Mpapatu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 221
- 119
Habari ya muda huu wana jukwaa. Nimejaribu kulinganisha sebene za wasanii mbalimbali hasa kutoka DRC nikaona werrason sebene zake zinakimbiza ile mbaya, mfano Kata fumbwa, mipende na mzigo unaosumbua hivi sasa block cadena.
sebene zake zina mvuto flani amazing halafu kwenye block cadena ametokelezea traditionally na kufanya muziki wake uwe wa kiafrika zaidi.
Vile vile kuna wakali wengine ambao wanasumbua kwa sebene mfano Koffi Olomide na Bebi Phillip wa Cote d'ivoire.
Hii Nyimbo ina Muda inaelekea Kutimiza Mwaka, sasa amini usiamini Jamaa hajawahi kosea na Juzi kati alichukua vijana Wawili Wa Ferre Gola na Wakashindwana ila jamaa hajatetereka.