Werrason kiboko ya sebene


Hii Nyimbo ina Muda inaelekea Kutimiza Mwaka, sasa amini usiamini Jamaa hajawahi kosea na Juzi kati alichukua vijana Wawili Wa Ferre Gola na Wakashindwana ila jamaa hajatetereka.
 
Hamna kitu hapo kwenye block cardena, ukitaka kujua hili sikiliza Power 001 ya Fally Ipupa iliyotoka 2013. Jamaa kaiga theme hadi baadhi ya midundo. Kwa mkongwe kama Wera, hapa alijishusha kwa kudokoa wimbo wa kijana Fally Ipupa 'asali ya warembo'. Zaidi ya zile sebene za Zenith, bado sijaona.
 

Siku nyingine uwe unafanya Kwanza Utafiti wa kutosha kisha ukitosheka na findings zako ndipo uwe unakuja nazo humu JF na siyo kukurupuka kama hivi ulivyofanya hadi wenye muziki Wetu wa Congo na ambao ndiyo umetukuza tunakushangaa.

Kwa taarifa yako tu ni kwamba ukiwaondoa akina Hayati Luanzo Makiadi Franco ' Le Grand Mitre ' na mwenzake Kabasele ya Mpanya Pepe Kalle mpaka sasa Congo DR ( zamani Zaire ) ni Bendi moja tu ambayo ndiyo Bingwa wa Masebene nayo ni Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana na wanaoifuata kwa karibu ni hili Kundi la Extra Musica BPBL baadae wakajiita Extra Musica Zangul na sasa wanajiita Extra Musica Oureguen chini yake Ibambi Ikombi wengi mnamjua kama Roga Roga ( Bingwa wa kupiga Solo guitar Congo Brazzaville ) na wanaofuatia kwa mbali sana ni Bendi ya Felix Wazekwa.

Kuna Vigezo vikubwa Saba vya kuifanya Bendi fulani isifike na ikubalike kuwa mahiri katika Sebene nazo ni :

  1. Best Soloist ( Mpiga Solo gitaa mahiri sana )
  2. Best drummer ( Mkaanga Chips mzuri au mpiga ngoma mzuri )
  3. Animateurs ( kwa Kiswahili mnawaita Marapa au Waghani na kwa Kikongo wanaitwa Atalakus )
  4. Catchphrase ( kibwagizo au kiitikio ambacho kimekubalika na kimewakaa Watu kwa sana )
  5. Creative Dancers with Creative dancing styles ( Wacheza Shoo Wabunifu )
  6. Entertaining Keyboardist ( Mpiga Kinanda anayeburudisha kwa vionjo vinavyoendana na wimbo upigwao )
  7. Energy ( Nguvu ya kutosha hasa kwa kuimba na kucheza bila kuchoka )
Kwa hivyo Vigezo au Sifa Kuu saba ( 7 ) hapo juu huyo Ngiama Makanda Noele Werrason wako anaachwa kwa mbali mno na hao wenzake Watatu ( 3 ) niliowataja hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…