahali tuliwahi kukosea na tukajuta
 
Nyumba ya vyumba vitatu ambayo in flat au ndogo ya kuishi inakuwa hivi,
Msingi utagharamia mfano

Mawe 90,000Tzs /au tofali za kulaza za inchi 6 kwa 150,000Tzs
Mchanga Lori mbili 200,000/= unabaki tena. Nunua ule wa Mawe Mawe na mwembamba kidogo wa zege.

Cement nunua mifuko 15 @ 13000Tzs weka
Mbao za kushikilia msingi pembeni zile za 1 by 10 hizi nunua used 50,000Tzs au azima.

Pesa ya Fundi na kibarua 100,000Tzs isizidi kwa msingi.
Mpaka hapo msingi tayari.

Njoo kupandisha tofali,
Nunua tofali 3500 za kuchoma bei 1,500,000Tzs au 900,000Tzs kutegemea na ulipo.

Nunua cement nyingine mifuko 25 hata kwa ajili ya kujengea tofali pia lenta na nondo za Laki 6 kwa ajili ya lenta na nguzo ya baraza.

Mwisho njoo pau kwa mbao za million 2 paa la wastani na bati za million 3.5 nzuri
Fundi mlipe milioni na laki tano mpaka kupaua.

Madirisha milango hizo ni cost nyingine madirisha 8 ya security laki 9 na aluminium ukiweka itaeza kula milioni 1.4 pamoja na milango yote .
Piga hesabu angalia vizuri unapata nyumba
Maji sijaweka na mfumo wa Maji taka pia bado.

Nicheki unipigie 0678502276 nikupe ushauri.
Shukurani sana Mkuu
 
Back
Top Bottom