Wenzetu huko Mbele huwa wanahamasisha mashabiki waende uwanjani au mashabiki wana mapenzi na timu zao hata zikishuka Daraja?

Wenzetu huko Mbele huwa wanahamasisha mashabiki waende uwanjani au mashabiki wana mapenzi na timu zao hata zikishuka Daraja?

Hizo timu zenyewe Aiko wapi bongo mpira unachezwa kama wanalima kuwa serious mazee utapata shabiki wakati mpira hauna radha yaani timu daraja la sita uingereza inacheza mpira mzuri kuliko simba na yanga
 
Apart from UK labda na South America hata Europe especially sehemu kama Italy watu kwenda viwanjani sio kwa sana....

That said UK mpira ni part ya utamaduni na pass time tangia mtoto akiwa mdogo kwenda uwanja na wazazi family as pass time..., Ila nilishashauri tangia 2014 kuifanya Ligi ya Bongo kuwa a Better Product.., moja ya suggestion ilikuwa kuonyesha kila game kwenye Luninga (Ashukuriwe Azam kwa kufanya hili) Jingine ni kuhamasisha kuwe na timu regional zenye mashabiki na uhusiano na jamii husika...

 
Bongo uswahili ni mwingi sana, na bado sana hata kwenye ushabiki wa Mpira, tuna ushabiki mwingi wa mdomoni wa kubishana kwenye vijiwe vya kahawa na mitandao ya kijamii kama humu.

Emegine kwamba mashabaki wenye timu yao lazima wahamasishwe, gari izunguke mtaani watu wakikata mauno kwenye gari ili wahamasishwe waingie uwanjani imefika hatua tunasema fulani anajua sana kuhamasisha , fulani hajui.

Ujinga ujinga sana, full uswahili.

Kwamba wasipo hamasishwa basi uwanjani hawaendi kushabikia timu yao na hao hao utasikia wanasema ohoo hatukuhamasishwa, hamasa ilikiwa ndogo sana hivyo tukaona tusiende. Ujinga.

Wenzetu huko Mbele tunaona timu inavuruta mkia still mashabiki wanajaa uwanjani kuisapoti timu yao ya mwisho kwenye msimamo wa ligi, na timu inashuka Daraja wanashuka nayo, inapanda wanapanda nayo.

Bongo timu ikipigwa mechi mbili mfulukizo eti mashabiki uwanjani hawaendi au lazima wabembelezwe sana.

Hakuna mashabiki seriou wa mpira Tanzakia tuna mashabiki waswahili, full ushabiki wa mdomoni, kwenye mitandao ya kijamii, vijiwe vya kahawa huko ndiko wamejaa. Shabiki muulize mara ya mwisho kununua jezi lini?
Nadhani wewe ndiye mjinga kwa vile hujui uchumi wa mashabiki na uwezo wao kulipia mechi.
Pia ujue watu wana mapenzi na soka sio haya mambo timu zinafanya kuruka mageti sijui kutumia uchawi wa manara.Huu ndio upuuzi unasababisha watu wapunguze mapenzi na soka

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Hao michezo na burudani ni utamaduni wao ndio maana utaona mechi inachezwa saa tano asubuhi watu wanafurika uwanjani baada ya hapo wanaenda kwenye mbio za farasi wanajaa wakimaliza wanaenda kwenye tamasha la Robbie Williams Nako wanajaa wakija kulala wako hoi kesho yake wanaingia kazini wanafanya sana kazi hata hawasimuliani Nini kumetokea Jana🙌🙌🙌🙌
Wazungu ni mbwa kwa starehe ndio maana wa Afghanistan na WA Iran wanakimbilia ulaya astaghafulurahi
 
Eti mpaka Manara, Ali kamwe au Ahmed ally aje akuhamasishe ndio uje uwanjani. Mnawapa wajinga credit Sana hii nchi
 
Kwa vile tumeanza kuufanya mpira wetu uwe 'professional', huko mbele mambo yatabadilika, watu watapenda timu zao.
 
Msichojua ni kwamba mashabiki wengi hawafiki uwanjani kutokana na kipato kidogo.

Kuna watu kipato chao Kwa siku ni 5000 mpaka 6000 Tsh hapohapo boss ni mkali.

Mtu huyu ana mke na watoto.
Aende uwanjani akatoe 10000 au 5000 uwanjani inakuwa ngumu.

Hujiulizi mbona kukitangazwa bure watu wanajaa?

Lakini licha ya hiyo bure bado mtu ana kosa 3000 ya kwenda na kurudi mfano

Mbezi mwisho to Taifa.

Tanzania ni nchi yenye watu wenye maisha magumu mno sema tu wameridhika na kuzoea.

Mtu akienda karume hapo anarudi amependeza

Shati 3000/=
Suruali 5000/=
Raba 6000/=
Kapelo 2000/=
Saa 1500/=

Yaani huyooo keshapendeza , tena akiwa na buku 5 analewa na yeye kwani
Kuna pombe zinaitwa visungura ni buku mbili tu

Mkewe nyumbani ana vijora vingi tu havivuki bei ya 7000/= per pic.

Haya maisha wewe acha tu
Halafu kuna watu wanasema Mshahara wa laki nane Kwa mwezi mdogo hapo Hana mtoto Hana mke. Labda mnatetea

Degrees zenu
Mtu anapokea laki8 analia kwamba anahujumiwa😅😅
Maisha mtaani huku magumu nyie, sijui ndo yametudumaza ubongo kama wanavyosema! Ila kuna vitu watu wakilalamika huwa nawaangalia sana kuna jamaa mmoja nilimwambia kama Unaona ualimu unalipws kidogo acha kazi uje uraiani tupambane alinyamaza kimya.
 
Back
Top Bottom