Ni kweli, pombe haijawahi kuwa sehemu ya kujenga.Huyo aliye leta Heineken pepo atapasikia tu maana hata unywe kreti zima baada ya pombe kwisha kichwani tabu ipo pale pale zaidi sana umepoteza pes yako bure .... kwanz nikinywa bia naumwa kichwa balaa na kulala nashindwa kabisa
Shukrani Sana mkuuKwanza Pole maana changamoto nisehemu ya maisha na ukiona changamoto zimezidi usidhani upo peke yako tupo wengi ila upokeaji ndo tuna tofautiana. Kwanza binafsi huwa najichanganya na watu ili kupunguza mawazo, pia kuwa mtu wa ibada sana, tafuta watu wenye mtazamo chanya, epuka kukaa peke yako, nenda mazingira mapya, mwisho kabisa jaribu kufanya kitu kipya.
Nilitegemea umwambia aingie zake mtandaoni ashushe video zake kadhaa za pilau, apige zake kimoja cha nguvu alale.Ungekuwa specific zaidi kwani kuna changamoto za kimaisha za aina nyingi. Fedha? Mke/Mume mkorofi? Kesi? Suluhisho sahihi linatokana na aina ya changamoto. Pia kila mtu ana namna yake ya kukabialina na changamoto. General rule ni: toka nyumbani, piga story na watu uone jinsi kuna watu wengine wenye changamoto kuliko wewe. Na mwisho jipe moyo na kamwe usikate tamaa
Piga jogging ya kishikaji, ukiweza valia na kamziki Kwa mbali masikioni. Ukipumzika Kaa tafakari Kwa utulivu, utatokaje ulipokwamia.Amani iwe nanyi.
Naomba tu mnisaidie kwani sijielewi hata kidogo. Nipo kwenye kiwango Cha juu Cha hasira iliyochanganyika na mvurugo wa akili.Chanzo ni Mambo na changamoto zakimaisha...
Shukrani mkuuTabia ulizo nazo ndizo zinachangia hasira, chunguza vyakula unavyokula,mazungumzo ambayo unayashiriki mara nyingi huko ndio kunatokea hayo, mabishano yasiyo na maana, mahusiano yasiyo na utulivu kila wakati wewe unakua ndio msuluhishi wa vitu vidogo vidogo, punguza matumizi ya pombe, sigara na kahawa pia jaribu kuwasamehe watu waliokukosea kwa maneno au vitendo, jisamehe wewe mwenyewe kwa kushindwa kutekeleza baadhi ya malengo yako, zingatia muda wa kulala, pumzika/ lala masaa 7/8.