Wenyeviti 'wakongwe' vyama vya siasa wanaopigania demokrasia

Wenyeviti 'wakongwe' vyama vya siasa wanaopigania demokrasia

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Ni katika kutafakari siasa za Tanzania na muelekeo mzima. Nikajikuta nikitafakari muda wote ambao viongozi wa vyama vya siasa wamekuwa wakishikilia hatamu za uongozi pasipo kuonyesha kuchoka, na wakiwa wepesi kurusha kila aina ya kashfa kwa chama tawala.

Freeman Mbowe aliingia katika uongozi mwaka 2004, amefikisha miaka 18 akiongoza CHADEMA na haonyeshi kupungukiwa nguvu wala hamu za kuwa mwenyekiti. Huo ni umri wa kijana anayeanza kupata haki ya kupiga kura anayefanya mtihani wa kidato cha sita.

Mbatia wa NCCR amefikisha miaka 22 akiwa kiongozi mkuu wa chama chake. Huyu ni Mzee wa matukio, anasubiri litokee janga la asili akosoe sera na mitazamo ya CCM akiwa kitaaluma ni mtu wa fani hizo za majanga. Pia husubiri upepo fulani wa kisiasa utokee ili apate cha kuongea kwa kuwaita wanahabari.

Profesa Lipumba amefikisha miaka 23 akiongoza CUF akikumbana na misukosuko ya kila aina. Huyu anajua sana kuishi na upepo wa kisiasa. Huwa anapata kazi zenye pesa nyingi za kiuchumi za Ulaya, anakaa huko miezi sita akirudi anakuwa yupo njema kabisa. Halafu anasikilizia mwito wa Hayati JPM au Mama SSH pale ikulu, kinachoongelewa wanakijua wenyewe!.

Mzee Lyatonga Mrema amefikisha miaka 23 akioongoza chama cha TLP, huyu ni mkongwe amekwepa mishale ya kila aina huko mwituni mpaka uzee umeshapiga hodi kwa sasa. Anahudhuria mikutano mikuu ya CCM na anatangaza hadharani kumuunga mkono mgombea wa CCM. Huwa naachwa na vicheko namna JK anavyomuongelea kwa vicheko kama vya masikhara.

Hao ni viongozi wakuu wa vyama vya upinzani Tanzania wanaoelekea kufikisha robo karne madarakani huku wakiikosoa demokrasia ndani ya nchi hii. Siasa ni akili kichwani mwako, ukiwa mjanja utaishi na watu vizuri huku ukizeeka na benki zikiwa zinaingia pesa ambazo ni pembeni ya kile kipato chako cha halali.
 
Jitahidi kutofautisha kati ya kupigania Demokrasia na kupigania Matumbo yao na Tamaa za madaraka .
 
Na mtoa hoja pia usisahau ccm inaitawala nchi yetu kwa zaidi ya 60yrs na bado wale maadui wakubwa wametamalaki, UJINGA,UMASIKINI, RUSHWA na sasa wamepata cousin wao RUSHWA, huku lingusenguse kwa mfano hadi sasa maji salama ni shida wakati huku kuna mvua ya kutosha (tungejenga mabwawa kuvuna maji ya mvua)na mto Ruvuma wenye fresh water upo within 200km away!
 
Back
Top Bottom