Werrason kiboko ya sebene

Mkuu umeongea facts sana hata.....ingawa radha zina badilika kizazi kwa kizazi.

Ila haoo ulio wataja juuu ni ma legend , niwape heshima yao...IGWEEEEEE.

Ila kwa kizazi hiki WERRASON anajitahid ku recruit watu makini kidogo.

Ndiio maana kama wakin JB huchukia wapiga drum, dancerz etc kwa Werrason.


Upo makini mkuuu......

[HASHTAG]#kuna[/HASHTAG] ngoma GEN.DEFAO COMPINASH,BANA CONGO , SALANOKI Niangushie mkuu kama zipo kwa device yako
 
hahahaha wacongo watu wa mapenzi tu
Tafuta ngoma za fally, etc then huwe na musix match app, inayo tafsiri...

Utasikia watu wanavyo lalamika.

[HASHTAG]#mtu[/HASHTAG] anakwambia hata nikinywa bia silewi, huh
 

Akhsante na tupo pamoja Mkuu.
 
Binafsi namkubali sana Werrason kwa kuibua vipaji vipya, tofauti na Mpiana na Koffi Le Grand Mopao, nakumbuka alipoanza na Maison Mere ile ya kwanza kabisa ya akina Ferre golla, GDT Mulopwe, Bill Macintosh, Celeo Scram, Ndombe Luatero, Ajeje Ajan, Chalz Mabila, mpiga solo maarufu Japone Maladi, na mpiga drums ambae mpaka leo bado yupo nae aitwae Sebondo, na wakina Didier Lacoste, na wengine wengi,
Binafai nilidhani baada ya hili kundi kuvunjika nilijua Werrason asongeweza kusimama tena, lakini chakushangaza aliunda kundi jipya lililokuja na wasanii chipukizi wenye vipaji vya kiwango cha juu sana na kuziba mapengo yalioachwa kana kwamba hapakua na mapungufu yoyote kwenye kundi, alichukua vijana wachanga kama akina, Heritier Wataplus japo huyu no kijana aliemlea mwenyewe, pamoja na akina Deplic, Fabrigas, Tadet, Capuchino, Caferum,Olivier, na wengine wengi ambao walikuja kua tishio baada ya kuwapika vizuri, Kwa hiyo kwenye suala la kuandaa vipaji yupo vizuri sana, japo ana mapungufu kwenye ubora wa tungo hawafikii JB mpiana na Ferre, japo Fere ni kijana aliyempika mwenyewe kwa kiasi kikubwa,
 

Mkuu GENTAMYCINE nilikuwa nasuburua mchango wako ktk hili maana nakujua wewe ndio unaujua vizuri mziki huu..
Kuna seben moja la Werrason kuna mdada mmoja anapiga SOLO Gitaa LIve on stage sijui kama umeishaiona ile video..
au kama vp ntaitupia uione.
 
WERASON NI NOMA KWA MASEBENE, WALE WAPIGA DRUMS WAKE WAMEENDA SHULE HATARI

Huyo mpiga drums wa Werrason aitwae Papii Kakol bado ana mengi sana ya kujifunza kutoka kwa Mpinzani wake mkubwa mpiga drums wa Wenge Musica BCBG aitwae Seguen Mignon Maniata a.k.a Maniata Ikuzu. Ukitaka uliamini hili tafuta Video clip ya angalau tu Masebene kadhaa ya Werrason na JB Mpiana ujionee mwenyewe. Hata hivyo ninamuheshimu mno huyo Mpiga drums Papii Kakol kwani kiukweli anatishia maisha kiasi kwamba anamfanya kila siku Seguen Mignon Maniata awe mbunifu ili asipitwe nae.
 

Yap namfahamu anaitwa Sarah Solo na kiukweli huyo Dada sasa anaanza kutishia amani kwa mpiga Solo Kiongozi wa Bendi ya Wenge Musica Maison Mere ya Werrason aitwae Flam Kapaya. Wakongo tuwaache tu jamani!
 
Ah Sarah Solo amekuwa mentored na Vieux Lutumba Simaro akahamia Ivory Coast na mwezi huu ndiye habari ya KIN.
 
kuna zile drum zilipigwa kwenyee LELE LELE LELE ni noma
 
DANCE BIBICIA live at zenith, huyu mdada wa werrason ni balaa kwa jnsi anvokta ilo uno...bonge moja ya sebene la le grande mopao
 
Yap namfahamu anaitwa Sarah Solo na kiukweli huyo Dada sasa anaanza kutishia amani kwa mpiga Solo Kiongozi wa Bendi ya Wenge Musica Maison Mere ya Werrason aitwae Flam Kapaya. Wakongo tuwaache tu jamani!

Sawa mkuu nimekupata....kwa kuongezea hivi yule dancer BIBICIA yupo wapi siku hizi, bado anacheza...mimi ile ZENITH Mpaka bado naitazama.
 
Mm naikubali sana ibracadabla kuna vtu adim balaaa
 
Sawa mkuu nimekupata....kwa kuongezea hivi yule dancer BIBICIA yupo wapi siku hizi, bado anacheza...mimi ile ZENITH Mpaka bado naitazama.

Bibicia nasikia kwa sasa kasimama Kimuziki. Tatizo kubwa la Bibicia kila Bendi anayokuwepo kuanzia Wenge ya JB Mpiana, Koffi Olomide na Wenge ya Werrason amekuwa haelewani vizuri na Dancers wenzake kwani anapenda sana ukubwa huku akiwa anawadharau wenzio hali ambayo imepelekea kila Bendi anayokuwepo achukiwe na wenzake kitu ambacho huwa kinamuathiri sana Kiutendaji. Ila ni Dancer mahiri mno ambaye umwonapo stejini utatamani mziki usiishe ili tu uwe unamwona jinsi anavyojua kuuchezea na kuutumia mwili wake mzuri.
 

Shukrani mkuu ..nimekupata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…