Wenzetu huko Mbele huwa wanahamasisha mashabiki waende uwanjani au mashabiki wana mapenzi na timu zao hata zikishuka Daraja?

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Bongo uswahili ni mwingi sana, na bado sana hata kwenye ushabiki wa Mpira, tuna ushabiki mwingi wa mdomoni wa kubishana kwenye vijiwe vya kahawa na mitandao ya kijamii kama humu.

Emegine kwamba mashabaki wenye timu yao lazima wahamasishwe, gari izunguke mtaani watu wakikata mauno kwenye gari ili wahamasishwe waingie uwanjani imefika hatua tunasema fulani anajua sana kuhamasisha , fulani hajui.

Ujinga ujinga sana, full uswahili.

Kwamba wasipo hamasishwa basi uwanjani hawaendi kushabikia timu yao na hao hao utasikia wanasema ohoo hatukuhamasishwa, hamasa ilikiwa ndogo sana hivyo tukaona tusiende. Ujinga.

Wenzetu huko Mbele tunaona timu inavuruta mkia still mashabiki wanajaa uwanjani kuisapoti timu yao ya mwisho kwenye msimamo wa ligi, na timu inashuka Daraja wanashuka nayo, inapanda wanapanda nayo.

Bongo timu ikipigwa mechi mbili mfulukizo eti mashabiki uwanjani hawaendi au lazima wabembelezwe sana.

Hakuna mashabiki seriou wa mpira Tanzakia tuna mashabiki waswahili, full ushabiki wa mdomoni, kwenye mitandao ya kijamii, vijiwe vya kahawa huko ndiko wamejaa. Shabiki muulize mara ya mwisho kununua jezi lini?
 
1000211276.jpg
1000211276.jpg
 
Mashabik mpaka watangaziwe kuna supu au miso misondo atakwepo ndo wanajaaa
 
Msichojua ni kwamba mashabiki wengi hawafiki uwanjani kutokana na kipato kidogo.

Kuna watu kipato chao Kwa siku ni 5000 mpaka 6000 Tsh hapohapo boss ni mkali.

Mtu huyu ana mke na watoto.
Aende uwanjani akatoe 10000 au 5000 uwanjani inakuwa ngumu.

Hujiulizi mbona kukitangazwa bure watu wanajaa?

Lakini licha ya hiyo bure bado mtu ana kosa 3000 ya kwenda na kurudi mfano

Mbezi mwisho to Taifa.

Tanzania ni nchi yenye watu wenye maisha magumu mno sema tu wameridhika na kuzoea.

Mtu akienda karume hapo anarudi amependeza

Shati 3000/=
Suruali 5000/=
Raba 6000/=
Kapelo 2000/=
Saa 1500/=

Yaani huyooo keshapendeza , tena akiwa na buku 5 analewa na yeye kwani
Kuna pombe zinaitwa visungura ni buku mbili tu

Mkewe nyumbani ana vijora vingi tu havivuki bei ya 7000/= per pic.

Haya maisha wewe acha tu
Halafu kuna watu wanasema Mshahara wa laki nane Kwa mwezi mdogo hapo Hana mtoto Hana mke. Labda mnatetea

Degrees zenu
 
Bongo uswahili ni mwingi sana, na bado sana hata kwenye ushabiki wa Mpira, tuna ushabiki mwingi wa mdomoni wa kubishana kwenye vijiwe vya kahawa na mitandao ya kijamii kama humu.

Emegine kwamba mashabaki wenye timu yao lazima wahamasishwe, gari izunguke mtaani watu wakikata mauno kwenye gari ili wahamasishwe waingie uwanjani imefika hatua tunasema fulani anajua sana kuhamasisha , fulani hajui.

Ujinga ujinga sana, full uswahili.

Kwamba wasipo hamasishwa basi uwanjani hawaendi kushabikia timu yao na hao hao utasikia wanasema ohoo hatukuhamasishwa, hamasa ilikiwa ndogo sana hivyo tukaona tusiende. Ujinga.

Wenzetu huko Mbele tunaona timu inavuruta mkia still mashabiki wanajaa uwanjani kuisapoti timu yao ya mwisho kwenye msimamo wa ligi, na timu inashuka Daraja wanashuka nayo, inapanda wanapanda nayo.

Bongo timu ikipigwa mechi mbili mfulukizo eti mashabiki uwanjani hawaendi au lazima wabembelezwe sana.

Hakuna mashabiki seriou wa mpira Tanzakia tuna mashabiki waswahili, full ushabiki wa mdomoni, kwenye mitandao ya kijamii, vijiwe vya kahawa huko ndiko wamejaa. Shabiki muulize mara ya mwisho kununua jezi lini?
Ubunifu
 
Taifa Stars na kamati za ushindi...
 
Back
Top Bottom