20PROFF
JF-Expert Member
- Nov 5, 2013
- 8,186
- 7,184
Mkuu umeongea facts sana hata.....ingawa radha zina badilika kizazi kwa kizazi.Siku nyingine uwe unafanya Kwanza Utafiti wa kutosha kisha ukitosheka na findings zako ndipo uwe unakuja nazo humu JF na siyo kukurupuka kama hivi ulivyofanya hadi wenye muziki Wetu wa Congo na ambao ndiyo umetukuza tunakushangaa.
Kwa taarifa yako tu ni kwamba ukiwaondoa akina Hayati Luanzo Makiadi Franco ' Le Grand Mitre ' na mwenzake Kabasele ya Mpanya Pepe Kalle mpaka sasa Congo DR ( zamani Zaire ) ni Bendi moja tu ambayo ndiyo Bingwa wa Masebene nayo ni Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana na wanaoifuata kwa karibu ni hili Kundi la Extra Musica BPBL baadae wakajiita Extra Musica Zangul na sasa wanajiita Extra Musica Oureguen chini yake Ibambi Ikombi wengi mnamjua kama Roga Roga ( Bingwa wa kupiga Solo guitar Congo Brazzaville ) na wanaofuatia kwa mbali sana ni Bendi ya Felix Wazekwa.
Kuna Vigezo vikubwa Saba vya kuifanya Bendi fulani isifike na ikubalike kuwa mahiri katika Sebene nazo ni :
Kwa hivyo Vigezo au Sifa Kuu saba ( 7 ) hapo juu huyo Ngiama Makanda Noele Werrason wako anaachwa kwa mbali mno na hao wenzake Watatu ( 3 ) niliowataja hapo.
- Best Soloist ( Mpiga Solo gitaa mahiri sana )
- Best drummer ( Mkaanga Chips mzuri au mpiga ngoma mzuri )
- Animateurs ( kwa Kiswahili mnawaita Marapa au Waghani na kwa Kikongo wanaitwa Atalakus )
- Catchphrase ( kibwagizo au kiitikio ambacho kimekubalika na kimewakaa Watu kwa sana )
- Creative Dancers with Creative dancing styles ( Wacheza Shoo Wabunifu )
- Entertaining Keyboardist ( Mpiga Kinanda anayeburudisha kwa vionjo vinavyoendana na wimbo upigwao )
- Energy ( Nguvu ya kutosha hasa kwa kuimba na kucheza bila kuchoka )
Ila haoo ulio wataja juuu ni ma legend , niwape heshima yao...IGWEEEEEE.
Ila kwa kizazi hiki WERRASON anajitahid ku recruit watu makini kidogo.
Ndiio maana kama wakin JB huchukia wapiga drum, dancerz etc kwa Werrason.
Upo makini mkuuu......
[HASHTAG]#kuna[/HASHTAG] ngoma GEN.DEFAO COMPINASH,BANA CONGO , SALANOKI Niangushie mkuu kama zipo kwa device yako