Wenzangu mkiwa na hasira au kuvurugwa kichwa mnafanyaje ili mkae sawa?

Wenzangu mkiwa na hasira au kuvurugwa kichwa mnafanyaje ili mkae sawa?

sepema

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2019
Posts
591
Reaction score
1,001
Amani iwe nanyi.

Naomba tu mnisaidie kwani sijielewi hata kidogo. Nipo kwenye kiwango cha juu cha hasira iliyochanganyika na mvurugo wa akili. Chanzo ni mambo na changamoto za kimaisha.

Sasa nyie mnafanyaje kuwa sawa pindi mnapokutana na hali kama hii?

Pengine mbinu unayotumia itanisaidia na mimi.

Wasalaam!
 
Kwanza Pole maana changamoto ni sehemu ya maisha na ukiona changamoto zimezidi usidhani upo peke yako tupo wengi ila upokeaji ndo tuna tofautiana.

Kwanza binafsi huwa najichanganya na watu ili kupunguza mawazo, pia kuwa mtu wa ibada sana, tafuta watu wenye mtazamo chanya, epuka kukaa peke yako, nenda mazingira mapya, mwisho kabisa jaribu kufanya kitu kipya.
 
Ungekuwa specific zaidi kwani kuna changamoto za kimaisha za aina nyingi. Fedha? Mke/Mume mkorofi? Kesi? Suluhisho sahihi linatokana na aina ya changamoto. Pia kila mtu ana namna yake ya kukabiliana na changamoto. General rule ni: toka nyumbani, piga story na watu uone jinsi kuna watu wengine wenye changamoto kuliko wewe. Na mwisho jipe moyo na kamwe usikate tamaa
 
Huyo aliye leta Heineken pepo atapasikia tu maana hata unywe kreti zima baada ya pombe kwisha kichwani tabu ipo pale pale zaidi sana umepoteza pes yako bure .... kwanz nikinywa bia naumwa kichwa balaa na kulala nashindwa kabisa
Ni kweli, pombe haijawahi kuwa sehemu ya kujenga.

Huwa nawashangaa watumiaji
 
Kwanza Pole maana changamoto nisehemu ya maisha na ukiona changamoto zimezidi usidhani upo peke yako tupo wengi ila upokeaji ndo tuna tofautiana. Kwanza binafsi huwa najichanganya na watu ili kupunguza mawazo, pia kuwa mtu wa ibada sana, tafuta watu wenye mtazamo chanya, epuka kukaa peke yako, nenda mazingira mapya, mwisho kabisa jaribu kufanya kitu kipya.
Shukrani Sana mkuu
 
sepema pole sana rafiki , fanya hivi ondoka walipo watu kakae mwenyewe na ufanye kile ambacho uwa unakipenda sana mfano kama unakunywa pombe agiza hata bia moja unywe huku unawaza mambo ya maendeleo juu ya maisha yako

Baada ya muda hasira zitaisha na utakuwa kawaida baada ya hapo sasa ni muda wa kuwasamehe wote waliosababisha hasira either kwa kuapa kutolipa kisasi au kuwaface .Kwa hayo utakuwa umeregain katika hali yako ya kawaida.

Ushauri tu [emoji120][emoji120][emoji120]

TEKERI.
 
Ungekuwa specific zaidi kwani kuna changamoto za kimaisha za aina nyingi. Fedha? Mke/Mume mkorofi? Kesi? Suluhisho sahihi linatokana na aina ya changamoto. Pia kila mtu ana namna yake ya kukabialina na changamoto. General rule ni: toka nyumbani, piga story na watu uone jinsi kuna watu wengine wenye changamoto kuliko wewe. Na mwisho jipe moyo na kamwe usikate tamaa
Nilitegemea umwambia aingie zake mtandaoni ashushe video zake kadhaa za pilau, apige zake kimoja cha nguvu alale.
 
Amani iwe nanyi.

Naomba tu mnisaidie kwani sijielewi hata kidogo. Nipo kwenye kiwango Cha juu Cha hasira iliyochanganyika na mvurugo wa akili.Chanzo ni Mambo na changamoto zakimaisha...
Piga jogging ya kishikaji, ukiweza valia na kamziki Kwa mbali masikioni. Ukipumzika Kaa tafakari Kwa utulivu, utatokaje ulipokwamia.
 
“Mwenye nguvu si yule mwenye kupiga watu mieleka bali ni yule anayemiliki nafsi yake anapo ghadhibika”.
 
Tabia ulizonazo ndizo zinachangia hasira, chunguza vyakula unavyokula, mazungumzo ambayo unayashiriki mara nyingi huko ndio kunatokea hayo, mabishano yasiyo na maana, mahusiano yasiyo na utulivu kila wakati wewe unakua ndio msuluhishi wa vitu vidogo vidogo, punguza matumizi ya pombe, sigara na kahawa pia jaribu kuwasamehe watu waliokukosea kwa maneno au vitendo, jisamehe wewe mwenyewe kwa kushindwa kutekeleza baadhi ya malengo yako, zingatia muda wa kulala, pumzika/ lala masaa 7/8.
 
Tabia ulizo nazo ndizo zinachangia hasira, chunguza vyakula unavyokula,mazungumzo ambayo unayashiriki mara nyingi huko ndio kunatokea hayo, mabishano yasiyo na maana, mahusiano yasiyo na utulivu kila wakati wewe unakua ndio msuluhishi wa vitu vidogo vidogo, punguza matumizi ya pombe, sigara na kahawa pia jaribu kuwasamehe watu waliokukosea kwa maneno au vitendo, jisamehe wewe mwenyewe kwa kushindwa kutekeleza baadhi ya malengo yako, zingatia muda wa kulala, pumzika/ lala masaa 7/8.
Shukrani mkuu
 
Back
Top Bottom