Wenye uzoefu wa ujenzi wa nyumba tafadhali ushauri wenu

Nakubaliana na wewe kwamba ni vizuri kuijua gharama ya jumla ili ujue kama utaweza kuimudu, lakini huo mfano wako wa mtu aliyefeli badala ya kukupa ujasiri unaweza ukawa unakupa woga tu mkuu...chukua na mifano ya waliofanikiwa kwa njia hiyo ili uwe inspired, ujenzi ni mgumu lakini inawezekana kwa kwenda mdogo mdogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Garama za ujenzi hazifanani, hata kama kwa ramani ile ile, kwanza inategemea ardhi sehemu unafanyika.

Mfano kwa wanaishi Dar, mtu anaejenga kuanzia kimara mpaka kibamba, mbezi mwisho mpaka goba, mbezi mwisho mpaka kinyelezi.

Hawezi kufanana garama za ujenzi na mtu aliejenga nymba kigambo, temeke Gongolamboto, chamanzi, kitonga, msongola, frem 10, mbagara.

Hata wakitumia ramani moja. Hivyo garama za ujenzi hukadiliwa kwa kuona ramani pamoja na eneo la ujenzi.
 
Asante Sana mkuu kwa wazo hilo la mahali pa ujenzi linavyoweza kuongeza au kupunguza gharama za ujenzi
 
Izo quotations unazitoa kwa kina nani kwani? Nakushauri tafuta Qs mzuri akuandalie BoQ yako hutojutia hao wamekaa darasani kusoma hizo mambo achana na hao fundi kanjanja.
A qs estimate has an error of + or - 5% to the actual cost of the project nothing more nothing less.
Usomi mwingi naona
 
Nyumba ya vyumba vitatu ambayo in flat au ndogo ya kuishi inakuwa hivi,
Msingi utagharamia mfano

Mawe 90,000Tzs /au tofali za kulaza za inchi 6 kwa 150,000Tzs
Mchanga Lori mbili 200,000/= unabaki tena. Nunua ule wa Mawe Mawe na mwembamba kidogo wa zege.

Cement nunua mifuko 15 @ 13000Tzs weka
Mbao za kushikilia msingi pembeni zile za 1 by 10 hizi nunua used 50,000Tzs au azima.

Pesa ya Fundi na kibarua 100,000Tzs isizidi kwa msingi.
Mpaka hapo msingi tayari.

Njoo kupandisha tofali,
Nunua tofali 3500 za kuchoma bei 1,500,000Tzs au 900,000Tzs kutegemea na ulipo.

Nunua cement nyingine mifuko 25 hata kwa ajili ya kujengea tofali pia lenta na nondo za Laki 6 kwa ajili ya lenta na nguzo ya baraza.

Mwisho njoo pau kwa mbao za million 2 paa la wastani na bati za million 3.5 nzuri
Fundi mlipe milioni na laki tano mpaka kupaua.

Madirisha milango hizo ni cost nyingine madirisha 8 ya security laki 9 na aluminium ukiweka itaeza kula milioni 1.4 pamoja na milango yote .
Piga hesabu angalia vizuri unapata nyumba
Maji sijaweka na mfumo wa Maji taka pia bado.

Nicheki unipigie 0678502276 nikupe ushauri.
 
Ni kweli fundi wa mwisho aliniambia kwa picha hiyo mfano gharama yake ni mil 55 tofauti kabisa na wengine.
Nadhani ushauri wako ni mzuri sana , ngoja nione wadau wengine wanasemaje
Huyu fundi alikuwa sahihi.
Hata mimi nilitaka kukwambia makadirio yanayoendana na huyu fundi.
Nimekubali makadirio ya huyu fundi kwa sababu mimi nimejenga nyumba inayoendana na hiyo.
 
Fundi ana bajeti kubwa sana
Huyu fundi alikuwa sahihi.
Hata mimi nilitaka kukwambia makadirio yanayoendana na huyu fundi.
Nimekubali makadirio ya huyu fundi kwa sababu mimi nimejenga nyumba inayoendana na hiyo.
 
