Umeuliza swali muhimu sana na hii ni elimu kabisa. Wakati tukiwa shule tulifundishwa dhana ya 'Matawi ya familia' tukawataja babu, bibi, baba, mama, watoto hatukufundishwa zaidi ya hapo.
Sasa kwenye numeriolojia ndio kuna haya mambo ya matawi ya familia, huko unahesabu vizazi vinne unavijua historia ya wazaliwa wake wote hakika utafahamu ni mzaliwa yupi au wanagapi na wanani atakuwa kama vizaliwa wa kizazi kilichotangulia.
Sasa ukishafahamu hiyo elimu (ngumu kuielezea yote hapa), utaweza kujua kabisa kuwa wewe/mimi nipo kwenye kundi gani na nitakuwa na hatma ya aina gani, kutokea hapo ndipo.unapotakiwa sasa kuchukua hatua.kurekebisha mambo yasikukute.
Kuna watu wataoa na kuolewa na kisha wenza wao kufariki baada ya miaka michache hii.huwasio bahati mbaya bali huwa ni mzunguko wa matawi ya familia, ukimchunguza vizuri huyo mtu utakuwa kuna mtu kwenye kizazi chao naye alikuw hivyo hivyo.
Au unakuta kuna wanawake hawaolewi au wakiolewa hawadumu kwenye ndoa ukiwachunguza kwenye vizazi vinne vya familia yao utakutana na mtu wa sampuli hiyo hiyo.
Sasa basi ili kuepuka haya mambo ambayo huwa pia yanaitwa laana na mikosi ni wewe sasa kujitenga na mfumo wa vizalia vyenu. Kama huwa mnaoa watu wa kabila lenu wewe nenda kaoe mtu wa kabila tofauti tena awe na historua.tofauti kabisa ya kimalezi na ya kwako
Pia hama eneomlilozoea kuishi vizazivyenu, nenda mbali kabisabafili mfumo wa maisha, hata ikiwezekana usijiitekwa jina la ukoo wenu, jitenge kabisa na hayo mambo lazima utaanzisha kizazi tofauti kisicho na balaa za kwenu.
Ila pia kumbuka kuna faida na hasara za kufanya hivyo hasa hasa unaweza kupoteza yale mazuri yanayobebana na mfumo wenu. Hivyo ni swalala kuzingatia pia kabla ya kuchukua maamuzi.