Nyumba ya vyumba vitatu ambayo in flat au ndogo ya kuishi inakuwa hivi,
Msingi utagharamia mfano
Mawe 90,000Tzs /au tofali za kulaza za inchi 6 kwa 150,000Tzs
Mchanga Lori mbili 200,000/= unabaki tena. Nunua ule wa Mawe Mawe na mwembamba kidogo wa zege.
Cement nunua mifuko 15 @ 13000Tzs weka
Mbao za kushikilia msingi pembeni zile za 1 by 10 hizi nunua used 50,000Tzs au azima.
Pesa ya Fundi na kibarua 100,000Tzs isizidi kwa msingi.
Mpaka hapo msingi tayari.

Njoo kupandisha tofali,
Nunua tofali 3500 za kuchoma bei 1,500,000Tzs au 900,000Tzs kutegemea na ulipo.
Nunua cement nyingine mifuko 25 hata kwa ajili ya kujengea tofali pia lenta na nondo za Laki 6 kwa ajili ya lenta na nguzo ya baraza.

Mwisho njoo pau kwa mbao za million 2 paa la wastani na bati za million 3.5 nzuri
Fundi mlipe milioni na laki tano mpaka kupaua.
Madirisha milango hizo ni cost nyingine madirisha 8 ya security laki 9 na aluminium ukiweka itaeza kula milioni 1.4 pamoja na milango yote .
Piga hesabu angalia vizuri unapata nyumba
Maji sijaweka na mfumo wa Maji taka pia bado.
Nicheki unipigie 0678502276 nikupe ushauri.
Nakushukuru sana kwa muda wako na ushauri wako pia.
 
Huyu fundi alikuwa sahihi.
Hata mimi nilitaka kukwambia makadirio yanayoendana na huyu fundi.
Nimekubali makadirio ya huyu fundi kwa sababu mimi nimejenga nyumba inayoendana na hiyo.
Kwa maana nyumba yako iligharimu milioni 55 kama makadirio ya fundi huyu wa mwisho?
 
yangu ilizidi milioni 55 kutokana na mbwembwe zangu mwenyewe lakini milioni 55 ndio gharama standard.

Yaani unakuta ukienda dukani kuna materials unakuta zina bei tatu tofauti sasa mimi nikawa nachagua za bei ya juu makusudi kumbe mwisho wa siku inaleta muonekano ule ule tu.

Kingine pia usimamizi pamoja na bei za mafundi lazima uwe makini.
Mafundi huwa hawana bei maalum ya kujenga,ni wewe mwenyewe jinsi unavyopatana nao.

Ukipatana nao vizuri mwisho wa siku haitazidi pesa hiyo milioni 55.
 
Asante
 
Basi hiyo ramani haitanifaa sitaki nyumba imayozidi mil25 kwa sasa
 
Inategemea una haraka kiasi gani kuhamia,kama una haraka sana ya kuhamia sawa haikufai hii ramani.

Na kingine pia kuna nyumba huwa naziona kwenye matangazo zinauzwa kwa bei kama hiyo zinakuwa zimebakiza hatua kidogo kukamilika ila unaweza kuhamia.
Vinginevyo milioni 25 huwezi kujenga nyumba ya kisasa labda ujenge mgongo wa tembo.

Mahesabu yangu kwa kuanzia nifikie hatua ya kuezeka, kuweka milango ya nje na kuhamia 25 million haiwezi kunifikisha kwa ramani hiyo? Halafu mengine taratibu?
 
haiwezi kutosha kabisa.
Kujenga pagale/boma peke yake inachukua kama milioni 10 hivi,na kuezeka bati ya msauzi pia inakula milioni 10 kwa hiyo kwenye milioni 25 utakuwa umebakiwa na milioni 5 tu hapo hujajaza kifusi ndani,hujaweka zege ndani,hujapiga plasta,hujaweka magrill lazima ukwame
 
Asante sana kwa ushauri wako nitawekea msisitizo wa namna ya kuchagua ramani nafuu kwangu
 
kuna nyumba kama hizi zinauzwa huenda xikaendana na bajeti yako kuna watu wamekwama wanauza kwa bei za kutupa
Screenshot_20200602-170433.jpg
 
Back
Top Bottom